Jaji Makaramba atajwa kuandaa kesi ya Zitto.

Status
Not open for further replies.
moderator potezea hii post kumtuhumu jaji kwa ushahidi hewa akilivalia njuga kwa kushushiwa hadhi jamii forum inaweza pata matatizo


Acha uwoga wewe,Kama mnategemea Buku7 ili muishi hapa mjini nakushauri utafute ajira ingine au njoo kwangu nikupe ajira maana msichana wangu wa kazi amefaulu na anaendelea na masomo yake ya sekondari.

Watu wazima mnashinda jf kwa kutegemea ujira wa buku7?
 
Wakili kufanya consultation kwa Jaji kabla ya kupeleka shauri mahakamani sio jambo jipya.Inawezekana kwa kutegemea ukaribu wa Jaji husika na wakili japo kimaadili ya sheria hairuhusiwi. Kwa mtazamo wa kesi hii ilivyona mvutano wa pande mbili CDM na CCM hili linawezekana kabisa.Ushabiki uwekwe pembeni alieleta mada hii atoe uthibitisho wa tuhuma alizotoa kwa kuwa tuhuma hizi ni nzito kwa Jaji alietajwa.
 
Pole sana. Ila mliposhinda kesi zenu mlipongeza na kusifi uwezo wa mahakama. Au umesahau ule usemi kuwa Sheria ni Msumeno? Au ulikuwa unaimba tu shuleni?

Pale majaji waligwaya nguvu ya umma na kujifanya they are not biased,ila ukweli utabaki palepale Tz hakuna fair,huoni jela wamejaa vibaka tu ila hakuna cha fisadi wala jambazi au wauza unga huko.
 

Taarifa hiyo ili leak mapema hata kabla ya judgement. Wengi baada ya kujua hilo tulijua hukumu itakuwaje. Kwa mazingira ya sasa taarifa kama hizi zitavamiwa na kupingwa sana humu jamvini. Lakini tusikate tamaa tuendelee kupeana taarifa. Chadema haipambani na Zitto bali na waliomtuma hiyo kazi maalum.
 
jambo hili linaitaji uchunguzi na ikibainika jaji aliyeusika achukuliwe hatua kwani ni ukiukwaji wa maadili ya mahakama na sheria jambo hili linaweza ikasabisha wananchi wasiheshimu maamuzi ya mahakama jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi
 

Habari hii ya kesi ilipoanza tu, mimi nilisema hapa, kwa nini CHADEMA hawalimalizi suala hili chamani?

Kwa nini hawaitishi hilo Baraza Kuu liamue?

Kwa nini wanakubali kwenda kwenye mahakama, mahakama ya dola la CCM ambalo kila siku wanalipigia kelele kwamba haliwapi haki?

Sijapata jibu mpaka leo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…