MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Mkuu, mimi kwa sasa nimeanza kujiuliza sana kuhusu hili suala.Unafahamu mkuu, kuna watu hivi sasa wanahangaika sana mara huku mara kule.
"Jaji"!?Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.
Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.
Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.
ni kazi yao wala hapo amna suala la usalama, usipotoshe jamiiHuo ndio utaratibu issue za kiusalama sio kila mtu anapaswa kuziangalia na kujitafutia umaarufu kama hawa wajumbe wa PAC
Unamshauri hivyo JPM wakati umeambiwa mamalaka za juu zimezuia mkataba kuwa public!Chonde chonde Magufuli kama unataka kuendelea na nafasi yako ya urais wa nchi hii, achana na mpango wako wa kuanzisha mahakama ya majizi kwani utaingia kwenye mgogoro na chama chako bure kwa kuwa majizi wote hutokea huko. Utakiua chama ama watakufukuza uanachama.
Tatizo mnaingiza uwongo mwingi na udaku kwenye suala hili mpaka linakosa hata maana nzima au watu wengine wenye fikra pana wanaanza kujiuliza na kuangalia kilichoko nyuma ya suala zima.
Ninaamini habari umeitoa hapa halafu ukaiongezea uwongo na udaku kwa faida ya ajenda zako;
Hivi huwa mnapata faida gani?
Pole sana Kama ni mmojawapo Wa wale wanaodhani Sasa amepatijana mkombozi, wapi watakaotolewa kafara Ila wengi watalindwa kwa nguvu zote ili kulinda heshima ya chamaLugumi ni kipimo cha tatu kigumu kwa Magu
- Cha kwanza ni Home Shopping Center (bado hatujajua nini kinaendelea kwani jamaa wanajipambanua kivingine)
- Ya pili ni sakala la Bandari (bado tunasubiri kama mtu yeyote wa "maana" ataumia)
- Sakata la tatu ni hili la Lugumi/Kitwanga/Mwema (tunaona watu wanabinuka-binuka tu)
Mengine mbwembwe...
ni kweli mkuu, kama alivyoachiliwa huru Mhando wa Tanesco leo.na takukuru wanajifaragua ati watakata rufaa kuficha aibu.tusubiri madai ya mamilioni ya fidia. tutakoma!Mmmmh!!!
Utasikia Lugumi ashinda kesi sasa kuishitaki serikali
hili move linaitwaje vile,THE BLACK NINJA,mtuhumiwa anachagua watu wa kumshughulikia balaa,tanzania nchi yangu umekonda kwa kunyonywa usiku na mchana na ndama wa kila ainaKatibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani jaji Projest Rwegasira ametoa ya moyoni kuhusu mkataba iliyopewa Lugumi Enterprises Ltd kusambaza vifaa maalum vya kuchukua alama za vidole kwenye vituo vyote vya jeshi la polisi nchini mwaka 2011.
Ndugu Rwegasira amesema kuwa ameagizwa na mamlaka ya juu kuuzuia mkataba kati ya Lugumi Enterprises Ltd na jeshi la polisi kwa madai kuwa kuutoa hadharani kwa wasio husika nao ni kukiuka taratibu za jeshi hilo.
Aidha ndugu Rwegasira amesema kuwa watakaoruhusiwa kuuona mkataba huo ni kamati ya bunge yenye mamlaka na jeshi la polisi nchini ambayo ni ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na si vinginevyo.