Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Jaji Mkuu Mstaafu wa Kenya, David Maraga, amekamatwa na Polisi asubuhi ya Jumatatu, Juni 8 2026, muda mfupi baada ya kuanza maandamano dhidi ya ujenzi wa miundombinu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Nairobi. Waandamanaji wengine tisa pia walikamatwa pamoja naye.
Polisi na maafisa wa kulinda misitu KWS wanatuhumiwa kuharibu takriban ekari 76 za msitu wa asili ndani ya hifadhi, kufuatia leseni ya mamlaka ya kulinda mazingira NEMA kubadilisha eneo la "Low Use Zone" lililohifadhiwa.
Eneo hilo litajengewa Hospitali ya Wanyama ya Nairobi Animal Orphanage na eneo la magari la ekari 8 kwa ajili ya jumba la kimataifa la mikutano la Bomas, kwa shilingi bilioni 41.9. Mpango pia unajumuisha daraja la watembea kwa miguu kuvuka barabara ya Lang’ata, jambo lililozua maswali kuhusu mpaka kati ya uhifadhi wa wanyamapori na miradi ya kibiashara.