Jaji Mstaafu Robert Makalamba: Watanzania hawakutaka mfumo wa vyama vingi, Nyerere ndio alitaka

Jaji Mstaafu Robert Makalamba: Watanzania hawakutaka mfumo wa vyama vingi, Nyerere ndio alitaka

Yuko sahihi asilimia 80 walikataa vyama vingi.

..Na asilimia 90% ya Watanzania hawajui katiba ni kitu gani.

..Pia katiba haileti maji, barabara, shule, wala chakula.

..Sasa unajiuliza kwanini CCM waliandika katiba mwaka 1977?
 

Katiba haiwezi kuwa juu ya Mwenyezi Mungu....."​


"Watanzania hawakutaka mfumo wa vyama vingi,Nyerere ndio alitaka"-Jaji Mstaafu,Robert Makalamba katika semina ya mawakili wanaotetea Haki za Binadamu Zanzibar,iliyoandaliwa na THRDC.
Watanzania hata chanjo ya Corona hawataki. Hata Katiba iliyopo haikuombwa na hawa watanzania kwa uwingi tunaotaka. Wanaamua wachache kwa faida ya wengi.
 
..Na asilimia 90% ya Watanzania hawajui katiba ni kitu gani.

..Pia katiba haileti maji, barabara, shule, wala chakula.

..Sasa unajiuliza kwanini CCM waliandika katiba mwaka 1977?
Naungana na ww, kama wanaamini kuwa Katiba haileti shule, Barabara wala maji, kwa nini iliandikwa, na kwa makusudi gani, kutoka kwa Nani kwenda kwa Nani.
 
Aliyeruhusu vyama vingi baada ya kusikiliza wataalamu na tafsiri ya matakwa ya wananchi ambayo yanapatikana katika mfumo wa vyama vingi ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Msimpe credit asiyehusika.

Aliyeua Azimio la Arusha baada ya kuona halina manufaa kwa Taifa ni Ali Hassan Mwinyi kupitia Azimio la Zanzibar.

Aliyeua Siasa za ujamaa ambao serikali ndio ilikuwa mmiliki wa uchumi ni Ali Hassan Mwinyi. Ndio maana leo kuna matajiri.

Nyerere alidhani Mwinyi ni mdhaifu angemuongoza kwa remote, alikuja kulalamika kuwa Mwinyi anashauriwa na mkewe! Akaita Pale Kilimanjaro hotel
 
Watanzania ni hawa wa sasa hivi sio wale zidumu fikra za mwenyekiti wa chichiemu
 
Yale yake kwenye nchi ya watanganyika,mtu mmoja akatuamlia tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi wakati majority ya watanganyika hawakutaka mfumo huu,na majaji njaa wakawa kimya tu
Hawakutaka au walikuwa wanaogopa kusema ukweli? Kwanza Zanzibar asilimia kubwa walitaka vyama vingi, pili Nyerere alitambua hilo ndiyo maana akageuza hoja na kusema watanzania wapewe vyama vingi.
 
Back
Top Bottom