Jaji Bomani umenena:CCM waachane na wazo la Serikali 2


Umetoka nje ya mada kabisa. Ni busara kujadili hoja ya Mhe. Mark Bomani. Sasa Pagija you are out of scope, na haya ni matatizo ya watu wanaojadili watu badala ya hoja. Hahahahahaaaa
 

Le Mutuz, heshima haiuzwi dukani, it is costless. Kwanini hueshimu wazee kama Mhe. Mark Bomani? Huyu ni kama mzazi wako jamani. Tatizo lako Le Mutuz unatafuta huruma ya uteuzi kutoka ndani ya CCM kitu ambacho huwezi pata kwa sababu ya mapungufu uliyonayo kuhusu misingi thabiti ya kujenga taifa. Bahati mbaya sijui kiwango chako cha elimu lkn hata hivyo kwa kupitia makala zako mbalimbali kwenye social media zinakuonesha uwezo duni wa kufanya tafakuri za maana kwa maendeleo na amani ya taifa letu.
 

vipi na wewe umeshakula kiapo cha kupinga serikali 3???
 
Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Boman amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuachana na msimamo wake wa muundo wa Serikali mbili na kwamba, wawaachie wananchi waamue.
Pia, Jaji Bomani alisema anasikitishwa na madai yanayoelezwa na baadhi ya viongozi, tena anao waheshimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ni muumini wa Serikali tatu kwamba ni upuuzi, kwani yeye siyo wa kwanza kutaja muundo huo.
Licha ya hilo, alisema anashangazwa na baadhi ya viongozi kuwa rasimu imekwenda kinyume cha matakwa ya waasisi wa Tanzania na kwamba, kama hali inalazimu kubadili uamuzi unafanyika.
Akitoa maoni yake kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba, Jaji Bomani alisema licha ya kwamba yeye ni mwanaCCM, anaona Serikali tatu ni muhimu kwani ndiyo suluhisho la migogoro ya Muungano.
Alisema amekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1960, lakini hajatetereka ingawa wakati mwingine amekuwa haridhiki na baadhi ya mambo.
“CCM ni chama tawala, chenye wanachama wengi kuliko chama kingine cha siasa, hivyo ina jukumu la kutoa uongozi na kuacha baadhi ya mambo wananchi waamue,” alisema Jaji Bomani na kuongeza:
“Nikisikia kitu kama wanaCCM kulishana kiapo ili wapinge Serikali tatu nafadhaika sana. Haya yote ya nini! Waachieni wanachama wenu waamue wanachokitaka kuliko kuwashinikiza kufanya uamuzi mnaotaka nyie.”
Alisema kazi ya chama ni kutoa ushauri na ushawishi, siyo kutoa shinikizo hivyo ni vyema kuacha kuwa na msimamao wa Serikali mbili, kwani kilichopendekezwa na Tume ndiyo sahihi.
Jaji Bomana alihoji kama CCM ilitaka Serikali mbili, iwapo waliwahi kuwapa wanachama wao elimu juu ya muundo huo.
“Itakuwa siyo uongozi bora kwa wana CCM kushinikiza kupigia kura mfumo wa Serikali mbili kwa namna ya vitisho. Nashauri wanachama na wananchi waachiwe uhuru bila kushinikizwa na mtu,” alisema Jaji Bomani.

Source: Mwananchi:israel:
 
Imechanika wapi mkuu mgongoni au kifuani weka picha tuoni jinsi ilivyochanika.
 
Mzee bomani kwani kasahau nini hawa wazee wakae na wajukuu home watuache.
 
Well said Judge Bomani.
Ukiona mtu hakuelewi ujue kalishwa yamini.
 

- Kaka kwa elimu niliyonayo nikihisi elimu yako ni duni sina sababu ya kukujibu maana kwa wenye akili nitaonekana nina elimu duni kama yako, hoja yangu ni kwamba Mzee Bomani alitakiwa kutoa maoni yake tu lakini sio kuwazungumzia wananchi wa Tanzania ambao hawajawahi kumchagua katika nafasi yoyote ile, naomba kujua hoja yako msomi mzito ni nini on this?

Le Mutuz
 

Magamba ni viumbe wa jabu sana--eti wanadai kwamba mfumo wa serikali 3 haupo kwenye katiba ya CCM!! Yaani wanashindwa kutofautisha kati ya katiba ya NCHI na katiba ya CCM!!! Hawa magamba watakuwa wamerogwa, sio bure!
 
Magamba ni viumbe wa jabu sana--eti wanadai kwamba mfumo wa serikali 3 haupo kwenye katiba ya CCM!! Yaani wanashindwa kutofautisha kati ya katiba ya NCHI na katiba ya CCM!!! Hawa magamba watakuwa wamerogwa, sio bure!

- Sasa kaka na wewe mbona unatoa mpya, CCM si ina Katiba yake na Serikali ina Katiba yake na Chadema ina katiba yake, au?

Le Mutuz
 
- Wanafiki na besides leo 2014 hatuwezi kuamuliwa maamuzi na watu walioongoza wakati hatujazaliwa man, enough!!

Le Mutuz

wewe kichwa chako lazima kitakuwa na wadududu, sio bure! serikalh 3 ni maoni ya wananchi, sio maoni ya warioba, dr slaa, mbowe, bomani, wala mama yako! wanachosema warioba na bomani ni photocopy ya maoni ya wananchi. tatizo kuna watu wanajitoa akili eti wanasame 'haya ni maoni ya warioba'! what a confusion and insanity!
 

Le Mutuz
Je unajua katiba mpya ya Zanzibar imeondosha uhalali wa serikali mbili?

1. Zanzibar ni nchi, hii haikuwepo enzi za Nyerere na Mwanasheria wake mkuu Bomani
2. Kwamba sheria zote zitakazotungwa na bunge la Muungano hazitofanya kazi Zanzibar unless zithibitiswe n Bunge la Zanzibar. Hii ina maana Bunge la Zanzibar liko juu ya Bunge la muungana kwa mambo yote!

Ni dhahili katiba hii imeshavunjwa na CCM ilishindwa kuwadhibiti Zanzibar kufanya hivyo kwanini povo liwatoke inapowekwa sheria mama ya kusawazisha hayo?

Leo umeona serikali ya Zanzibar ikiingia katika mkataba wa gesi na mafuta kama nchi? Je katika huo mkataba ni wapi mpaka wao?

Ni dhahiri Rais wa Zanzibar na Bunge lao litasimama kidete kulinda maslahi yao Hata kama Rais wa Muungano akitoka Bara na akawa mbabe! Je Rais wa Muungano akitoka Zanzibar na akawa mbabe na kuwapunja wabara huku akiwapendelea Wazanzibar, nani atawatetea Watanganyika? Hakuna ! Maana huyo huyo mtu wa nchi nyingine ndiye Rais wa Bara!

Mazingira yamebedilishwa sana na katiba ya Zanzibar, kero za muungano kwa sasa na kuongezeka kwa uhuru wa kujieleza ukilinganisha na hapo awali!

SERIKALI TATU AU MOJA NDIO JIBU, SELIKALI MOJA WENZETU WA VISIWANI HAWAITAKI HIVYO SULUHU PEKEE NI SERIKALI TATU
Nakushauri Le Mutuz usiwashambulie watoa hoja personaly bali toa hoja mbadala
 

Kama watu wanaona serikali mbili ni kiini macho, basi serikali tatu ni mizungu. Unajua kwenye CCM kuna kitu cha ajabu, kilichoandiokwa kwenye sera na manifesto ya CCM ni tofauti na maoni ya watu. Issue hapa sio kukwepa matatizo ya muungano kwa kivuli cha serikali tatu. Unless tuigawe Tanzania kwenye mapande 8 au 9, tuwe na serikali ya Shirikisho na serikali nyingine 9. That will somehow make sense.. serikali 3?
 

mkuu, hii ndiyo pointi mujarab. huyo mburula aseme faida za serikali 2 na namna kero za muungano zinavyoweza kutatuliwa tukiwa ndani ya mfumo huu, sio kubwabwaja tu!
 
- Sasa kaka na wewe mbona unatoa mpya, CCM si ina Katiba yake na Serikali ina Katiba yake na Chadema ina katiba yake, au?

Le Mutuz

sasa kwa nini mnapinga katiba ya nchi yenye kuwa na serikali serikali 3 kwa kigezo kwamba SIO SERA YA CCM? kwani katiba ya nchi lazima ifanane na katiba ya CCM? acha ujuha wenu.
 
 

1. Unasema wacha wananchi washirikishwe lakini wewe na Bomani, Warioba mnasema mmesahaamua kwamba wananchi wanataka Serikali Tatu, unasema for this wewe una akili sana masikini wa Mungu yaani hata kuendelea kukujibu na mimi nitaonekana sina akili kama wewe mkuu pole sana!!

Le Mutuz
 
At a Julia wapi yote hayo mtoto wa mama huyo? Siku zote Jamaa huwa anaongea km kafumaniwa yaani blabla tu. Sijui utajipwnyeza kwa kigezo lipi wkt ccm inawenyewe, wazee wako waliisha wekwa pembeni na chama muda mrefu. Wewe Basi Kila jf tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…