Jaggi Vasudev (Sadhguru): Maisha yake, mafunzo yake na changamoto ya walimwengu hasa wasomi wetu, sisi vijana na wanasiasa

Jaggi Vasudev (Sadhguru): Maisha yake, mafunzo yake na changamoto ya walimwengu hasa wasomi wetu, sisi vijana na wanasiasa

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2020
Posts
12,077
Reaction score
12,786
Jaggi Vasudev (Sadhguru) ni mwalimu wa yoga, mtunzi wa vitabu na public speaker huko nchini India.

Mtu huyu mwenye busara na kipawa kikubwa cha utulivu alichopewa na Mungu Mwenyezi anatufundisha mengi walimwengu.

Amekuwa akialikwa kwenda kutoa midahalo sehemu mbalimbali ulimwenguni.

Kwa anayetaka kumfahamu zaidi amtafute online atampata.

Kikubwa ninachotaka kuwapendekezea wanaJF kumsoma mtu huyu ni yale mafundisho yake mepesi ambayo hayafungamani na dini zetu ila yenye lugha nyepesi katika kutafsiri mambo mengi duniani hata mazuri ya imani zetu zozote zile.

Kwa mfano amekuwa akiongelea kuwa mwanadamu anapojitambua ya kwamba yeye binafsi hajui na hafahamu vitu(ignorant) basi ndio mwanzo wa utulivu kwake na hata kwa wenzake.

Sadhguru amekuwa akisema ya kwamba mwanadamu anavyozidi kujua vitu vingi na kutambua kuwa anajua. Ndio mwanzo wa kuvimbiwa(ujuzi mwingi) na kuanza kutotaka kuthamimi asiyoyajua.

Sadhguru amekuwa akifundisha usawa wa viumbe kama wanyama na wadudu,kwa kusema kuwa wote hao ni sawa na hakuna mbora zaidi ya mwingine. Yaani tembo si mbora zaidi ya sisimizi kwani wote ni viumbe waliojikuta wako ulimwenguni na hawajui watokako wala waendako na hawajajiumba sembuse binadamu?

Anamuongelea binadamu kama kiumbe aliofinyangwa na kuumbwa hivyo alivyo kwa nature kumpa uwezo mkubwa zaidi ya wengine ila haina maana yeye ana thamani kubwa zaidi ya viumbe wengine(hapa mnaweza mkampinga kwa kutumia maandiko ya vitabu vyenu vya kiimani).

Kwa kufupisha maneno,sadhguru anatukumbusha kuwa wale wanaojifanya wanajua sana zaidi ya wengine ndio wanaotengeneza migongano, umaskini, chuki, ubaguzi, migogoro, maonevu, dharau, kedi, kebehi, dhulma na umwagaji damu popote walipo....Ima

1. Familiani

2. Makazini

3. Mashuleni na vyuoni

4. Nyumba za ibada

5. Siasani

6. Uongozini

7. Mitaani

8. Biasharani.

Sadhguru anatukumbusha kuwapa viumbe na mazingira yatuzungukayo attention kubwa. Hakika tutauona mwanga wa maisha na kuifanya nchi na dunia kuwa mahali bora zaidi kwa kila mmoja wetu(wadudu,wanyama na sisi binadamu).

Jumbe brown.

Kijana muuza Al kasus

Tandale kwa Mtogole.
 
Sawasawa ana utambuzi wa hali ya juu Sana inaonekana anapenda kuongea mambo ya Mungu nitamfuatilia mtandaoni.wahindi na wa Pakistan nawakubaligi Sana na kina yesu na kina mtume wote hawana shida.
 
Sawasawa ana utambuzi wa hali ya juu Sana inaonekana anapenda kuongea mambo ya Mungu nitamfuatilia mtandaoni.wahindi na wa Pakistan nawakubaligi Sana na kina yesu na kina mtume wote hawana shida.
Swadakta Mkuu....

Utamfaidi HASWA!

Kudos!!
 
Nimejifunza mambo mengi sana kutoka kwa huyu Mzee. Napenda kumsikiliza kila mara. Ana hekima na busara za hali ya juu mno.
 
Sandguru anasema maisha ni vile unavyoyatafsiri kwahiyo tafsiri yoyote ya maisha ni sawa [emoji23]..
Nmemsikilizaga sana mpaka vitu vingine sikumbuki haki
 
Back
Top Bottom