Jaji Mkuu atangazia mashahidi kiama

Jaji Mkuu atangazia mashahidi kiama

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
headline_bullet.jpg
Ni kwenye kesi za uchaguzi



Ramadhani%281%29.jpg

Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani



Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amewataka majaji na mahakimu nchini kuwahukumu kwa mujibu wa sheria watu wanaokiri mbele ya mahakama kwamba walipokea rushwa kutoka kwa wagombea katika uchaguzi.
Jaji Ramadhani alitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua warsha kuhusu sheria ya uchaguzi kwa mahakimu wakazi wafawidhi nchini, inayofanyika jijini hapa.

Alisema haiingii akilini kwa jaji au hakimu anayesikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi, kumuacha huru shahidi anayekiri kupokea rushwa kutoka kwa mgombea.
“Sheria inasema wazi kuwa mtoa rushwa na mpokea rushwa ni sehemu ya kosa, kwa hiyo wote wanastahili adhabu, iweje wewe umuache mtu aliyekiri kupokea rushwa akaenda zake,” alihoji.

Jaji Ramadhani alisema sheria ya uchaguzi inawaruhusu majaji na mahakimu kutoa adhabu mbalimbali, ikiwemo ya kuwafungia watuhumiwa wanaotiwa hatiani kutogombea.
Alisema kwa vile watoa rushwa wanazuiwa kugombea, itafaa zaidi ikiwa mashahidi wanaopatikana na hatia ya kupokea rushwa katika kesi za uchaguzi, wakazuiwa kupiga kura kwa muda maalum.

“Tusipoyafumbia macho makosa haya, watu wengi hawatakubali kupokea rushwa au kutumiwa na wagombea kuja mahakamani kukiri kupokea hongo kwa faida ya kumnufaisha mlalamikaji,” alisema.
Alisema kuna mazingira yanayoonyesha kuwa baadhi ya mashahidi katika kesi za uchaguzi, licha ya kuapa kwa kutumia misahafu, lakini wanashiriki kuidanganya mahakama.

Jaji Ramadhani alisema mafunzo ya sheria ya uchaguzi kwa majaji na mahakimu ni azma aliyokuwa nayo tangu akiwa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Alisema azma hiyo ilitokana na ukweli kwamba hakuna chuo kinachotoa mafunzo ya sheria ya uchaguzi kwa majaji na mahakimu.
Pia alisema maamuzi mbalimbali yaliowahi kufikiwa na mahakama katika kesi hizo, hayakuzingatia taratibu za uchaguzi.

Alisema kuwa maamuzi hayo kwa kiasi kikubwa yalifikiwa kutokana na majaji na mahakimu kutoifahamu vizuri sheria ya uchaguzi.
Maamuzi hayo aliyoyazungumzia Jaji Ramadhani yalihusu hukumu iliyowahi kufikiwa na Mahakama Kuu, kutengua ushindi wa mmojawapo wa wagombea ambao hata hivyo hakumtaja kwa jina.

Alisema hukumu ya kubatilisha ushindi wa mgombea huyo, ilitolewa kwa sababu ya kukuta baadhi ya kufuli na sili za masanduku ya kupigia kura, zikiwa zimechezewa.
Uamuzi mwingine ni ule uliofanywa na Mahakama Kuu wa kutengua sharti la kuweka Sh. milioni tano, kama dhamana ya mtu kuruhusiwa kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge.
Aliwataka mahakimu wanaoshiriki kwenye warsha hiyo, kujifunza kwa umakini kwa kuwa watashughulikia malalamiko na rufaa za uchaguzi zitakazowasilishwa mahakamani.




CHANZO: NIPASHE
 
Tufuatilie kesi ya Mwakalebela labda italeta change
Ila kauli ya JAJI mkuu ni pigo kwa TAKOKURU kwa jinsi wanavyopika kesi za rushwa zisizo na mashiko. Haiwezekani mtu apokee rushwa ndipo akatoe ripoti. toa ripoti kwanza upewe hela za moto za kutimiza lengo kisha waachie takukuru wafanye kazi ndipo utakuwa shahidi mzuri. Haiingii akilini kusema kwamba jamaa juzi alinihonga thumuni nikachukua naomba ashtakiwe. NOOOO WAY
 
Back
Top Bottom