Jaji Bomani umenena:CCM waachane na wazo la Serikali 2

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
2,638
Reaction score
1,218
Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Boman amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuachana na msimamo wake wa muundo wa Serikali mbili na kwamba, wawaachie wananchi waamue.

Pia, Jaji Bomani alisema anasikitishwa na madai yanayoelezwa na baadhi ya viongozi, tena anao waheshimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ni muumini wa Serikali tatu kwamba ni upuuzi, kwani yeye siyo wa kwanza kutaja muundo huo.

Licha ya hilo, alisema anashangazwa na baadhi ya viongozi kuwa rasimu imekwenda kinyume cha matakwa ya waasisi wa Tanzania na kwamba, kama hali inalazimu kubadili uamuzi unafanyika.

Akitoa maoni yake kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba, Jaji Bomani alisema licha ya kwamba yeye ni mwanaCCM, anaona Serikali tatu ni muhimu kwani ndiyo suluhisho la migogoro ya Muungano.

Alisema amekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1960, lakini hajatetereka ingawa wakati mwingine amekuwa haridhiki na baadhi ya mambo.

“CCM ni chama tawala, chenye wanachama wengi kuliko chama kingine cha siasa, hivyo ina jukumu la kutoa uongozi na kuacha baadhi ya mambo wananchi waamue,” alisema Jaji Bomani na kuongeza:

“Nikisikia kitu kama wanaCCM kulishana kiapo ili wapinge Serikali tatu nafadhaika sana. Haya yote ya nini! Waachieni wanachama wenu waamue wanachokitaka kuliko kuwashinikiza kufanya uamuzi mnaotaka nyie.”

Alisema kazi ya chama ni kutoa ushauri na ushawishi, siyo kutoa shinikizo hivyo ni vyema kuacha kuwa na msimamao wa Serikali mbili, kwani kilichopendekezwa na Tume ndiyo sahihi.

Jaji Bomana alihoji kama CCM ilitaka Serikali mbili, iwapo waliwahi kuwapa wanachama wao elimu juu ya muundo huo.

“Itakuwa siyo uongozi bora kwa wana CCM kushinikiza kupigia kura mfumo wa Serikali mbili kwa namna ya vitisho. Nashauri wanachama na wananchi waachiwe uhuru bila kushinikizwa na mtu,” alisema Jaji Bomani.

Souce: Mwananchi






 
Je, chama cha Magamba CCM wataelewa somo hili toka kwa Jaji Bomani ambaye ni mkongwe wa Siasa na Mwanasheria wa kwanza wa Tanganyika??

Kweli CCM ni magamba ya chuma ambayo hayawezi kuvuliwa labda mpaka kwa shoka kama alivyodai kada wao wa CCM almaarufu Mzee wa Vijisenti!!!! Kama Tume ya Katiba mpya chini ya Jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba imepokea mapendekezo ya Watanzania kuwa wanataka Serikali 3 kwanini CCM wanang'ang'ana na Serikali 2???Nini agenda ya CCM kutaka serikali 2????

Ama kweli Sikio la kufa halisikii dawa!!!
 
Nangoja naye wamfukuze kama walivyomfukuzilia mbali yule Mkhojani.
 
sijui kwa nini watu wengine wakizeeka wanakuwa wasemaji sana hii ni mifano tosha kwa huyu mzee bomani na mwenzake slaa.
 

mkuu siasa haina ukongwe kwa sababu hubadilika kulingana na wakati kila jambo na wakati wake mkuu huzi zama siyo zile za kipindi kile acha habari zako kabisa.
 
Dar es Salaam.

Alisema amekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1960, lakini hajatetereka ingawa wakati mwingine amekuwa haridhiki na baadhi ya mambo.

Jamani wale wenye kumbukumbu vizuri naomba mnikumbushe. Hivi CCM imezaliwa mwaka gani?
 
Jana niliiona Tanzania hamna wasomaji. Mtu anaenda kwenye malumbano ya hoja hajasoma hata draft ya katiba anauliza eti huo mpka wa Tanganyika utakuwa wapi na Rais wa Tanganyika akiamua kuwa na jeshi lake wakati majibu yote hayo, yapo kwenye draft ya katiba.Na aliyekuwa anauliza hayo ni msomi wa Chuo cha Mwlmu Nyerere.Huyo mtu basi angesuggest basi kuwe na serikali 1 wameng'ang'ania mbili hawajui kuwa tume ya kutatua mambo ya muungano toka zianzishwe hamna cha maana na watu wengi walienda pale walikuwa hawajui Zanzibar wamevunja vipengele vingi vya katiba ya muungano wawo kuwa na katiba yao.
Mtu kajazwa maneno pale tena kwake anajiita baba anashikishwa kitu kichwani bila kutafakari.
 

Akili za akina Bomani, Warioba, Salim, na wachache walioachwa na Mwl Nyerere ndio akili pekee zilizobakia CCM! Yeliyobaki mengine ni Mizigo, Mavuvuzela, Magamba yaliyogandiana ufisadi, yamejaa ubinafsi na woga wa kuachia wanachi wapate elimu wafanye maamuzi yao sahihi....!

Mzee Bomani kawapa swali rahisi kabisa 'CCM mnaojidai sera yao Serikali mbili...Je mlishawahi kuwapa wananachi hata elimu kuhusu huo muundo wa Serikali mbili ambao ndio sera yenu...'? Jibu ni HAPANA! HAPANA! HAPANA! ...Sasa elimu hawajawahi kutoa na sasa wanaweweseka kuvuruga Serikali tatu ambayo wananchi wanaelimishwa na kuelewa kwa zaidi ya 80%....! CCM imefilisika kwa kila wigo! Kisera, Kiuongozi, Kimaadili na kidira...ndio maana kila pahala ni zogo dhidi ya CCM! WAANCHIENI WANANCHI WAAMUE WAO, NCHI ISONGE MBELE!
 

Ndio uzuri wa CCM mwanachama anaruhusiwa kukosoa msimamo wa chama bila kuonekana msaliti........ikiokea leo Chadomo mtu akaja na wazo tofauti ghafla atageuka msaliti na mhaini.....wakati wa mchakato wa kutengeneza rasimu ya katiba Prof.Baregu aliwashushua CDM pale Slaa alipomshinikiza ajitowe kwenye tume na akawaambia 'anachagua kuitumikia nchi na sio chama' Kina Slaa/Mbowe waliaibika sana na leo Rasimu imekuwa nzuri sasa wanatokwa povu..............sasa wanalalamika muda wa katiba mpya ni mdogo wakati Slaa aliahidi katiba mpya ndani ya siku 100.......hawa ni vichaaaaa!
 
Watatafutana na kumalizana mashetwain wakubwa hao........... yetu Macho
 
Watatafutana na kumalizana mashetwain wakubwa hao........... yetu Macho
 

- Sasa look huyu ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mwalimu, alipokuwa hai Mwalimu hatukusikia huyu wala Warioba wakidai Serikali Tatu wote walifyata mikia sasa Mwalimu hayupo ndio wanajifanya wana akili sana za namna ya kutusaidia Tanzania kwani alipokuwa Serikali kilichomshinda kulilia Serikali Tatu ni nini hasa mpaka aje alilie leo amepitwa kabisa na wakati? I mean anaongea nonsense kwa sababu kama anajua uamuzi ni wananchi angesema maoni yake tu kuhusu the ishu lakini sio kujifanya anwaongelea wananchi wote kwa sababu hana nafasi yoyote ya kuchaguliwa na wananchi kwamba ana uhalali wa kuwazungumzia Serikali TaTU,

- Halafu hawa wazee ninapata taabu sana kuelewa elimu zao I mean ni mtu gani mwenye akili timamu anaweza kulilia Serikali Tatu? ni wapi kuna Serikali Tatu na kuna maendeleo ambayo hawakuwa nayo kabla ya kuwa na Serikali Tatu? Muungano wa sasa una matatizo yes yanatakiwa kutatuliwa sio kukimbiwa na visingizio vya Serikali Tatu, kama alijua kwamba Serikali Tatu ndio the way alipokuwa Serikalini tena Mwanasheria Mkuu mbona hakusema wala kulia lia kama anavyofanya sasa?

- Yeye ni mwananchi tu kama wengine anachotakiwa kufanya ni kusema maoni yake tu lakini sio kutisha Serikali na CCM, hapana CCM kama chama kuna haki kikatiba ya kusimia maamuzi na misimamko yake, hawa watu ni wa kuwapuuza na ni hatari sana kwa Taifa, ninasema hivi Kiongozi yoyote aliyekuwepo under Mwalimu na hakusema kitu kuhusu Serikali Tatu then ni bora wakanyamaza ninaweza kuelewa leo Kasaka Njelu akisimama na kusema anataka Serikali Tatu lakini sio hawa wanafiki!!

Le Mutuz
 
sijui kwa nini watu wengine wakizeeka wanakuwa wasemaji sana hii ni mifano tosha kwa huyu mzee bomani na mwenzake slaa.

Chama kipya cha desmond tutu? maana kila uzi lazima uje na lopolopo, Dr. Slaa anahusika vip hapa?
 
Nyerere alikuwa anafanya kazi na watu ambao hawana imani nae, wote wamemgeuke,ni ishara tosha kwamba either walikuwa wanafiki au nyerere alijiwekea mazingira ya kuwa na washauri wanafiki
 
Wee ni kichwa maji kweli, wakati wa nyerere kulikuwa hakuna migogoro mingi ya muungano kama leo hivyo basi mahitaji ya Serikali Tatu yalikuwa siyo makubwa kama leo hii, ukitaka ujue Serikali mbili ni tatizo kuwe kuna Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ifutwe kimya kimya kama ilivyofutwa Tanganyika kwa miaka Mingi
 
hahahahaha! Each case shoud be decided on its own merits because there is no simmilarities of facts...as per Lord Denning as he then was.....
 
Serikali 2si ndio ziko ss hivi ambazo ni usanii mtupu? Tunataka Tanganyika yetu kama Zanz. walivyopewa Zanzibar yao.
 

- Kichwa cha maji huwa kinajisema chenyewe kaka, huyu bomani ni mnafiki asingekuwa angesema enzi za MWalimu, wale wote ambao hawakusema then wanyamaze wamuchaie Kasaka Njelu aseme!1

Le Mutuz
 
Nyerere alikuwa anafanya kazi na watu ambao hawana imani nae, wote wamemgeuke,ni ishara tosha kwamba either walikuwa wanafiki au nyerere alijiwekea mazingira ya kuwa na washauri wanafiki

- Wanafiki na besides leo 2014 hatuwezi kuamuliwa maamuzi na watu walioongoza wakati hatujazaliwa man, enough!!

Le Mutuz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…