I posted
this information for archiving in 2008. Originally I posted it to one government website that was purpoted to be collecting people's opinions.
I repost it here again:
Tuesday, January 15, 2008
Ikumbukwe tu ilishasemwa…
[FONT=verdana,geneva]Wizara [inayohusika na sheria na katiba] itoe Waraka wa Serikali wa Kuongeza kanuni zifuatazo kwenye uendeshaji wa Kesi za Jinai na za Madai:[/FONT]
[FONT=verdana,geneva]1. Kabla ya Kumtia Hatiani Mshtakiwa Yoyote, akabidhiwe nakala ya Mwenendo wa Kesi. Kabla ya Kutolewa Hukumu yoyote, Mshtakiwa apewe nakala ya Mwenendo wa Kesi.[/FONT]
[FONT=verdana,geneva]2. Hukumu inapotolewa kwa Kesi yoyote, Mshtakiwa apewe PAPO HAPO nakala ya Hukumu. Kwa mshitakiwa asiyeona, mwenendo wa Kesi, pamoja na Hukumu viwe kwa maandishi maalum ya wasioona.[/FONT]
[FONT=verdana,geneva]3. Kama Mshitakiwa atatiwa hatiani pasipo kupewa nakala ya mwenendo wa Kesi KABLA ya kutiwa hatiani, hatia hiyo isitambuliwe kisheria.[/FONT]
[FONT=verdana,geneva]4. Kama mshtakiwa yoyote atahukumiwa pasipo kukabidhiwa nakala ya Hukumu PAPO HAPO, basi Hukumu hiyo ihesabiwe kuwa ni batili, isipokuwa pale mtu anaposhitakiwa pasipo kuwepo Mahakamani, ambapo itamlazimu Mtoa Hukumu kuiweka Nakala ya Hukumu hiyo tayari.[/FONT]
[FONT=verdana,geneva]5. Muda wa Mahabusu uhesabiwe kwenye kifungo [Mahabusi zina hali mbaya zaidi kuliko hata magereza!, au, Mahabusu wana hali mbaya zaidi kuliko Wafungwa!] Mtu anayekaa Mahabusu kwa Muda unaofikia Kiwango cha Chini cha Adhabu, Aachiliwe Huru, na kesi yake ifutwe. Mtu anayekaa mahabusu Miaka Kadhaa, Halafu akahukumiwa kwenda Jela Miaka Kadhaa+Miaka Kadha wa Kadha, basi atakaa jela Miaka Kadha wa Kadha tu, kwa vile ashakaa Mahabusu miaka kadhaa.[/FONT]
[FONT=verdana,geneva]6. Kwa kosa lolote lenye adhabu ya Kifungo cha zaidi ya Miaka Mitano (5), Rufaa iwe ni \'automatic\' - Mshitakiwa hahitaji kufanya lolote ili kesi yake iangaliwe na Mahakama ya Juu zaidi… Labda kama Mshitakiwa mwenyewe atasema bayana hataki Rufaa. [Ufaransa ni moja ya nchi zifanyazo hivyo][/FONT]
[FONT=verdana,geneva]7. Kanuni ya Adhabu itamke kwamba "Kifungo cha Maisha" maana yake ni "Miaka 15 Jela". Adhabu zote zinazozidi Miaka 15 zipunguzwe na kuwa kuwa "Kifungo cha Maisha" au, vizuri zaidi, cha chini ya hapo. [Sweden hufanya hivi pia][/FONT]
[FONT=verdana,geneva]8. Pawepo na "Automatic Parole" kwa vifungo. Labda tuseme 60% ya kifungo itakuwa gerezani, na 40% itakuwa ya "parole", labda isipokuwa mfungwa atakuwa anatumikia pia adhabu nyingine muda huo wa 'parole'.[/FONT]
[FONT=verdana,geneva]
"Ukitaka kujua watu ni binadamu kiasi gani, tembelea magereza yao!" - Nukuu[/FONT]