Jombaa, tuwe wakweli bana. Njagua ni mtu ovyo kupindukia, matamshi yake ya kichonganishi kando, kwenye uongozi ni zero! Kilichombeba ili akachaguliwa ni chama cha Jubilee tu na pia alivyolia baada ya kuchezewa rafu na aliyekuwa mbunge wa Starehe Maina Kamanda. Kwenye shughuli za 'nominations' za wagombea ubunge wa chama cha Jubilee. Jamaa anatuangusha sana kama vijana, mara sijui wapigane makonde na kinyangarika mwenzake Babu Owino wa ODM. Alafu ndio yeye huyu tena na chuki dhidi ya wageni. Umemsikia hata siku moja akiongea bungeni kuhusu masuala yanayohusu vijana wenzake? Watu wa eneo bunge la Starehe watajuta kutompigia kura Boniface Mwangi 'Boni Boni', mkenya halisi, kijana jasiri, kiongozi natural na mtu mwenye maono makubwa kwa nchi yetu tukufu ya Kenya. Watz nawaombeni wajameni, huyu lofa akitia mguu wake Tz, piteni na shingo!.