Jaji mkuu: Rushwa imekithiri mahakamani, polisi na taasisi nyingine za Serikali

IMG_7951.jpeg

Maana yake hili jumba lenye gharama la mabillioni ya walipa kodi ni pambo.

Sio maneno yangu ndio kauli ‘jaji mkuu’ kwa lugha nyingine; system ni hovyo.

Hakuna serikali kwa lugha ngumu.

Sada kama polisi rushwa, mahakamani rushwa na taasisi serikalini rushwa.

Huo si ndio msingi ☝️wa banana republic kwa mujibu wa mahakama.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju, amesema changamoto ya rushwa bado ipo ndani ya taasisi muhimu za utoaji haki, akisisitiza kuwa nidhamu na uwajibikaji ndiyo nguzo kuu zitakazosaidia Mahakama kufikia hadhi inayokusudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza Septemba 24, 2025 jijini Dodoma, wakati wa kufungua mkutano maalumu wenye ajenda ya “Ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki” uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya Jaji Mkuu, Masaju amesema hakuna haki itakayoweza kupatikana ikiwa Mahakama itaendelea kusumbuliwa na vitendo vya rushwa.

“Hatuwezi kujifanya kwamba rushwa hazipo kwenye taasisi zetu, zipo, zipo mahakamani, zipo polisi, ziko kwenye taasisi nyingine zote, zipo. Imeandikwa hapa kwenye hii Dira, wamesema taasisi zinazohusika na utoaji haki zimegubikwa na uzembe na rushwa, hii itapunguzwa rushwa.,” amesema.

Amefafanua kuwa Mahakama mara nyingi hujikuta kwenye mazingira magumu kutoa maamuzi sahihi kutokana na upungufu wa ushahidi, tofauti na Mahakama Kuu ambayo pande zote zinakuwa na ushahidi kamili unaoiwezesha kutoa maamuzi kwa ufanisi.

Katika hatua nyingine, Jaji Masaju aliitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuacha tabia ya kuwatetea watu wanaoshtakiwa kwa kesi za madai, akisema ni matumizi mabaya ya madaraka.

“Hizi ni kesi za madai. Wengine wanashtakiwa, mnaenda mnawatetea. Waacheni wapambane na hali zao wenyewe. Haiwezekani mtu akibambikiza kesi atetewe kwa kisingizio cha kutekeleza majukumu ya ofisi. Hii ni matumizi mabaya ya madaraka. Kama kuna kesi kama hizo, wacha DPP azisimamie kwa mujibu wa sheria,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, hatua hiyo itasaidia kujenga nidhamu ya utumishi wa umma, kuongeza uadilifu, kuharakisha upelelezi kwa makini na kuhakikisha kesi zinamalizika mapema bila kucheleweshwa.

“Upelelezi ukifanyika mapema na kwa makini, hata maamuzi nayo yatatolewa haraka. Hii itasaidia pia majaji na mahakimu kufanya maamuzi yenye umakini, maana ushahidi watakuwa nao tangu mwanzo na wanaweza kuuliza maswali ya ufafanuzi ipasavyo,” ameongeza.

Pia Soma: GE2025 - Jaji Masaju aagiza mashauri ya uchaguzi yamalizwe mapema kujenga imani kwa Mahakama
​

Chanzo: Jambo Tv​
Hapa anamuongelea judge Kiswaga wa mahakama ya Kisutu. Ukimwangalia tu utaona kama ana matatizo ya akili. Yupo kama ana shida tangu kuzaliwa, halafu anategemea amtetee mama ili apandishwe cheo kwa sababu hawezi kupanda kwa merit, ila kwa uchawa.
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju, amesema changamoto ya rushwa bado ipo ndani ya taasisi muhimu za utoaji haki, akisisitiza kuwa nidhamu na uwajibikaji ndiyo nguzo kuu zitakazosaidia Mahakama kufikia hadhi inayokusudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza Septemba 24, 2025 jijini Dodoma, wakati wa kufungua mkutano maalumu wenye ajenda ya “Ushirikiano na mahusiano katika utekelezaji wa majukumu ya utoaji haki” uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya Jaji Mkuu, Masaju amesema hakuna haki itakayoweza kupatikana ikiwa Mahakama itaendelea kusumbuliwa na vitendo vya rushwa.

“Hatuwezi kujifanya kwamba rushwa hazipo kwenye taasisi zetu, zipo, zipo mahakamani, zipo polisi, ziko kwenye taasisi nyingine zote, zipo. Imeandikwa hapa kwenye hii Dira, wamesema taasisi zinazohusika na utoaji haki zimegubikwa na uzembe na rushwa, hii itapunguzwa rushwa.,” amesema.

Amefafanua kuwa Mahakama mara nyingi hujikuta kwenye mazingira magumu kutoa maamuzi sahihi kutokana na upungufu wa ushahidi, tofauti na Mahakama Kuu ambayo pande zote zinakuwa na ushahidi kamili unaoiwezesha kutoa maamuzi kwa ufanisi.

Katika hatua nyingine, Jaji Masaju aliitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuacha tabia ya kuwatetea watu wanaoshtakiwa kwa kesi za madai, akisema ni matumizi mabaya ya madaraka.

“Hizi ni kesi za madai. Wengine wanashtakiwa, mnaenda mnawatetea. Waacheni wapambane na hali zao wenyewe. Haiwezekani mtu akibambikiza kesi atetewe kwa kisingizio cha kutekeleza majukumu ya ofisi. Hii ni matumizi mabaya ya madaraka. Kama kuna kesi kama hizo, wacha DPP azisimamie kwa mujibu wa sheria,” amesisitiza.

Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, hatua hiyo itasaidia kujenga nidhamu ya utumishi wa umma, kuongeza uadilifu, kuharakisha upelelezi kwa makini na kuhakikisha kesi zinamalizika mapema bila kucheleweshwa.

“Upelelezi ukifanyika mapema na kwa makini, hata maamuzi nayo yatatolewa haraka. Hii itasaidia pia majaji na mahakimu kufanya maamuzi yenye umakini, maana ushahidi watakuwa nao tangu mwanzo na wanaweza kuuliza maswali ya ufafanuzi ipasavyo,” ameongeza.

Pia Soma: GE2025 - Jaji Masaju aagiza mashauri ya uchaguzi yamalizwe mapema kujenga imani kwa Mahakama
​

Chanzo: Jambo Tv​
Huyu jaji kichaa anaongea na kubadilika badilika kama kinyonga.....shame on him.
 
Back
Top Bottom