Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi ya juu kuulinda mkataba wa LUGUMI

Jaji Rwegasira: Nimeagizwa na ngazi ya juu kuulinda mkataba wa LUGUMI

Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.
"Jaji"!?
 
Ivi wakuu, kuna evidence yoyote inayo onyesha serekali iliwahi kuwahukumu au kuwafunga hawa watu wenye amjina kama linalo fanan na la prince (Mafisadi)?.
 
Lugumi ni kipimo cha tatu kigumu kwa Magu

  1. Cha kwanza ni Home Shopping Center (bado hatujajua nini kinaendelea kwani jamaa wanajipambanua kivingine)
  2. Ya pili ni sakala la Bandari (bado tunasubiri kama mtu yeyote wa "maana" ataumia)
  3. Sakata la tatu ni hili la Lugumi/Kitwanga/Mwema (tunaona watu wanabinuka-binuka tu)

Mengine mbwembwe...
 
Serikali ya tzania haijawahi shinda kesi zidi yake kwa mtuhumiwa yeyote.hvyo msijisumbue kwamba wanapigana na mafisadi wala nin na kama hamuamini subir kesi za wakina masamaki,wazee wastaafu wa tra muone kama hawatashinda na serikali kutakiwa kuwalipa.
 
Chonde chonde Magufuli kama unataka kuendelea na nafasi yako ya urais wa nchi hii, achana na mpango wako wa kuanzisha mahakama ya majizi kwani utaingia kwenye mgogoro na chama chako bure kwa kuwa majizi wote hutokea huko. Utakiua chama ama watakufukuza uanachama.
Unamshauri hivyo JPM wakati umeambiwa mamalaka za juu zimezuia mkataba kuwa public!
 
Tatizo mnaingiza uwongo mwingi na udaku kwenye suala hili mpaka linakosa hata maana nzima au watu wengine wenye fikra pana wanaanza kujiuliza na kuangalia kilichoko nyuma ya suala zima.

Ninaamini habari umeitoa hapa halafu ukaiongezea uwongo na udaku kwa faida ya ajenda zako;

Hivi huwa mnapata faida gani?

Hao ni 'fanatics' wala wasikupe shida kwani dunia nzima wapo na sifa yao kuu moja ni kuwa 'they are just clouded by self-justification.'
 
Safi kabisa katibu mkuu....kiukweli masuala ya jeshi hayafai kuanikwa .....ikumbukwe masuala ya jeshi si kama taasisi zingine za Mkonge....
 
Lugumi ni kipimo cha tatu kigumu kwa Magu

  1. Cha kwanza ni Home Shopping Center (bado hatujajua nini kinaendelea kwani jamaa wanajipambanua kivingine)
  2. Ya pili ni sakala la Bandari (bado tunasubiri kama mtu yeyote wa "maana" ataumia)
  3. Sakata la tatu ni hili la Lugumi/Kitwanga/Mwema (tunaona watu wanabinuka-binuka tu)

Mengine mbwembwe...
Pole sana Kama ni mmojawapo Wa wale wanaodhani Sasa amepatijana mkombozi, wapi watakaotolewa kafara Ila wengi watalindwa kwa nguvu zote ili kulinda heshima ya chama
 
kuna siku mtasema kununua kofia za ccm ni swala la kiusalama mbona zipo madukani izo mashine four ways hapo zipo za kumwaga tuu..
 
Mmmmh!!!
Utasikia Lugumi ashinda kesi sasa kuishitaki serikali
ni kweli mkuu, kama alivyoachiliwa huru Mhando wa Tanesco leo.na takukuru wanajifaragua ati watakata rufaa kuficha aibu.tusubiri madai ya mamilioni ya fidia. tutakoma!
 
Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.

Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.

Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.
hili move linaitwaje vile,THE BLACK NINJA,mtuhumiwa anachagua watu wa kumshughulikia balaa,tanzania nchi yangu umekonda kwa kunyonywa usiku na mchana na ndama wa kila aina
 
Hapo ndo mtajua pombe siyo chai!! Eti kutumbua majipu? Tumbua hilo hapo basi tukusikie, mbona unaishia kutumbu vichunusi nawe unajitapa unatumbua majipu? Ila na wewe mleta mada naomba nikutukane basi japo kidogo, mamamaeeeeee unaletaje habari bila chanzo?
 
Back
Top Bottom