Jaji Mkuu, kagueni mahakama za mwanzo, wananchi wanateseka sana

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Shikamoo Baba yangu. Habari za uzima. Naamini Mungu ametuwezesha kuamka salama ili tuweze kuwatumikia wananchi wetu.

Baba yetu, Mzee wetu — leo nimeona nikujuze tu kuhusu yanayoendelea kwenye mahakama za mwanzo.

Mheshimiwa Jaji Mkuu,
Mahakimu wa mahakama za mwanzo wanatesa sana wananchi. Wanawaumiza sana wananchi wasio na uwezo. Yaani hata watu wanaokwenda jela, si wote wana makosa.

Mheshimiwa Jaji Mkuu, kuna wafanyabiashara wenye pesa wakiamua kukuweka ndani, unafungwa kifungo atakacho yeye — mhusika mwenye nguvu au ushawishi.

Hata ujitetee vipi, mahakimu wengine wamekuwa hawatoi msaada kabisa, hawaelewi au hawataki kuelewa.

Niliaga sana na nilishaandika malalamiko, hasa kuhusu mirathi na jinsi inavyotesa wananchi kwenye hizi mahakama za mwanzo.

Kwa kweli, zimekuwa siyo mahakama za msaada. Wakati mwingine, unapoamua kusaidia mtu unajiuliza: Kwa nini nimefika huku? Lakini wakikutana kule, wanasikiliza kesi moja kwa moja — hata kama awali walipanga kuimaliza mwaka unaofuata, ghafla wanaihitimisha wiki inayofuata!

Mheshimiwa Jaji Mkuu, kuhusu kuahirishwa kwa kesi:
Hii imekuwa sehemu mojawapo ya rushwa na mateso. Nawaomba kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, awape nguvu. Nendeni mkakague kesi za Kanda ya Kaskazini — Arusha, Moshi, Rombo, Mwika.

Wananchi wanateseka. Wanalia mahakamani. Zipo kesi za mirathi — amebaki mwanamke na watoto wake — na wamama wanateseka hadi wanafariki, pamoja na kupeleka nyaraka zote zinazotakiwa.

Zipo kesi za mirathi za miaka 7…8, na nyaraka zote zipo halali. Unajiuliza: Shida ni nini? Hazimalizwi tu.

Njia mojawapo wanayotumia ni kuahirisha kesi mara kwa mara.

Nendeni mkakague mahakama za mwanzo, na siyo Kaskazini tu — bali kote nchini. Shida ni nini kesi hazimalizwi? Nendeni mkachunguze chanzo cha kuahirishwa kwa kesi.

Biblia inasema: “Ukiijua kweli, nayo kweli itakuweka huru.”

Zipo kesi ambazo Mungu amesaidia watu wachache kupitia mahakama za mwanzo, na wamepata haki zao. Wapo pia waliopata mirathi yao kihalali.

Lakini wengine ukiwauliza: Mbona mama analia? Anakuambia: “Nina mwaka wa tano hapa mwanangu. Nimeleta kila kitu. Kila nikija, naambiwa nimpe fulani kiasi fulani ili amalize kesi. Nikitoa pesa, siku ya kesi naambiwa imeahirishwa.” Unajiuliza: Shida yangu ni nini? Habari za mume wangu zote zipo — au wanataka nife ndio warithi?

Mheshimiwa, wakisema haya maneno, hii ni laana kubwa. Tuiweke pembeni kwa gharama yoyote.

Waamshe wakaguzi waende mahakamani. Wawaulize wananchi waliokuta kule nani ana malalamiko.

Na tafadhali, msiwajulishe mapema kwamba mnaenda kukagua — kwa sababu wakijua, huwa wanaahirisha zile kesi wanazojua zitawachoma wakifuatiliwa. Wananchi wanapigiwa simu kabisa kuwa kesi zimeahirishwa.

Tunataka kwenda mbinguni.
Tutende haki.

Wakaguzi, tuamke! Maumivu haya — Mungu hayaachi yapite hivi hivi. Tukifa, tuache historia njema wapendwa, si historia ya kuumiza watu.

Tuwe watu wa kutimiza ramani ya maisha yetu.

Mungu anapotupa nafasi ya kusaidia jamii — hiyo ni sadaka maalum katika maisha yako. Pale unapofanya mema, ndipo na Mungu anaendelea kusaidia na kubariki kizazi chako.

Wapo marubani nje ambao watoto wao nao wamekuwa marubani.

Wapo majaji ambao watoto wao wote wamekuwa majaji.

Hizi ndizo baraka ambazo Mungu ametupa.

Mungu atubariki.
 
Sema mwanzo mpaka mwisho wa mahakama. Ile kesi ya ubakaji Dodoma aliyewatuma kisa anacheo alilindwa ikiwa mahakama inajua sheria. Uozo ni mahakama za mwanzo mpaka mwisho.
 
Kazi ya muhimu ya kwanza ya mahakama ni kuhakikisha mwenye haki anakataliwa, poleni sana wana Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…