TANZIA Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Bongole afariki Dunia

TANZIA Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Bongole afariki Dunia

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma anasikitika kutangaza kifo cha Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora Mhe. Salvatory Bongole aliyefariki Dunia jana saa 5 usiku wa kuamkia leo baada ya Kuugua ghafla.

Jaji Bongole alipofikishwa hospitali ya Mkoa ya Kitete kwa matibabu, Daktari alithibitisha kuwa amefariki.

Taarifa Kuhusu Mipango ya Mazishi zitajulikana hapo baadaye.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE

Bongole.jpg

Taarifa za Mipango ya Mazishi zitajulikana baadaye.

Zaidi soma:

Rais Jakaya Kikwete amewaapisha Majaji akiwemo Joaquine De-Mello

Hongera Mahakama kufunguliwa MwanaHalisi
 
Inategemea alikuwa akita hukumu zake kwa mlengo gani, kama alikuwa kama akina Feleshi basi kwa kweli abanikwe kwanza kabla ya kuhukumiwa, ila kama alisimama kwenya haki kama akina Rumanyika basi apewe tuzo ya fadhila na mwisho mwema bila hila
 
Du!
 
Corona imekatili maisha ya mja wa mnyeezi mngu.
 
Corona imekatili maisha ya mja wa mnyeezi mngu.
WaTZ wanaamini hakuna korona kabisa,ukipanda kwenye daladala yaani peke yako tu ndio umevaa mask tena abiria basi zima wanakushangaa,kwasasa hakuna cha level seat wala nini daladala zinajaza pomoni.

Ila jana Aman Karume alivaa mask na alikataa kupeana mikono na watu!!
 
Corona inatulia denge, ikikamilisha mzunguko wake itaanza kufanya vitu vyake kikatili zaidi.
Lamentation.
 
Msidanganyike, Korona bado ipo tena sana! Na sasa hivi dalili zimebadirika, ni kufa ghafla!
Chukua taadhari, jikinge na wale uwapendao; hao wajinga wanaoamini imeisha watajua wenyewe!
 
Anaenda kuhukumiwa na yeye katika haki kutokana na matendo yake.
 
Kama hakujenga na mjane alikuwa maza hausi soon watahamishwa kutoka nyumba za serikali waje tubanane nao uswaz
 
Back
Top Bottom