Namfahamu Jaji Augustino Ramadhani tangu akiwa kijana. Anatoka kwenye a very humble family of late Mwalimu M. Ramadhani aliyekuwa miongoni mwa waalimu waafrika wa Tabora School miaka ya 1960s. Bahati mbaya, miaka hiyo hiyo ya 1960s sikumbuki mwaka, alipokuwa Uingereza kujiendeleza kimasomo akafariki dunia kwa ajali ya treni na kuwaacha akina Augustino wakingali vijana wadogo. Wamelelewa na mama yao very humbly na ni wacha Mungu sana. Kwa hiyo, sishangai kabisa kwa Augustino kufanya hiyo noble gesture ya kutumia fedha alizotengewa yeye na kuzitoa zitumike kwa ajili ya kumbukumbu ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kwanza wa nchi yetu baada ya nchi kupata Uhuru.
Si hilo tu ambalo judge Ramadhani ameweza ku-sacrifice kwa ajili ya wengine, yapo mengine mengi na amefanya hivyo bila motive yoyote binafsi ama kisiasa. Moja ninaloweza kulieleza hapa ni kwamba anayo nyumba Mbagala ambayo aliamua kumwachia Askofu mmoja wa Kanisa la Anglican aishi bure kabisa kwa kuwa Mzee yule alipostaafu alikuwa hana nyumba Dar es Salaam na familia yake ilibidi iishi Dar kwa sababu mbalimbali. Askofu yule aliishi ndani ya nyumba ile kwa miaka zaidi ya 10 bila kutakiwa kumlipa Jaji Augustino chochote hadi Mzee huyo Askofu alipofariki dunia mwaka jana.
Kasheshe, Pape et al,
Nyie mwaweza kuyafanya hayo?