Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Jaji Mkuu mstaafu, Chande Othman amewataka majaji wa Mahakama Kuu kumaliza haraka kesi wanazopangiwa, ili kuondoa wasiwasi kwa jamii na wao kujiweka huru.
Amesema ucheleweshaji wa kesi zikiwamo zenye mvuto huku akiitolea mfano kesi ya wabunge- Halima Mdee na wenzake 18 wanaopinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, mbali na kuwapa wasiwasi wananchi, pia zinatoa nafasi kwa vyombo vya habari kuandika mengi.
Alitoa rai hiyo juzi wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya majaji 22 wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Zanzibar inayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).
Alisema kutokana na muundo wa Mahakama, jaji ndiye anayejipangia ratiba ya usikilizaji wa mashauri aliyopangiwa, kwa hivyo hana sababu ya kuchelewesha utoaji wa hukumu na kuwapa nakala ya hukumu walalamikaji ili kama hawajaridhika wakate rufaa.
“Jambo la msingi ni kuwa kila jaji wa Mahakama Kuu anajiendesha mwenywe kwa mashauri aliyopangiwa na siyo mawakili au wenye mashauri,” alisema Jaji Chande.
Alisisitiza kitu ambacho kinaweza kuwaacha huru majaji ni kutoa hukumu kwa haraka katika kesi au mashauri yenye mvuto ikiwamo kesi ya wabunge 19.
“Kesi yenye mvuto kwa jamii kama ya wabunge 19 ikisikilizwa haraka, hukumu ikatolewa na nakala ya hukumu ikaharakishwa, itatoa nafasi kwa upande ambao haujaridhika kukata rufaa,” alisema.
“Hii inaondoa wasiwasi kwa wananchi na presha kwa jaji aliyepangiwa kuisikiliza inaondoka,” aliongeza Jaji Chande.
Chanzo: Mwananchi