Jaji Warioba: 4R za Rais Samia zinafanya kazi licha ya kuwapo changamoto chache hasa kisiasa

Jaji Warioba: 4R za Rais Samia zinafanya kazi licha ya kuwapo changamoto chache hasa kisiasa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema bado anayaona mafanikio ya falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya R nne (4R) anazozitumia katika utawala wake na kuifanyia nchi kuwa katika utulivu.

Aidha amesema falsafa ya maridhiano (Reconciliation), Mabadiliko (Reforms), Ustahimilivu (Resilience) na Kujenga upya (Rebuilding), inaendelea kufanya kazi licha ya kuwapo changamoto chache hasa kisiasa.

Warioba amesema hayo leo Oktoba 4,2024, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, na kwamba kwa sasa nchi imetulia kisiasa tofauti na miaka mitatu iliyopita.

Amesema changamoto za kisiasa ni kama kuna mapambano kwa serikai na wapinzania ambao hawawasilishi hoja ipasavyo, huku akishauri wanasiasa kukaa meza moja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Amani inajengwa na wananchi wenyewe na sio polisi, kwasababu hata tulipopata uhuru hatukutumia mtutu wa bunduki bali kwa amani. Polisi wanaposikia maandamano yametangazwa alafu wanasema wanalinda amani wajifakari kwa kuwa ulinzi wa nchi unatokana na wananchi wenyewe bila kujali taasisi moja,”amesema.

Soma: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini
 
Back
Top Bottom