Jaji Manento: Rais apunguziwe mamlaka uteuzi wa Majaji

Jaji Manento: Rais apunguziwe mamlaka uteuzi wa Majaji

Angetakiwa awe anayashauri hayo wakati akiwa jaji.

Anyway wazo zuri.

Mwisho angetakiwa kusema kuwa tume ya haki jinai ipo kupumbaza watanzania na kuchelewesha katiba mpya

serekali ya ajabu sana hiii
Sasa unataka atoe mawazo yake kama vile ni yako, we toa ya kwako
 
..Jaji Manento akiwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu aliingilia kati suala la kifo cha mwandishi Daudi Mwangosi na kutoa ripoti iliyobainisha ukweli kuhusu tukio lile. Serikali ilikuwa inajaribu kusema uongo.

..labda kuna wanaomfahamu zaidi, lakini ktk tukio lile na ripoti aliyotoa nadhani ni Jaji mwenye msimamo na aliyenyooka ktk haki.
Tunaomba hiyo ripoti tuipitie na sisi
 
Jaji Kiongozi mstaafu, Amir Manento amependekeza Katiba iweke udhibiti kwa Rais asiwe na mamlaka ya kuteua majaji nje ya mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Mahakama. Manento alitoa mapendekezo hayo jana kwa kwa Tume ya Haki Jinai, iliyoundwa па Rais Samia Suluhu Hassan, kuangalia jinsi ya kuboresha mfumo na taasisi zinazosimamia haki jinai, inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande.

Akizungumza па waandishi wa habari baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Tume hiyo, Jaji Manento alisema kuwa ingawa Tume ya Utumishi wa Mahakama hupendekeza majina ya majaji, lakini Katiba inampa Rais mamlaka ya kuteua majaji hata nje ya orodha inayopendekezwa.

Ibara ya 109 ya Katiba inasema kuwa majaji watateuliwa na Rais kwa kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

"Rais hatakiwi kushughulikia mambo ya kitaaluma, yeye ni mwanasiasa, anaweza akateua majaji wa kisiasa. Haki haitatendeka wala haitaonekana inatendeka ingawa ni jaji. Waachiwe wataalamu wa sheria, vigezo ni vingi kwa sababu nilikuwa huko."

"Tunaangalia hukumu zako, mwonekano wako mbele ya watu, lugha unayotumia, je, unawafokea, unawatisha na heshima yako.

"Sasa leo unamwachia Rais, na washauri wake ni wanasiasa, haki haitatendeka," alisema.

Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk Rugemeleza Nshala alisema "Tume inashauri tu, anayeteua ni Rais. Kwa hiyo. ushauri si lazima ufuatwe.

Kwa upande mwingine, Jaji Maneno alipendekeza kuwepo na chombo kinachosimamia utekelezaji wa haki za jinai.

Pia chombo hicho kiwe chini ya Mahakama akisema kwamba kwa mfumo wa Mahakama kitakuwa huru, kwani polisi wanakiuka haki tangu kukamata watu.​
kiukweli, wengi walioteuliwa kwa mamlaka ya moja kwa moja ya rais, ni vilaza sana. wengine anawatoa huko kwenye waalimu wa sheria ambao hawana uzoefu wowote kupractice sheria, wakija mahakamani wanatusumbua kweli kwasababu hawana uelewa wa practice, wanajua theory tu. kuna baadhi ya majaji tukiwataja hapa hadi wanatia huruma wakati nje ya ujaji kwenye theory huko walikuwa vizuri sana. ila mahakamani hadi wanasaidiwa na makarani.
 
Back
Top Bottom