Jaji Mutungi mwambie Rais ukweli kuwa kauli yake ni kinyume na Sheria na Katiba ya JMT

Jaji Mutungi mwambie Rais ukweli kuwa kauli yake ni kinyume na Sheria na Katiba ya JMT

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Baada ya purukushani za mitandaoni wiki nzima kati ya wanaharakati, wanasiasa na Serikali kuhusiana malalamiko mbalimbali ya kisheria na kikatiba. Hili lilipelekea matamko, vitisho, kejeli na kashfa mbalimbali kutoka katika majukwaa mbalimbali na hata kufikia jana tulijionea kuwa Kada wa Chama cha Chadema mkoani Njombe kushikiliwa na jeshi la polisi kwa kauli zake mtandaoni.

Kiini cha hili suala kiko wazi, na labda inaonekana kuna Mtu au mamlaka fulani ndo inayopaswa kuangazia hili.
Nami pasi na kuchelea Namuasa MSAJILI WA VYAMA vya siasa Jaji Mutungi kujitokeza hadharani na kumwambia mama kuwa hana Mamlaka ya kikatiba kupiga marufuku shughuli za kisiasa hususan mikutano ya hadhara. Anapaswa kutoa muongozo wa kikatiba na kisheria na ikibidi kushauri Mamlaka nyingine kuhsiana na Taratibu na kanuni zinzoendesha shughuli za vyama vya siasa,

Jaji Mutungi akumbuke kuwa yeye ni mlezi wa vyama hivi, na pale haki zao zinapominywa Kisheria au kikatiba anapaswa kuingilia na kutoa Miongozo. Anapaswa kulikemea Jeshi la polisi pale linapozuia Mikutano hii bila sababu za Msingi, n.k

JAJI Mutungi mwambie Mama Ukweli Uwe Huru. Hizo kelele zote na chokochoko zinaanziaga hapo.

Hamsa za katiba mpya inazidi kuchochewa na viashiria vyakurudishana enzi za manyanyaso na uonevu.
 
Hivi hamnaga kazi nyingine za kufanya!?.. kukaa una Spin ishu moja zaidi ya wiki huoni ni matumizi mabaya ya ubongo!?, Huna hata kademu kakuweke bize au hunywi hata bia leo weekend inaanza ukapoze koo mahali!?.. mbona Siasa zinawafanya muwe WAPUMBAVU kiasi hiki!??
 
Mademu na ulevi vimekufanya uwe Mjinga hivi?

Mimi ni Kada na katibu wa uenezi wa Chauma. Umeona sasa?
 
Baada ya purukushani za mitandaoni wiki nzima kati ya wanaharakati, wanasiasa na Serikali kuhusiana malalamiko mbalimbali ya kisheria na kikatiba. Hili lilipelekea matamko, vitisho, kejeli na kashfa mbalimbali kutoka katika majukwaa mbalimbali na hata kufikia jana tulijionea kuwa Kada wa Chama cha Chadema mkoani Njombe kushikiliwa na jeshi la polisi kwa kauli zake mtandaoni.

Kiini cha hili suala kiko wazi, na labda inaonekana kuna Mtu au mamlaka fulani ndo inayopaswa kuangazia hili.
Nami pasi na kuchelea Namuasa MSAJILI WA VYAMA vya siasa Jaji Mutungi kujitokeza hadharani na kumwambia mama kuwa hana Mamlaka ya kikatiba kupiga marufuku shughuli za kisiasa hususan mikutano ya hadhara. Anapaswa kutoa muongozo wa kikatiba na kisheria na ikibidi kushauri Mamlaka nyingine kuhsiana na Taratibu na kanuni zinzoendesha shughuli za vyama vya siasa,

Jaji Mutungi akumbuke kuwa yeye ni mlezi wa vyama hivi, na pale haki zao zinapominywa Kisheria au kikatiba anapaswa kuingilia na kutoa Miongozo. Anapaswa kulikemea Jeshi la polisi pale linapozuia Mikutano hii bila sababu za Msingi, n.k

JAJI Mutungi mwambie Mama Ukweli Uwe Huru. Hizo kelele zote na chokochoko zinaanziaga hapo.

Nchi ipo kwenye corona, na mwenyekiti wa chadema tayar ameshapata chanjo. Sasa mikutano ya kazi gani? Kwamba watu wakusanyike na kuambukizana corona kwa faida ya nani? Inashangaza kuona viongozi wanao/waliokuwa wanawaasa watanzania kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa corona mpaka kufikia hatua ya kuitaka serikali iweke lockdown nchi nzima eti leo wanataka mikutano ya hadhara bila kuangalia madhara yatakayotokana na mikusanyiko hiyo.
 
Brother, you can't be serious for sure. Yaani unatarajia Jaji mtungi ndiyo amwambie kuwa kuzuia shughuli za kisiasa ni kinyume na katiba ya JMT na sheria zingine za Nchi.

Tatizo kubwa la Watanzania ni elimu na uelewa mdogo. Watanzania hatupo tayari kulinda katiba yetu na sheria zetu kwa hali na mali ili zisilivunjwe na viongozi wa Umma.

Nchi za wenzetu wanajua umhimu wa kulinda katiba yao ma ikitokea kiongozi ametenda au amekiuka masharti ya katiba au sheria fulani huwa wanafanya maandamano bila kujali chochote na huwa wanafanikiwa. Hii ni kwa sababu uelewa wao ni mkubwa sana na wanajua haki zao.

Huwa hawapendi kudhulumiwa haki zao kiboyaboya kwa sababu wanajitambua sana. Watanzania tumetawaliwa na uoga mkubwa sana, uelewa mdogo na elimu ndogo pia ni tatizo.

Watanzania badala ya kujitokeza na kudai haki zao unakuta wanaogopa kwa kuhofia kwamba akifa ni nani atalea familia yake. Anaona ni bora akimbie na asitetee haki yake ambayo ingesaidia kumkomboa katika umasikini wake ila anabariki haki yake kuvunjwa na viongozi ambao kwa asilimia 85% ndiyo chanzo cha umasikini wa Taifa hili.
 
kazi ya Msajili wa vyama ni nn? maana naona amekaa kimya sana akiachilia baadhi ya vyama vya upinzani vikitoa matamko yenye kuashiria uvunjifu wa amani na utulivu bila kukemewa au hata kuchukua hatua ya kukifuta chama hicho ambacho nia yake ni kuteteresha amani ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom