McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Mafunzo ya Namna Bora ya Uendeshaji wa Mashauri ya Uchaguzi yaliyokuwa yakitolewa kwa Majaji, Naibu Wasajili na Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama za Hakimu Mkazi na za Wilaya nchini yamehitimishwa leo, huku Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akishauri kwamba Kanuni za Uchaguzi zifanyiwe marekebisho (electoral laws) ili kuwawezesha Majaji na Mahakimu kusikiliza ipasavyo mashauri hayo.
Akizungumza leo tarehe 18 Septemba, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo hayo yaliyohusisha washiriki wa kundi la mwisho la Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Masaju amesema majadiliano mbalimbali pamoja na changamoto zilizowasilishwa na washiriki wa Mafunzo yameonesha kuwa, kanuni hizo zina mapungufu na hivyo kuwa na haja ya kuzifanyia mabadiliko.
“Niwashukuru kwa kukubali kufanya mabadiliko ya kanuni hizi zinazotungwa na Jaji Mkuu, tumepata ushauri mzuri hapa na Jaji Mkuu Mstaafu ametushauri maeneo ya kuangalia , tuna pa kuanzia na wawezeshaji wetu ni mahiri na ninyi wenyewe ni mahiri mna ustadi mkubwa kwenye maeneo haya na hili tutalifanya kabla ya tarehe ya uchaguzi wenyewe na litakuwa zoezi shirikishi lakini maboresho ya mwisho yatakayotolewa lazima yapate kibali cha Mahakama maana sisi ndio wenye ile sheria na mwenye mamlaka ya kuitunga ile sheria ni Jaji Mkuu,” amesema Mhe. Masaju.