Jaji Mkuu Ibrahim Juma ametugeuka sasa anapotaka Magereza yaongezwe nchini

Jaji Mkuu Ibrahim Juma ametugeuka sasa anapotaka Magereza yaongezwe nchini

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
520
Reaction score
2,930
Mapendekezo yetu siku zote sisi wananchi, Azaki, activists na vyama yapo wazi kabisa sio kuongeza Magereza kila wilaya hapana. Nakumbuka hata wewe Jaji Mkuu umekuwa ukiyapigilia msumari mapendekezo mahususi ya kutatua changamoto ya msongamano wa wafungwa na Mahabusu katika magereza yetu uliwahi toa mapendekezo mazuri sana ambayo hata sisi wananchi tunayaunga mkono, ulipokuwa ukiwaapisha mawakili katika chuo cha sheria tar 20/07/2019.

Pia hata aliyekuwa Naibu waziri wa Mambo ya ndani Ahmadi Masauni aliwahi sema tar 13/Julai/2019 alipokuwa akifanya ziara katika magereza ya Tabora, Geita na Mwanza Butimba.Ila leo Jaji mkuu ametugeuka tofauti na alivyopendekeza awali,unataka Magereza tena.

Siku zote mapendekezo yetu kwa pamoja ya kupunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza yetu sio kujenga Magereza kila wilaya. Hata hata na katu haijawahi kuwa hitaji namna hiyo. Lazima tuanze kutatua changamoto zilizopo katika mifumo yetu ya utoaji haki. (Justice System) ndio sababu kubwa la kuendelea kuwa na msongamano wa Mahabusu na wafungwa katika magereza yetu.

1. Kabla ya kujenga magereza tuanze kwanza kubadili sheria zetu kwa kutoa mwanya wa makosa yote kuwa na dhamana ,(All unbailable offences ziwe bailable ). Kenya wameweza hilo sisi tunashindwa nini? Mahabusu wengi wamejaa magereza sababu kesi zao hazina dhamana. Kama hatuwezi makosa yote kuwa na dhamana basi makosa kadhaa yenye watuhumiwa wengi yawe na dhamana.

2. Kabla ya kujenga Magereza, lazima tuwanyooshee mkono IGP, @policetanzania na ofisi ya DCI (Upelelezi) kwa kuchelewesha upelelezi na kukimbilia kukamata watu kabla ya kumaliza upelelezi. Mahabusu wapo ndani miaka na miaka eti upelelezi haujakamilika. Tuwe na sheria ya kwamba kesi ambayo itatimiza kipindi fulani bila upelelezi kukamilika IFUTWE na mtuhumiwa aachiwe asikamatwe tena kwa shauri hilo hilo.

3. Kabla ya kujenga Magereza, Mahakama zetu zianze kujikita katika kutoa adhabu mbadala pia,sio kifungo kifungo, kifungo.Kosa dogo kifungo. Tujikite pia Adhabu za nje na mbadala mfano,kufanya usafi na njia zingine (Tuangalie sheria zetu)

Serikali inaingia hasara sana kuwahudumia wafungwa na Mahabusu bila sababu, kwanini tusibadili mifumo yetu ya utoaji haki ili kutatua changamoto hizi za msongamano wa wafungwa na Mahabusu katika magereza yetu nchini?

IMG-20210810-WA0176.jpg
 
Jaji mkuu wa Tanzania Prof Juma ameiomba serikali kuongeza kasi ya kujenga magereza ili yawepo kila wilaya nchini.

Source: Mwananchi News
 
Iweke na huruma za kisasa

USSR
 
Kwanini bwashee?

Sasa kama hadi wakuu wa wilaya wanatuhumiwa kwa ujambazi unadhani magereza zilizopo xinatosha?!!
Watu wanatafuta njia mbadala za kutoa hukumu yeye anakuja na ustaarabu wa zamanii miaka ya 80
 
Back
Top Bottom