Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, huhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa
Mchakato tulioumaliza sasa hivi (Uchaguzi wa Serikali za Mitaa) yametokea yale yale ya mwaka 2019/20 na chanzo chake ni wasimamizi wenyewe wa Uchaguzi, kama tukiendelea na utaratibu huu tunajenga mazingira yakuja kulea vurugu ambayo itahatarisha amani yetu.
Nimesikiliza maelezo ya Serikali lakini hayakutosha, haiwezekani kwamba wananchi waamini kwamba walioenguliwa walikosea tena kwa marefu, lakini wanaoenguliwa ni waupande mmoja, kwamba kuna vyama ambavyo wanachama wake wanajua wanafuata manasharti na kuna vyama hawafuati, tunazungumzia watanzania wakawaida.
Haiwezekani na wala tusijedanganyika kwamba kuna maelezo, sababu kuu ya watu kuenguliwa ni kwamba hawakufuata masharti, tutakuwa tunajidanganya kama tukiamini hivyo. Haiwezekani kwamba inatoka kura bandia.
Jaji Warioba amesema matatizo ya uchaguzi wa mwaka 2000 yaliyotokea Zanzibar na kusababisha maandamano na vurugu kubwa na kusababisha vifo na majeruhi, anaona hayo yakijirudia.
Ilikuwa hali ngumu kushawishi CUF na CCM kufanya mazungumzo na kuwa kitu kimoja. Tusipopata njia ya kumaliza matatizo ya hayo tutafikia hali ya kama Zanzibar ya mwaka 2000, Tuna wasiwasi mkubwa haya matatizo sio ya CCM bali Serikali ambayo imejitenga na CCM, si mmeona matamko ya katibu mkuu? Msimamo wa CCM sio kama ambavyo wamefanya wasimamizi wa uchaguzi.
Nazungumza kutokana na uzoefu, tuliporudisha mfumo wa vyama vingi uchaguzi wa kwanza ulifanyika mwaka 1995, kwenye uchaguzi huo yalitokea matatizo makubwa sana Zanzibar, yakaleta mgawanyiko Zanziba, kukawa na uadui, kukawa na chuki baadhi yetu tukaona hilo, tukaona tujaribu kutoa ushauri kwamba viongozi wasiache ile hali iendelee.
Nikaanza kujaribu kushawishi viongozi, hali hii ni mbaya Zanzibar, watu wanachukiana hata ndugu wanasusiana, haikiuwa kazi rahisi, Jumuiya ya Madola (commonwealth) walikuja wakajaribu ikashindikana wakaondoka, baadae mwaka 1998 Jumuiya ya Madola wakaombwa kurudi kujaribu kusaidia.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025, Jaji Warioba ameonya Jeshi la Polisi:
Tangu Uhuru watu wa Kongo, Burundi, Rwanda wamekuwa na machafuko, wananchi wa huko walikuwa wakikimbilia huku na wengine wakitaka kuendeleza harakati zao kutoka ndani ya nchi yetu, jeshi letu lilidhibiti mikoa mbalimbali hasa ile ya mipakani kuanzia Katavi, Kigoma, Kagera kukawa salama kabisa.
Mnajua chokochoko iliyotokea Uganda, na mnajua kazi iliyofanywa na jeshi, tulipoteza vijana wengi sana, wale wameapa kuifia nchi na waliifia nchi, tusije tukawaingiza kwenye haya matatizo ya kisiasa, wananchi wakaanza kuwaona nao wanapendelea upande mmoja. Mimi ninaomba kabisa jeshi la ulinzi lisije likaingizwa kwenye mambo ya siasa, siyo kazi yake, kazi yake ni kulinda usalama wa nchi.
Katika miaka michache iliyopita tumeliingiza Jeshi la Polisi kwenye siasa, linatoa matamko ya kisiasa na hii italeta mgawanyiko.
Wananchi watagawanyika. Kuna wale watakaoona, Jeshi la Polisi ni adui, tusifike huko. Tuliache Jeshi la Polisi lifanye kazi zake za kawaida.
Amesema kwa bahati nzuri Rais (Samia Suluhu Hassan) alipoingia madarakani alisikia malalamiko ya wananchi kuhusu suala hilo na kuunda Tume ya Haki Jinai.
Tume ikaleta mapendekezo mazuri na ikapendekeza, Jeshi la Polisi liachwe lifanye kazi zake, lakini sasa hivi tumeliingiza Jeshi la Polisi kwenye siasa, lakini ujue polisi wale ni raia wa kawaida, ikifika kwenye mambo ya siasa wana mawazo yao, wakienda kupiga kura kila mmoja ana mapenzi yake, tukianza kuwaliza mle mle watagawanyika.
Chombo kikubwa kama polisi kugawanyika kuna hatari