Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Jaji awashauri waliomshtaki Askofu Kakobe kuondoa kesi
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 02 August 2011 20:13 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
James Magai
JAJI wa Mahakama Kuu, Augustine Shangwa, amewashauri wachungaji wanaomshtaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe, wakatafari upya juu ya madai yao kuona kama yana msingi na wanapaswa kuendelea nayo.Wachungaji hao wanaodai kuwa ni wa kanisa hilo, ni Dezedelius Patrick, Angelo Mutasingwa na Benedict Kaduma, wamemfunguliwa Askofu Kakobe kesi wakimtuhumu kwa matumizi mabaya ya fedha za kanisa yanayokadiriwa kufikia Sh14 bilioni.
Kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo jana, Jaji Shangwa aliwashauri walalamikaji hao kutafakari madai yao na ikiwezekana wayaondoe mahakamani.Pia, Jaji Shangwa aliwatahadharisha kuwa iwapo wataamua kuendelea nayo na katika uamuzi wa mahakama, wakishindwa watajuta kwa sababu watatakiwa kumlipa Askofu Kakobe fidia kubwa na gharama za uendeshaji kesi, ambazo hana hakika kama watamudu.
Kabla ya kuwashauri walalamikaji hao, Jaji Shangwa alianza kwa kuonyesha wasiwasi wake juu ya msingi wa madai ya walalamikaji kuhoji matumizi ya fedha za kanisa hilo.Alisema kwa mfumo wa FGBF, Kakobe ndiyo kanisa na kwamba mapato ya kanisa hilo ni mali ya Kakobe kwa sababu, kanisa hilo alilianzisha mwenyewe na kuhoji iweje wamhoji mtu anayetumia mali yake.
Kwani ni nani alimpa Kakobe uaskofu? Kakobe alijifanya mwenyewe, ni tofauti na maaskofu wa Katoliki ambao mpaka waende wakasomee;
Msiniambie nina-prejudge (nihukumu kabla), maana huwa mnatulaumu kesi kurundikana mahakamani. Mimi hapa natafuta suluhu na suluhu ni pamoja na kuondoa kesi mahakamani, alisema Jaji Shangwa.
Jaji Shangwa alihoji kosa la Kakobe kukusanya michango kutoka kwa wanajumuia na kwenye mikutano ya mahubiri anayofanya nchi mbalimbali, kujengea nyumba yake kama walalamikaji wanavyodai.
Lakini si anatumia fedha zake? Mimi najiuliza maana ndiyo alianzisha kanisa, kama kulikuwa na wafadhili ndiyo akawafundisha nanyie mkawa wachungaji;
Hizi fedha hapewi na serikali ni za wale anaowatibu na wanaokuja kuombewa mapepo. Kwa hiyo anazikusanya kwa huduma, sasa mtamuulizaje na chake?;
Labda mngesema kuwa hawapi au anawapunja mshahara wakati mnashinda kanisani mnaombea mapepo, maana hii ni kazi kubwa, alihoji Jaji Shangwa.
Hata hivyo, Jaji Shangwa aliwataka walamikaji hao kujibu pingamizi lililowekwa na Kakobe dhidi yao, Septemba 5, mwaka huu kesi hiyo itakapoendelea.
Kakobe kupitia kwa Wakili wake, Miriam Majamba, anapinga walalamikaji hao hawana hadhi ya kisheria kumshtaki kwa kuwa siyo wachungaji wa kanisa hilo, kwani walishafukuzwa uchungaji hivyo hawana mamlaka ya kuhoji jambo lolote linalohusiana na kanisa hilo.
Wakati Kakobe akiwawekea pingamizi hilo, walalamikaji nao juzi waliwasilisha maombi mahakamani wakiomba mahakama isipokee maelezo ya utetezi wa maandishi ya Kakobe kwa kuwa yamewasilishwa nje ya muda wa siku 21 kisheria.
Katika kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2011, ilifunguliwa na wachungaji hao Juni 21, wakiorodhesha tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya fedha za kanisa hilo yanayofanywa na Kakobe na kwamba, amekuwa akikiuka Katiba ya kanisa hilo.
Wanadai Sh10 bilioni zinazodaiwa kutumika kwa ujenzi wa eneo la kanisa na Sh800 milioni zinazodaiwa kutumika kuanzisha kituo cha televisheni. Pia, wachungaji hao wanamshutumu Askofu Kakobe kwa kutoitisha mkutano mkuu wa kanisa hilo tangu mwaka 1989.