Jaji Mkuu Masaju: Kesi ya mwezi mmoja mnasema ichukue miaka miwili. Hiyo Mahakama itaheshimika?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji George Masaju katika ufunguzi wa wiki ya Usuluhishi Aprili 09, 2026 Wiki ya Usuluhishi, inayofanyika katika Ukumbi wa PSSSF Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam tarehe 9 Aprili, 2026, amekemea vikali Mahakama kukaa na shauri kwa muda mrefu.

Aidha, Jaji Masaju amebainisha kuwa kuna kesi zinapangwa kabisa muda wa usikilizwaji kuwa uwe miezi minne, miaka miwili na pande zote mbili zinakubaliana, Masaju amesema jambo hili linasababisha watu kutopata haki kwa wakati, "Mahakama sio sehemu ya kupaki kesi"

Your browser is not able to display this video.

​
 
Kwani hasa kinachocheleweaha KESI hua ni nini,je mahakimu,majaji na wengine kwenye circle ya mahakama hua wanawajibishwa na nani?lakini pia katika kuongea ongea na waliowahi kua na kesi nzito mahakamani wanasema kama wewe ni mshitakiwa ukataka kesi iende haraka basi utafungwa na kama ni mshitaki usikubali kesi icheleweshwe utakosa haki kwakua mshitakiwa wako anaendelea kujipanga.
 
KAMA KESI YA T.A.L....kesi imeisha kitambo ila mnaendelea kumshilikilia...ipo siku mtaingiza hii nvhi kwenye mauaji ya kutisha kwa chuki na hasira mnajengea watu....mahkma zmekuwa kma T.P...
 
Posho mkuu, kesi inavyozidi kuwa ndefu ndio mawakili, majaji wanatengeneza pesa. Otherwise ni mazoea tu, ni kama NIDA unajiuliza kinachofanya kitambulisho kichukue miaka ni nini hauelewi. Wanapenda urasimu na kujiona wa muhimu
 
Mbwa asiye na meno kamwe hawezi kung'ata. Zaidi ataishia kubweka tu
 
Mbona kesi ya Lissu imekaa muda mrefu hakuna walichofanya wamekuja na mashahidi wamewaficha kwenye boxi wapi ni uhuni tu leo anakuja kuongea vitu tofauti kabisa kama havipo kwenye maeneo yake ya kazi.
 
Mpaka Leo bado anauma na kupuliza! Huu ni unafique wa viwango vya juu mno
 
Huyu jamaa huwa sijui ana akili gani tu!! Kila siku yeye analalamika yaleyale tu..wakati yeye ndo jaji mkuu!?Kwa nini asije na suruhisho..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…