Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, ameziagiza Mahakama za Wilaya na Mahakama za Hakimu Mkazi kuhakikisha zinamjulisha kila mtuhumiwa iwapo kosa linalomkabili linastahili dhamana, kama sehemu ya haki yao ya kikatiba.
Masaju amesema kuwa kutowajulisha washtakiwa kuhusu haki ya dhamana ni moja ya sababu zinazochangia mrundikano wa mahabusu magerezani. Aidha, amebainisha kuwa ucheleweshwaji wa upelelezi na kubambikiziwa kesi kwa baadhi ya watuhumiwa ni miongoni mwa matatizo yanayochangia hali hiyo na kusisitiza kuwa vitendo hivyo ni kinyume cha sheria na haviwezi kuvumiliwa.
Mheshimiwa Jaji Masaju ametoa kauli hiyo jijini Dodoma siku ya Jumanne, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau wa haki jinai wakiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ambapo kikao hicho kililenga kujadili changamoto mbalimbali katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Aidha, Jaji Masaju amesema kuwa ili kukomesha tatizo la watu kunyimwa dhamana kila mshtakiwa anayekabiliwa na kosa linalostahili dhamana anatakiwa kupewa haki hiyo bila vikwazo, kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.