Jaji Mkuu Masaju: Nawashauri watumishi tusiwe wanaharakati kudai haki

Jaji Mkuu Masaju: Nawashauri watumishi tusiwe wanaharakati kudai haki

..kwanini Jaji Mkuu Masaju asilishauri Bunge litunge sheria kwamba uanaharakati ni kosa la jinai?

..Masaju na Ibrahim ni majaji wakuu wa ajabu na wa hovyo kabisa.
 
..kwanini Jaji Mkuu Masaju asilishauri Bunge litunge sheria kwamba uanaharakati ni kosa la jinai?

..Masaju na Ibrahim ni majaji wakuu wa ajabu na wa hovyo kabisa.
Nahisi anazungumzia watumishi wa Mahakama. Nisichoelewa ni kama hataki wasiwe wanaharakati katika kudai haki zao kama watumishi wa Mahakama au haki za watanzania wenzao?

Amandla...
 
Uanaharakati ni nini? Maana naye hapo yupo kwenye harakati.
 
Mtu ambaye si mwanaharakati wa haki, huyo anawezaje kuhukumu kwa haki?

Au yeye haelewi nini maana ya mwanaharakati? Hao ni wafuasi/mawakala wa haki unapokataa watumishi wa mahakama wasiwe hivyo maana yake unapinga Mfumo wa haki mahakamani badala yake wafanye kwa matakwa watu
 
Mbinu za kuwafunga midomo wafanyakazi, kuwafanya wawe watumwa wa mifumo kandamizi bila kuhoji au kuuliza chochote
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, amewashauri watumishi wa mahakama na watumishi kwa ujumla kutokuwa wanaharakati katika kudai haki, akisisitiza umuhimu wa kutumia njia na taratibu zinazotambulika katika kutafuta haki zao.

Soma Pia: Jaji Mkuu Masaju Aonya Mahakama Kuishi Kwa Maelekezo

Yeye mwenyewe anaonesha double standard. Anapowakataza hao watumishi wasiwe wanaharakati, anatakiwa pia awashauri watimize majukumu yao kwa kufuata taratibu za kiutimishi; badala ya kuwa CHAWA au watu wa kutekeleza majukumu yao kwa kujipendekeza kwa wanasiasa.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, amewashauri watumishi wa mahakama na watumishi kwa ujumla kutokuwa wanaharakati katika kudai haki, akisisitiza umuhimu wa kutumia njia na taratibu zinazotambulika katika kutafuta haki zao.

Soma Pia: Jaji Mkuu Masaju Aonya Mahakama Kuishi Kwa Maelekezo

Malisa Godlisten Leo alikuwa safarini kutoka Marekani ambapo amekuwa kwa zaidi ya miezi tisa (9), tangu alipoenda kuiwakilisha nchi yetu kama mtanzania pekee aliyechaguliwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kwenda kupata mafunzo ya uongozi. Fursa ambayo hujitokeza kwa watanzania wachache sana kama ilivyowahi kutokea kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Alipofika Nairobi- Kenya asubuhi ya leo, alishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi unaondelea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Hivyo aliamua kusafiri kwa usafiri binafsi mpaka Namanga ambao ni mpaka kati ya nchi yetu na Kenya ili kuingia nchini kupitia Arusha.

Aliwasili Namanga majira ya saa tisa(9) mchana na kwenda kwa maafisa uhamiaji ili kugongewa hati ya kusafiria (Passport) na hatimaye kuingia nchini kama utaratibu unavyotaka.

Baada ya kufika kwa maafisa uhamiaji hao, walichukua hati yake ya kusafiria na kumwambia kuwa haisomeki kwenye mfumo (system) hivyo wao hawana namna ya kufanya mpaka mkuu wao (in- charge) aje ndio anaweza kuona kwenye mfumo.

Kutokana na kadhia hiyo, na kwa kuwa aliambiwa Mkuu huyo hayupo kwa muda Malisa GJ aliendelea kukaa katika ofisi hizo za uhamiaji akisubiri Mkuu huyo kuja na kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.

Cha kushangaza ilipofika saa moja jioni, alichukuliwa na gari ambalo si la Polisi jeupe Double Cabin na kupelekwa kituo cha Polisi Longido. Hata hivyo gari hilo halikukaa sana likaondoka kuelekea uelekeo wa Arusha.

Mpaka natoa taarifa hii hakuna taarifa kamili za aliko Malisa GJ na nini ni sababu ya kukamatwa kwake. Aidha simu zake zote zimezimwa tangu alipokuwa anatolewa Namanga.

Nitoe rai kwa Polisi na Uhamiaji kumwachia huru mara moja au kuhakikisha wanatoa taarifa kwa umma za aliko Malisa GJ na sababu ya kukamatwa kwake. Kama haitoshi kuhakikisha anapewa haki zake za kisheria ikiwemo kuonana na mawakili wake na haki ya Mawasiliano.

Dickson Matata (Wakili)
31/8/2026
Arusha-Tanzania.
 

Attachments

  • e773c1bd-d6de-4bec-acb8-a6f6b8fa6d72.jpeg
    e773c1bd-d6de-4bec-acb8-a6f6b8fa6d72.jpeg
    72.3 KB · Views: 9
  • Screenshot 2026-08-31 at 14-41-33 Instagram.png
    Screenshot 2026-08-31 at 14-41-33 Instagram.png
    1,007.3 KB · Views: 8
Jaji la hovyo kuwahi kutokea katika historia, halina tofauti na machawa kama Lucas Msandambwa,ameigeuza taasisi kuwa mahakama ya mbuzi 👎🤮
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, amewashauri watumishi wa mahakama na watumishi kwa ujumla kutokuwa wanaharakati katika kudai haki, akisisitiza umuhimu wa kutumia njia na taratibu zinazotambulika katika kutafuta haki zao.

Soma Pia: Jaji Mkuu Masaju Aonya Mahakama Kuishi Kwa Maelekezo

Huyu naye haeleweki na vimaneno neno vyake vya kipuuzi kila mara.

Sijui anasimamia wapi.

Kwa hiyo hapa anawahimiza wafanyakazi wapuuze HAKI, wafanye nini sasa wageuke wote kuwa CHAWA?
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju, amewashauri watumishi wa mahakama na watumishi kwa ujumla kutokuwa wanaharakati katika kudai haki, akisisitiza umuhimu wa kutumia njia na taratibu zinazotambulika katika kutafuta haki zao.

Soma Pia: Jaji Mkuu Masaju Aonya Mahakama Kuishi Kwa Maelekezo

Angeheshimika sana kama angetoa mapendezo ya mabadiliko ya katiba ili majaji wasiwe wateule wa raisi ili waweze kufanyakazi zao kwa uhuru bila kuwa chawa-based.
 
Nahisi anazungumzia watumishi wa Mahakama. Nisichoelewa ni kama hataki wasiwe wanaharakati katika kudai haki zao kama watumishi wa Mahakama au haki za watanzania wenzao?

Amandla...
Itakuwaje kudai HAKI iwe tatizo bila kujali ni mtumishi wa mahakama au ni Mwanaharakati?
Kwa nini asizungumzie "kunyima HAKI"; maana kukiwa hakuna kunyima haki, hapatakuwepo na kuidai hiyo HAKI

Kuna sababu zipi zinazohusisha kudai HAKI na Uanaharakati? Ukidai haki, wewe tayari unatambulika kuwa mwanaharakati!.
 
Back
Top Bottom