Jaji Mkuu Masaju awataka Mawakili wasiwe wanaharakati!!

Jaji Mkuu Masaju awataka Mawakili wasiwe wanaharakati!!

..ni tamko la CJ Masaju.

..na video ziko mitandaoni.
Basi amekosea. Watu pekee ambao hawatakiwi kuwa wanaharaki ni majaji na ofisi ya DPP. Hawa hawapaswi kuegemea upande wowote kati ya serikali na wananchi. Ndio maana ingekuwa vyema kama Jaji Mkuu angejitenga na shughuli za serikali. DPP nae anatakiwa kuzingatia haki za mtuhumiwa anapofungua na kuendesha kesi. Jaji nae anapaswa kulinda haki hii kwa wivu mkubwa. Jaji anaezingatia haki ya mtuhumiwa hawezi kuruhusu kesi iendelee bila kuwa na kikomo.

Amandla...
 
Kwa mwenendo wa nchi ulivyo hiyo kauli ya Jaji inaonekana anatetea upande fulani
kwa kauli hiyo anapaswa kujiuzulu kwa heshima

Nilitegemea angekemea utekaji, upoteaji na kuuwawa kwa watu na serikali kuingilia uhuru na maamuzi ya mahakama
 
Basi amekosea. Watu pekee ambao hawatakiwi kuwa wanaharaki ni majaji na ofisi ya DPP. Hawa hawapaswi kuegemea upande wowote kati ya serikali na wananchi. Ndio maana ingekuwa vyema kama Jaji Mkuu angejitenga na shughuli za serikali. DPP nae anatakiwa kuzingatia haki za mtuhumiwa anapofungua na kuendesha kesi. Jaji nae anapaswa kulinda haki hii kwa wivu mkubwa. Jaji anaezingatia haki ya mtuhumiwa hawezi kuruhusu kesi iendelee bila kuwa na kikomo.

Amandla...

..kulinda haki kwa wivu mkubwa ndio uanaharakati wenyewe.
 
..kulinda haki kwa wivu mkubwa ndio uanaharakati wenyewe.
Hapana. Majaji wetu anatakiwa kuwa reactive na sio pro active. Jaji akiona mtu anaonewa hawezi kuchukua hatua mpaka anayeonewa alalamike. Akilalamika ndio anapaswa kuhakikisha haki yake inalindwa kwa wivu mkubwa. Jaji anapaswa kuongozwa na sheria tu anapofanya maamuzi na sio mawazo au imani yake binafsi. Clarence Thomas ni activist judge.

Mwanaharakati ni proactive. Hangojei kulalamikiwa hasa kwa sababu mara nyingi wanaoonewa hawajui kuwa wanaonewa.

Mwana harakati akiona mtu/watu hawatendewi haki anawaelimisha kuhusu haki zao na anasimama nao katika kumkabili mbaya wao. Jaji anatakiwa kuwa neutral wakati mwanaharakati anaweka wazi msimamo wake na yuko upande gani. Wengi wanakuwa upande wa haki lakini wako wanaosimama na madhulmati.

Amandla...
 
Ninaposema kuwa Jaji hatakiwi kuwa activist nina maanisha kuwa k.m. anapotoa hukumu katika ugawaji wa mali baada ya kesi ya talaka ambapo mume amemfumania mke wake hapaswi kumnyima mwanamke haki yake kwa sababu imani yake inakataza uzinifu. Anapaswa kuangalia tu sheria inampa stahili gani mke katika mgawanyo wa mali baada ya taraka bila kujali kuwa ni mzinifu.

Amandla...
 
Hapana. Majaji wetu anatakiwa kuwa reactive na sio pro active. Jaji akiona mtu anaonewa hawezi kuchukua hatua mpaka anayeonewa alalamike. Akilalamika ndio anapaswa kuhakikisha haki yake inalindwa kwa wivu mkubwa. Jaji anapaswa kuongozwa na sheria tu anapofanya maamuzi na sio mawazo au imani yake binafsi. Clarence Thomas ni activist judge.

Mwanaharakati ni proactive. Hangojei kulalamikiwa hasa kwa sababu mara nyingi wanaoonewa hawajui kuwa wanaonewa.

Mwana harakati akiona mtu/watu hawatendewi haki anawaelimisha kuhusu haki zao na anasimama nao katika kumkabili mbaya wao. Jaji anatakiwa kuwa neutral wakati mwanaharakati anaweka wazi msimamo wake na yuko upande gani. Wengi wanakuwa upande wa haki lakini wako wanaosimama na madhulmati.

Amandla...

..Jaji Mwanaharakati hawezi kuruhusu " technicalities " zicheleweshe mwenendo wa shauri analolisimamia.

..hapo umemtaja Jaji Clarence Thomas wa Marekani, mimi ningependa kumtaja Jaji Thurgood Marshal kama mfano wa Mwanasheria, na Jaji Mwanaharakati.
 
..Kichwa cha habari kinahusika.

..Kwa kweli kauli ya Jaji Mkuu imenishangaza.

..Lakini zaidi imenisikitisha, na kuniudhi.

..Hivi Wakili ktk nchi zetu za Kiafrika, anayetetea HAKI za watu, anaachaje kuwa Mwanaharakati?

..Kusipokuwa na Mawakili wanaharakati nani atawatetea wananchi wanyonge?

..Na Jaji Mkuu Masaju hakueleza kwanini hataki Mawakili wawe wanaharakati.

..Hakufafanua wanaharakati wana kasoro gani ktk utoaji wa HAKI hapa nchini.

..Je, wanaharakati ni kikwazo ktk utoaji wa HAKI, na utendaji wa Mahakama hapa nchini?

..Jaji Mkuu Ibrahim Juma aliwahi kusema Mahakama anayoiongoza haitatoa ushirikiano kwa wanaharakati.

..Naona Jaji Mkuu Masaju naye anatembea mulemule alipokuwa akitembea mtangulizi wake.

..Kwa kauli za Raisi, na Jaji Mkuu, kuhusu wanaharakati, wanaosema nchi yetu inahitaji KUKOMBOLEWA hawajakosea.
Huyu hastahili hata kuwa "karani wa mahakama" sijui alipataje kuwa jaji! Inatakiwa elimu yake ichunguzwe. Kiti anachokalia inabidi kipakwe upupu.
 
..Jaji Mwanaharakati hawezi kuruhusu " technicalities " zicheleweshe mwenendo wa shauri analolisimamia.
Jaji yeyote anayependa haki hawezi kuruhusu mtuhumiwa aendelee kusota rumande kwa sababu zisizo na msingi. Nakumbuka kuna Jaji alimtoa rumande Lema na kuwasema vibaya waendesha mashtaki kwa kutaka aendelee kukaa ndani kwa sababu "uchunguzi haujakamilika". Yule Jaji hakuwa activist bali mtenda haki. Jaji yeyote anayekubali kesi iendelee kuahirishwa kwa miaka mingi kwa sababu DPP hajakamilisha uchunguzi anafanya mockery ya Katiba ya Nchi.
..hapo umemtaja Jaji Clarence Thomas wa Marekani, mimi ningependa kumtaja Jaji Thurgood Marshal kama mfano wa Mwanasheria, na Jaji Mwanaharakati.
Thurgood Marshall alikuwa mwana harakati kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji. Alihusika sana katika kumtafuta Rosa Park lakini alipokuwa Jaji alikuwa anasimamia haki. Clarence Thomas ni activist kwa sababu katika maoni yake akiwa mezani amekuwa akitoa ushauri kwa wanasheria wa kulia wa namna ya kushinda kesi. Ushauri wake ulitumiwa na Jaji Aileen Connor kutosa kesi dhidi ya Trump.

Amandla...
 
Back
Top Bottom