Jaji mkuu akamilisha jengo la mahakama kwa fedha alizotengewa yeye!

Jaji mkuu akamilisha jengo la mahakama kwa fedha alizotengewa yeye!

Lazima afanye hivyo maana ndio msimamizi wa sheria katika Taifa letu, Sasa kama yeye naye akiwa fisadi itakuaje
 
Karabati/ujenzi wa nyumba za serikali zilikuwa zinafanywa na Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala (D.A.P) wa wizara mama ya idara husika. Hakupewa mtu hela mkononi akajenge paa mpya ya nyumba anayoishi. Na si vibaya, maana asiye mwongofu angeweza ziba nyufa za nyumba za serikali na kubakiza cha juu kuezekea nyumba ya mke mdogo; ulikuwa utaratibu mzuri.

Jaji Ramadhani alipewaje hela mkononi?

Jaji Ramadhani alipataje uhuru wa kujiamulia nyumba ipi aijenge kwa hela yetu?

Jaji Ramadhani atakapostaafu na kutoka kwenye nyumba hiyo iliyobaki mbovu atatoa hela za kumkarabatia nyumba mrithi wake? Maana sisi tulishatoa kodi yetu kukarabati nyumba ya Jaji Mkuu, sio ya Ramadhani au ya “hero” wa Ramadhani; ya Jaji Mkuu. Ramadhani atatulipa hela yetu?
 
Nyie hamkosi cha kusema, wewe unayetoa maoni yako umesaidia nini.U just have big stinky mouth.
 
Bibi Ntilie,

Hata mimi nafahamu angalau kwa kidogo kwamba kama kuna watumishi watatu WASAFI nchini basi jaji AR. atakuwepo ... ninalokataa ni hili hapa.

1. Hilo jengo liliokuwa linajendwa ni la Jaji Mkuu wa Tanzania sio la Jaji Augustino Ramadhani.

Of course; lakini hilo siyo halalisho kuwa lazima kiasi hicho kitumike. Kwa vile ni la Jaji Mkuu haina maana Jaji Mkuu Augustino Ramdhani hatofurahia kile kitakachokamilika. Jaji Mkuu siyo mtu wa kufikirika. Kama vile Gavana anapojijengea jumba kwa mabilioni na vikolombwezo kibao ambayo yeye ni mkazi wake haitoshi kusema kuwa "siyo ya kwake bali ni ya Gavana yeyote atakayekuja baadaye".. tunajuaje kuwa huyo atakayekuja na yeye hatofanya mabadilko yatakayomnufaisha yeye akidai kuwa "hata wa baadaye naye atanufaika"?

2. Waliokadiria (budget) kwamba majengo hayo mawili la Jaji na la Mahakama ni hao hao.

Waliotenga fedha.. walitenga kiasi kikubwa kwa nyumba ya Jaji Mkuu kuliko ya jengo la ofisi na hivyo inaonesha ni jinsi gani wamefulia kifikra.

3. Jaji mkuu anastaafu karibuni kwa tetesi za hapa jamvini... mwaka huu kama sikosei... hivyo hakuna masilahi kwake kujenga helo hekalu.

Ni tetesi tu.. anaweza kuendelea au kuombwa kuendelea; na sidhani kama amefikia umri wa kustaafu kwa lazima anyway.

----> kilichofanyika ni changes of priority lakini majengo yote mawili yatajengwa... nothing special to me.

Hapana.. hakukuwa na priorirty ya jengo la ofisi vinginevyo Jaji Mkuu asinge divert fedha ya nyumba yake kupeleka kwa jengo la ofisi. Kama vyote vingekuwa kwenye kipaumbele au kama ofisi ingekuwa na kipaumbele basi Jaji Mkuu asingefanya alilofanya.
 
Karabati/ujenzi wa nyumba za serikali zilikuwa zinafanywa na Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala (D.A.P) wa wizara mama ya idara husika. Hakupewa mtu hela mkononi akajenge paa mpya ya nyumba anayoishi. Na si vibaya, maana asiye mwongofu angeweza ziba nyufa za nyumba za serikali na kubakiza cha juu kuezekea nyumba ya mke mdogo; ulikuwa utaratibu mzuri.

Jaji Ramadhani alipewaje hela mkononi?

Jaji Ramadhani alipataje uhuru wa kujiamulia nyumba ipi aijenge kwa hela yetu?

Jaji Ramadhani atakapostaafu na kutoka kwenye nyumba hiyo iliyobaki mbovu atatoa hela za kumkarabatia nyumba mrithi wake? Maana sisi tulishatoa kodi yetu kukarabati nyumba ya Jaji Mkuu, sio ya Ramadhani au ya “hero” wa Ramadhani; ya Jaji Mkuu. Ramadhani atatulipa hela yetu?

Nani amekuambia anaishi kwenye nyumba mbovu; Miaka nenda miaka rudi kwanini hatuna Jumba zuri linalosimamiwa vizuri kwa ajili ya Jaji Mkuu. Hawa watu wanaoishi kwenye hizo nyumba wanazitumiaje kiasi kwamba miaka michache tu zinahitaji matengenezo makubwa? Kuna viwanda humo?

Jaji Mkuu ni taasisi huru na una uwezo wa kuamua fedha gani ziende wapi.. hayuko chini ya Waziri fulani hivi! Ni kama Spika au Rais katika mihimili yao ..
 
Jaji Mkuu ni taasisi huru na una uwezo wa kuamua fedha gani ziende wapi.. Ni kama Spika au Rais katika mihimili yao ..

La hasha!

Jaji Mkuu na mahakama zake hana fungu la kujiamuliai azitumie atakavyo. Rejea hotuba yake Siku ya Sheria Duniani mwezi ulopita. Hela ya idara yake anaomba na kuamuliwa matumizi na mabwana fedha Serikali Kuu.

Kwa viwango vya wongofu vilivyo chini sana nchini kwetu, hakuna anaeona kwamba kuelekeza hela kwingine ni tatizo hata kama hutazibadhiri. Kutofuata utaratibu ni penyo la kubadhiri. Leo una Ramadhani, mwongofu, kajenga jengo la “hero” wa Ramadhani, kesho una Athumani, dakika mbili mbele, atatujengea kathiri la mke mdogo wa Athumani. Ndo maana hela hapewi mtu mkononi kiholeholela.

Ramadhani alipewaje hela mkononi akakarabati nyumba aishio badala ya utaratibu wa mtumishi huru anayehusika na uangalizi wa makazi (pamoja na mengine yahusuyo watumishi na utumishi) kusimamia ukatabati huo?

Na baada ya kupewa, Ramadhani alijibebeshaje mamlaka ya kuelekeza fungu la pesa kwingine?

Nani amekuambia anaishi kwenye nyumba mbovu; ..

Sasa kwa nini alipokea fedha za kukarabati nyumba ya Jaji Mkuu kama haikuwa mbovu?
 
Hakika wanadamu tunawaza sana tofauti, Sasa hoja ni ipi? Kasheshe, Kinnega, MMwanakijiji.....
Majibu tafadhali.
 
Yani waziri mkuu anampongeza jaji! Aoni aibu? Ilikuwaje wanapitisha matumizi ya anasa namna hiyo na mahakama nchini zina shida?
 
Hawa ndiyo viongozi tunawataka katika nchi hii na siyo kufikiri maslahi yako binafsi, kukaa kwenye hekalu wakati ndugu yako hata hela ya kula hana
 
Nyie hamkosi cha kusema, wewe unayetoa maoni yako umesaidia nini.U just have big stinky mouth.

Kinakuuma nini, unataka asipongezwe? nani apongezwe sasa, na kwa lipi!?
Wewe uliandika hapa ukiwa umebanwa sana na haja kubwa, siyo bure!
 
Wengi kumbe hamumjui huyu Jaji Mkuu. Huyu ni mwanasiasa. Hapa anacheza politics kwa sababu ana malengo yake ya kisiasa baada ya kustaafu mwisho wa mwaka. Sintashangaa mweiz Aprili akitoa hukumu ya kuruhusu wagombea binafsi. He is from Zanzibar. One time in the past aliwahi kugombea Urais kama sikosei.

Kama siasa zenyewe anazocheza ni hizi basi nitakuwa CAMPAIGN MANAGER wake.....
 
Zakayo,
Sorry to say this but you must be one stupid fella and wont apologise for saying this!!
I really feel offended for the fact that you have gone so off topic. For your information Jaji Ramadhani hajawahi hata kufikiria urais. Qualification zake na ethics tu zisingeruhusu. Amekuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, Brigedia Generali wa jeshi, Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na Jaji Mkuu wa Nchi. Mtu wa namna hii kweli atahitaji kuwa Mwanasiasa?

For your information JK alimtaka aendelee na Ujaji Mkuu lakini akakataa kuongeza mkataba. Siyo tu anapenda lakini alihisi pia ni lazima awape nafasi watu wengine.

Kwa maoni yangu Jaji Mkuu amesoma alama za nyakati na ameona hakuna wakati muafaka kwa Tanzania kuwa na Jaji Mkuu mwanamke na ndio maana anaachia ngazi ili nafasi iende kwa Mama Munuo.

Such a man is so honest kuwa mwanasiasa!!

Wengi kumbe hamumjui huyu Jaji Mkuu. Huyu ni mwanasiasa. Hapa anacheza politics kwa sababu ana malengo yake ya kisiasa baada ya kustaafu mwisho wa mwaka. Sintashangaa mweiz Aprili akitoa hukumu ya kuruhusu wagombea binafsi. He is from Zanzibar. One time in the past aliwahi kugombea Urais kama sikosei.
 
For your information Jaji Mkuu hakuwahi kuhamia nyumba aliyopangiwa simply because ilihitaji matengenezo makubwa na yeye hakuona umuhimu wa kuishi kama mfalme wakati kuna shida za vyumba vya majaji kukaa ili kundaa na kutoa hukumu.

For your further information, just know kama distance ni fupi mara nyingi jaji Mkuu hupenda kutembea kwa mguu kuliko kutumia mafuta ya serikali kama viongozi wengine.

Pia Msafara wake huwa hauongozwi na vingora kama wa watu wengine na huwa anatumia bodyguard mmoja tu kutoka usalama wa taifa ingawa he is the fifth in line katika utawala wa nchi.

You need to be noble to do what he does.
You need to have roho ya chuma kufanya maamuzi kama yale.

Back
Top Bottom