Jaji Mutungi, kama sheria ipo lakini kuna msuguano wanaosuguana hawasuluhishwi

Jaji Mutungi, kama sheria ipo lakini kuna msuguano wanaosuguana hawasuluhishwi

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Kitendo cha kuvitaka vyama vya siasa vikutane na jeshi la polisi kupata usuluhishi kuhusu haki ya kufanya siasa ni kukwepa wajibu wako, vyama husika vipo kisheria na viliposajiriwa vilipata maelekezo yote ya kikatiba, sidhani kama vilipata maelekezo ya kutokufanya siasa bila ya makubaliano na jeshi la polisi.

Hata hivyo kama ulipovisajiri sheria ya kufanya siasa ulivyovipa ni moja ni vipi Chama Cha Mapinduzi kinafanya siasa kwa sheria ulizowapa hakina msuguano na polisi na vingine vinafuata sheria hizohizo vinamsuguano na polisi!

Wewe ni Jaji na unajua fika kuwa endapo vikundi viwili vinamsuguano wa kisheria wewe hautakiwi kuvipatanisha nje ya sheria bali mahakama ndiyo inayotakiwa kutoa suluhisho, suluhu nje ya mahakama ni jambo la hiari ambapo kutekeleza si lazima.
 
Kitendo cha kuvitaka vyama vya siasa vikutane na jeshi la polisi kupata usuluhishi kuhusu haki ya kufanya siasa ni kukwepa wajibu wako, vyama husika vipo kisheria na viliposajiriwa vilipata maelekezo yote ya kikatiba, sidhani
Halafu kuna wapumbavu wanaona ni sawa tuu ccm kuwa huru kufanya shughuli zake za kisiasa huku vyama vingine vinazuiwa.

Ni mpumbavu tuuu ndio atana kua mtungi yuko sawa.
 
CCM wanafanya siasa za kipumbavu sana
CCM wanampa wakati mgumu sana Jaji Mutungi, jana Jumatatu Jaji Mutungi alionekana kwenye runinga ITV akijaribu kuelezea kuhusu mikutano atakayoifanya na jeshi la polisi kisha na vyama vya siasa, Jaji Mutungi alionekana kama ni mtu anayejilazimisha kuchukua hatua hizo kinyume na sheria huku akijua kuwa ni uvunjaji wa katiba.

Tutegemee kumsikia Jaji Mutungi anaviambia vyama husika kuwa haviruhusiwi kufuata sheria za uendeshaji wa vyama vyao bila ridhaa ya polisi! Jaji Mutungi kazi anaitaka, kuwaambia polisi vyama vipo kisheria na sheria zinaviruhusu kufanya siasa ndani ya sheria anashindwa! Amebaki anatapatapa na kuwatupia mzigo polisi na vyama vinavyokatazwa na polisi kufanya siasa eti vielewane na yeye akiwa msuluhishi.
 
CCM wanampa wakati mgumu sana Jaji Mutungi, jana Jumatatu Jaji Mutungi alionekana kwenye runinga ITV akijaribu kuelezea kuhusu mikutano atakayoifanya na jeshi la polisi kisha na vyama vya siasa, Jaji Mutungi alionekana kama ni mtu anayejilazimisha kuchukua hatua hizo kinyume na sheria huku akijua kuwa ni uvunjaji wa katiba...
Kinacho sikitisha eti alikua jaji.
 
Huenda anadhani yeye si kiongozi wa taasisi bali yupo mahakamani!

Ukitumika vibaya wanaokutumia wanakucheka vibaya mwisho wa siku.

RIP Paul Sozigwa
 
Jaji Mutungi anakwepa kwa makusudi kutimiza wajibu, halafu anataka jukumu lake lifanywe na polisi ambao hata yale yaliyopo ndani ya PGO zao wenyewe hawayajui!
 
Jaji Mutungi anajua nini kinatakiwa kufanyika ila anashindwa afanyeje, bosi anapokuambia rekebisha tafuta jinsi yoyote utavyoweza, alivyokuwa akieleza alikuwa ni mtu anayetafuta maneno ya kuunganisha japo hayaingii kichwani, kazi anaipenda, polisi hawezi kuwaambia wazisome na kuzitekeleza sheria za vyama na katiba ya nchi.
 
Ujinga ni mzigo unaoweza kuwekwa chini kwa mapumzi

Upumbavu ni mzigo hakuna anayeweza kuutua toka kichwa kichwani mwake
HICHI NDICHO KINACHOMTESA MUTUNGI

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Tunamlaumu Jaji Mutungi kwa jambo moja tu, kushindwa kuachia ngazi. Ukijiamini kuwa ni mwanasheria na utasimama na kiapo cha sheria (sijui kama wanaapa kwa sheria au kwa Rais) hautakubali kukiasi kiapo chako, utakuwa radhi kuachia madaraka kuliko kushinikizwa.
 
Back
Top Bottom