Jaji M.C. Othman Jaji Mkuu mpya wa Tanzania

CV imetulia, I hope na utendaji pia umetulia
 
sijawahi kusikia Jaji ambaye ni Kilaza..........heshima mbele kwa Majaji
 

Mkuu nadhani wote tunazielewa terminology za kisheria ila tunabishana tu katika uteuzi wa ndugu wawili sehemu mbili. Jibu la swali lako liko katika nini kazi za DG wa Usalama wa Taifa na kazi za Chief Justice wa Tanzania. Ikiwa kuna uwezekano wakawasiliana na kufanya kazi pamoja naweza kukubaliana na wewe. Lakini hawa wako far apart mkuu mmoja yuko katika mahakama mwengine yupo katika idara nyeti ya serikali sasa niambie conflict of interest inatoka wapi? Hebu nifafanulie pengine mie silioni!
 
Ikiwa kuna uwezekano wakawasiliana na kufanya kazi pamoja naweza kukubaliana na wewe.

Ndio mkuu issue iko kwenye kuwasiliana na kufanya kazi pamoja (now hawa Jamaa being ndugu) huoni kwamba kaka mtu anaweza akainfluence decision za mwingine au vice versa..?????
 
Hujui function za TISS ndio maana unaona na kudhani hizo idara zinaingiliana.

Kama unazijua functions za TISS na unaona zinaingiliana na za idara ya CJ, basi zitaje.

Wapi ilikuwa imeandikwa kwamba TISS ituchagulie rais watanzania? Did not they do it?
 
Wapi ilikuwa imeandikwa kwamba TISS ituchagulie rais watanzania? Did not they do it?

Lete ushahidi usio na shaka kwamba TISS wamechagua rais. Leo niambie kuwa wananchi waliopiga kura wametoka au wapo TISS.
 
Lakini wakristu kuna mawaziri 33 vs 17 vipi mbona JK hana imani na waislamu kwenye mambo uwaziri?

I hope umejumlisha na idadi yote ya baraza la wawakilishi. Hawa nao wanatumia resources za Tanzania maana Tanzania ni moja licha ya vikorombwezo vya maneno ya kisiasa
 
Ndio mkuu issue iko kwenye kuwasiliana na kufanya kazi pamoja (now hawa Jamaa being ndugu) huoni kwamba kaka mtu anaweza akainfluence decision za mwingine au vice versa..?????

Hizo ni hearsay mkuu maana kuna mipaka ya kazi na wanaongozwa kwa mujibu wa utaratibu wa kazi sasa sijui labda avunje sheria naweza kukubaliana na wewe but this purely speculation mkuu tuwaachie wafanye kazi tusiwahukumu pasina hatia.
 
Hizo ni hearsay mkuu maana kuna mipaka ya kazi na wanaongozwa kwa mujibu wa utaratibu wa kazi sasa sijui labda avunje sheria naweza kukubaliana na wewe but this purely speculation mkuu tuwaachie wafanye kazi tusiwahukumu pasina hatia.

People break the law....... Huo ni ubinadamu...... sasa hili kuepuka hilo Tanzania inabidi tuanze kuangalia kwenye ngazi zote watu ambao wapo madarakani hawana uhusiano wa karibu ambao unaweza lead to corruption... (its like a scenario polisi anakushika alafu baba yake ndio anayekuhumu... am sure unajua where am coming from with this)
 
Hongera zake anaonekana anafaa kwa post hiyo!
 


tukisema Mkwere mdini mnakataa,udini na kikwete ni mtu na binamu,lakini utamgarimu sana.
 
Tunabishana na kilaza mmoja ambaye hajui hata maana ya confict of interest! Tunapoteza muda wetu bure. Haya ni matokeo ya system mbaya ya elimu ya Tz... watu wanasomea kushinda mtihani....
 
tukisema Mkwere mdini mnakataa,udini na kikwete ni mtu na binamu,lakini utamgarimu sana.

Hapa sasa ndio kuna conflict of interest Je unaweza kutwambia kwa ufasaha zaidi mkuu vp JK na CJ Chande ndugu?
 
Nina wasiwasi kama CCM wamemwonea choyo huyu jamaa na sasa wanatafuta njia ya kumtelekeza ! Ila sasa ndio yupo kwenye mtihani mkubwa maana Tz kumejaa urojo na mbatata.
 
Hakuna shaka yeyote kuwa anafaa... wala mambo ya udini mimi sijayaona, na wala sidhani kuwa busara rais anapoteua mtu aangaliye balance ya mikoa au undugu. Issue ni kuwa hizi positions za hawa jamaa ni sensitive sana na zina mwingiliano wa kimaslahi. Na mifano uliyotoa ni irrelevant ya hawa jamaa!
 
..mbona wako kwenye mihimili tofauti ya utawala.

..na pia tayari CJ Chande alikuwa kwenye court of appeals. sasa hizi conflict of interests zitakuwepo kwasababu tu amepanda cheo?

..so far sina matatizo na uteuzi huu. unless mtu aje hapa atueleze kuhusu legal philosophy ya CJ Chande, au atuonesha hukumu alizopata kutoa kama zina matatizo.

..wenzetu wanapojadili teuzi za majaji huchunguza HUKUMU walizotoa, OPINIONS zilizoko ktk maandishi ya mhusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…