Jaji Mihayo: Wasimamizi wa Uchaguzi wasipokee maagizo ya kuvuruga Uchaguzi kutoka kwa Viongozi wa Serikali

Jaji Mihayo: Wasimamizi wa Uchaguzi wasipokee maagizo ya kuvuruga Uchaguzi kutoka kwa Viongozi wa Serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kamishna wa Tume ya uchaguzi NEC Mhe. Jaji Mihayo amewataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuwashirikisha Viongozi wa Vyama vya Siasa pale inapostahili kufanya hivyo ili uchaguzi uweze kuwa Huru na Haki.

Kadhalika Jaji Mihayo amewaasa wasimamizi hao kutopokea maagizo kutoka kwa Viongozi wa Serikali yatakayopelekea kuvuruga Uchaguzi.

Jaji Mihayo alikuwa mkoani Geita kutoa semina kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa October, 2020.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Hiyo ndiyo Tanzania ya viwanda tuliyo aminishwa ni sera ya mzee Baba kumbe ana tekeleza sera za Mzee Ben. Wapumbavu na malofa..
 
Kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii hawezi kusimamia hii kauli.
 
Nina hakika madhara ya kuvuruga uchaguzi anayajua.
Ni juu yake kusimamia ukweli huo ili kumaliza uchaguzi huo kwa haki, amani na salama.
 
Huyo jaji ni tapeli, jiwe haogopi majaji wanaoongozwa na tumbo. Na huyo jaji hana uwezo wa kumuhakikishia ajira msimamizi yoyote wa uchaguzi, iwapo atafukuzwa kazi na jiwe. Hiyo tume sio huru asitake kujifanya ana power ya kuzuia chochote wakati yeye mwenyewe hiyo power hana.
 
Anawaadaa wananchi na dunia
Danganya toto hiyo
 
Danganya toto, na zaidi, tuitumie kauli hii kujiandaa kisaikolojia

Mbona hamueleweki jamani, yaani hata juzi Mh. Lissu karudi watu wameandamana free yaani bila hata usumbufu bado Lema na wana CDM wanadai hawaamini, Lema anasema kuna kitu kinaandaliwa wawe makini, yaani hata maandamano mmefanya, hamjaguswa bado hata past event mna wasiwasi.. Jaji kasema kabisa uchaguzi utakuwa huru na haki, bado mnatia shaka.. Labda tuwape Tume yote ya Uchaguzi mchukue na kila kitu, alafu bado hamtaridhika.. Sasa mtapewa nn? 😅
 
Back
Top Bottom