Jaji M.C. Othman Jaji Mkuu mpya wa Tanzania

Mpaka sasa mimi sijaona mgongano wa kimaslahi ulio moja kwa moja. Endapo ikatokea hapo mbeleni kukawa na shauri linalowahusisha wote wawili kwa ukaribu basi jaji Chande atatakuwa kuji-recuse kutoka kwenye hilo shauri ili kuepuka huo mgongano wa kimaslahi.

Kwa hiyo mimi hadi hivi sasa ningependa kujua zaidi judicial philosophy yake na opinion alizokwisha andika. Kuna anayejua hayo?
 
Sidhani kuna kitu cha kubishania hapa! ..wenzetu wanapojadili teuzi za majaji huchunguza HUKUMU walizotoa, OPINIONS zilizoko ktk maandishi ya mhusika. Hiyo dini sijui inaingiaje hapa, labda kama aliyemteua ndo awe na ajenda yake siri ambayo hata hivyo hatuwezi kuithibitisha hapa. Cha muhimu hapa ni huyu jamaa kuwa independent kwenye maamuzi ya kama CJ bila kuogopa pressure za the big men in power kama alivyofanya mtangulizi wake kwenye kesi ya katiba!
 
hongera zake, na cha msingi afanye kazi nzuri bila upendeleo
 

What happened to the special considerations to womens, which we saw on the issue of the speaker of the parliament. No more womens who deserves high post anymore?
 

nakuunga mkono asilimia zote
 
Nakumbuka wakati niko sekondari nilikuwa na special interest with African American history na literature. Nadhani hii ilichangiwa zaidi na kwenda kwangu pale USIS (maelezo sasa hivi) baadae ilipohamia kule PUGEOT HOUSE. Katika kusoma kwangu among my favorites alikewa Malcolm X ambaye quote yake ni ninayoipenda ni aliposema kuwa TOMORROW BELONGS TO THOSE WHO PREPARE FOR IT TODAY lakini pia bila kumsahau WEB DU BOIS lakini nilisoma kitabu kilichoandikwa na FREDRICK DOUGLASS ambaye alisema..."TO UNDERSTAND, A MAN MUST STAND UNDER." Kwa maneno mengine ni kuwa only by considering all the hardships a man has overcome in life, hivi ndivyo Douglass alivyokuwa anaamini, so can the rest of us judge him fairly. ivyo jaji Othman hana tofauuti katika hili.

Mimi ninamfahamu Jaji Othman and i fail to understand kwa nini uteuzi wake uwe issue nzito tena katika ukumbi huu wa the so called EXPERTS and GREAT THINKERS


Anyone who knows Judge Othman should by now realize that reputation was everything to him the work of art he had sculpted, the summit he had climbed, the treasure he had stored up from years of public service. Jaji Othman ninavyomjua mimi has often spoke of his life and reputation as one and the same. It really concerns me kuwa hakuna aliyekuja na any constructive criticism of his intellectual work as the learned au mtu aliyebobea kwenye fani yake.



Huyu Jaji wetu mpya, like most who rise to power, he had toiled for years in anonymity serving others of higher station. I just wanna tell you one thing, endeleeni kumtukana na kumkejeli as much as you want lakini mkae mkijua kuwa huyu jaji mkuumpya is not for turning. Ndio ni Muislam na kama kuna mtu hapendi then he hilo ni shairi lake. Lakini kwenye Tanzania iliyojaa maskini ya leo hii na pia Tanzania ambayo its common waislam kuambwa kuwa HAWAJASOMA lets just say kuwa hizi baseless accusations if anything zitamsaidia in an important way, by underscoring the fact that he carried along with him the aspirations of the 'under-educated' Muslims in Tanzania.


Hapa once again JK na team yake imeweza kuwathinitishia kuwa you dont have to be born into privilege ndio utafanikiwa. Hii pia ni kkuwaonyesha wanaolalamika kuwa its possible for a MSWAHILI na MUSILAM kuwa Jaji Mkuu Tanzania ni possible tena Jaji ambaye miaka ypte yake ya utumishi amekuwa akitoa huduma bila kujali MKRISTO au dini nyingine yoyote ile. As a nation we should be proud kuwa we are moving on from petty politics na kuangalia mbele. If anything appointment ya Jaji Othman ni culmination of his life and his struggles.
 
Mkwere mdini na atuendleza forever

Kipimo cha utendaji wa mtu kiwe ndo kigezo cha uteuzi, wtz tukianza kuangalia udini au upendeleo hatutafika.
Je upendeleo umeanza leo.Mwl enzi zake alizungukwa na karibu ndugu zake k.m tulikuwa na katibu mkuu Timothy Apiyo toka Musoma, Butiku,Msuguri,Twalipo,n.k mbona hilo hatukuliona?

Tukikumbatia udini tutajikuta tunaogopa kuwapa watu madaraka wanaositahili. kipimo chetu kiwe utendaji wa mtu.
Tatizo analolipata Kikwete ni pale tu anapo shindwa kuongoza nchi kama rais, hilo limewapa wasiwasi wananchi wengi kwani kwa mtizamo wangu nadhani baadhi ya wananchi walio wengi wameanza kukosa imani na yeye.

Mimi naimani kuwa wapo wakristu wazuri na waislam wazuri ambao wanastahili kuaminiwa.Bwana Othman tumwangalie kiutendaji
hicho ndo kiwe kigezo chetu.
Swala la kuwa mdogo wa Rashid Othman, naamini kuwa hata mimi ningekuwa Rashid ningempa kipaumbele ndugu yangu kwanza kabla ya mtu yeyote mwingine ilimradi anauwezo.

Jambo tu ambalo tunaweza kumtaka Rais ni kuhakikisha kuwa hatuchagulii watu kwa misingi ya urafiki,hata kama hawana uwezo
jambo ambalo watz wameliona sana kwa bwana Kikwete kama tutakuwa wakweli.
Jambo jingine ambalo tunahitaji tulione kwake ni kulinda katiba hata kama bado ina mapungufu,
 
What is there more kindly than the feeling between host and guest? Wacha tumuone na yeye, tumpe nafasi.
 



Kwakwel naomba nikubaliane na wewe na kupingana pia na wewe, nakubaliana kwamba haina maana kuanza kuona uteuzi ni mbovu sbb huyu mtu ni muslim,na kwa mtu anaye furahi mkiristo au muislam kupata uteuzi ana akili mbovu mana kama si ndugu yako huyo mtu hawez kukusaidia lolote. Mana akiwa muislam na wewe ni muislam haina maana ndo ukikutana nae njian atakupa hela,kwaiyo suala hapa tuangalie sifa zake.

Ila naomba kukupinga kua suala la boss wa usalama wa taifa kua kaka yake halina vigezo napingana na wewe maana kila mtu anajua rais hawez fanya uteuzi wowote bila kupata ushauri wa usalama wa taifa,sasa kma ktk mchakato huo wa uteuzi huyu boss wa usalama mdogo wake yupo kati wanao wania unazan huyo boss atasema nani ateuliwe?kwel jamaa CV yake imeshiba ila me naona kaka yake amechangia kumpa iyo post mdg wake
 
Kahinda,
Twalipo alikuwa Mtanga. Ni hilo tu. Na Apiyo Mjaluo. Lakini nadhani kwa sisi tunaotoka Mara tunajumlishwaga kama kabila moja ingawa tuna makabila 23. Ni hayo tu.
 

We huna karatasi ndo mana huwez kurudi,ila sijaona sbb ya kututusi namna iyo aise,ingawa kwel tuna judge mambo kwa kuangalia vitu visivyo kua na maana ila huwez kututusi ivyo,we endelea kubeba box huko si tunajenga nchi huku
 

wanaJF,
Ninyi kweli ni great thinkers,
nimepitia thread hii na kupitia hii hapa chini. Nimese mumeniacha hoi. Double-standard for anyone to see!!keep it up!

Yesterday 07:43 PM #1
The Informer

Senior Member
Join DateMon Jun 2010Posts61Thanks22Thanked 165 Times in 31 PostsRep Power21


Did you find this post helpful?
|
Dk. Mwele Malecela ateuliwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa NIMR


Rais Jakaya Kikwete amemteuwa Dk. Mwele Malecela kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa National Institute for Medical Research (NIMR) iliyo chini ya Wizara ya Afya. Dk. Mwele alikuwa ni mtafiti mkuu wa NIMR na amekuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu kwa muda. Ni kijana na mwanamke wa kwanza kuiongoza NIMR. Huyu mama ni kichwa sana na anaweza sana kazi. JK huwa anafanya mapupu mengi sana kwenye uteuzi wake ila hapa kafanya kweli.

Source: channel ten news bulletin leo 7pm​
 
yaani mlitaka awe mkatoliki?
 
nyerere alisema tutizame utendaji wake tusiangalie udini wake.
 
Nonda,

Hawako hapa kuficha double standards wako kazini kuchafua kila abdul...ndio JF
 
shida kubwa hapa we rutashubanuyma ni udini wako. pale viongozi wako waliposema huyu ni chaguo la mungu uliwajibu lolote.? uteuzi huo ni mzuri chuki zako si za upendo ni chuki mbaya kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…