PreGE2025 Jaji Warioba ajitosa kusaka suluhu kati ya Tume ya Uchaguzi na CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mwanaccm yuko radhi akeshe usiku mzima ila sio kukubali tume huru ya uchaguzi.

Hicho kikaragosi cha CCM kinachoitwa tume huru kwa sasa ni tume iliyo uhuru kwa CCM.
 
Kwa ninavyojua kwa hila za CCM anamaisha mafupi sana Warioba
 
Mzee anaelewa vizuri sana ila ukiangalia anajitahidi kusimama katikati ili apate imani kwa pande zote mbili,hawezi kuingia mzimamzima-anajua wakishakaa lazima yote yataibuka-Negotiator lazima aaminike na pande zote ndio atafanikiwa.
 
KWA NINI CCM WABISHI KUNA SHIDA MAHALA
Hakuna "SHIDA" mahali pengine popote, SHIDA ni CCM yenyewe. Wanacho kazia shingo ni kile kile walichozoea kufanya katika chaguzi zote za hivi karibuni.
Wanafanya kila linalo wezekana kulazimisha ushindi kwa njia zisizo kuwa halali. Hili ndilo litakalosababisha uvunjifu wa amani; kunyima HAKI ya raia kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze.
 
Na zaidi ya yote, ukorofi wa CCM unazidi kuwa bayana kwa wananchi wengi. Hapa ndipo palipo na hatari kubwa juu ya hiyo hadaa ya "AMANI", ambayo sasa hawachoki kuiweka mbele kama kinga yao kuwahadaa wananchi.
Wananchi sasa watajuwa ni nani anaye hatarisha amani ya nchi hii. Siyo CHADEMA, bali CCM wenyewe.
 
WARIOBA ni mzee pekee mwenye akili ccm kati ya wanachana m12
 
Nilivyo muelewa mimi, hayo mapendekezo ya kubadilisha "KANUNI" ni rahisi kufanyika sasa hivi kutokana na ufinyu wa muda hadi uchaguzi.
Kanuni zinaweza kurekebishwa haraka kuliko kubadili sheria husika zinazohusu chaguzi.
Hii inaweza kuwa "nusu shari" badala ya "shari nzima" itakayowezesha angalau kuwa na kiasi kikubwa cha uchaguzi HURU. Ametoa mfano wa "uenguzi wa wagombea toka vyama vya upinzani". Ni rahisi kutengeneza kanuni inayoelekeza ababu za kuenguliwa na kuwa wazi zaidi kuliko ilivyo sasa.

Kanuni zote zinazohusika na uchaguzi zikirekebishwa na kuwa wazi kabisa sasa hivi na kueleweka vizuri; hata wapinzani watakuwa na sababu ya kuzishikia bango waziwazi, wanapoona HAKI zao zinaporwa kinyemera.
Kama polisi ni sehemu ya vurugu wakati wa uchaguzi, nao watungiwe kanuni zinazo wabana kufanya hivyo. Wasizuie mikutano ya wapinzani kwa vile tu wameota kwamba kutakuwepo na vurugu kwenye mikutano hiyo.
 
Watu nyie ni Kwanini mnashindwa kutambua mtego wa CCM na serikali yao wanaojaribu kuitega CHADEMA ili itoke kwenye msimamo wake...?

Ishara moja iliyojitokeza wazi mara baada ya hicho kinachoitwa kanuni za maadili ya uchaguzi kusainiwa na puppets wao huko Dodoma, wa kwanza kuwasha moto kijinga tu na pasipokuwa na ufahamu mzuri wa sheria na katiba ni Mkurugenzi wa uchaguzi, kada wa CCM Kailima kuropoka kuwa CHADEMA kwa kutosaini huo ujinga, eti wamejiondoa kushiriki uchaguzi wowote kwa miaka mitano...!

Baada ya kauli hiyo ya "mbwa wao mkuu toka Tume", chawa wa Lumumba kama mazoba vile, wakaibuka na kuishikia bango hiyo kauli na kuanza kuishambulia CHADEMA wakidhani watatuliza moto wa No Reforms No Election....

By the way;

1. Hamuwezi hata kufikiri ni kwanini katikati ya kasi ya kampeni za NO REFORMS NO ELECTION za CHADEMA hawa wanaojiita "INEC" wanaandaa sherehe na kuvikusanya vyama vya siasa vya mfukoni huko Dodoma ili eti kusaini ujinga unaoitwa "kanuni za maadili ya uchaguzi mkuu 2025" wakati huohuo wao wenyewe hao INEC wakiwa hawana maadili (zero morals)?

2. Hamuwezi hata kufikiri ni kwanini wanamkamata Tundu Lissu (Mwenyekiti wa CHADEMA) halafu ghafla huko wavikusanya vyama vya siasa uchwara, wanawalipa viongozi wao posho nono nono kama hongo na kama chambo ya kuwalainisha wasaini huo ujinga...?

3. Na hebu fikrini, kwamba, kama kweli haya yametoka kwa Jaji Joseph Warioba, Je ina maana huyu mzee hajui madai ya CHADEMA na Watanzania ni nini..?

#Kwa akili za Joseph Warioba anadhani shida na madai ya CHADEMA ni kanuni za uchaguzi au ni ubovu wa mfumo mzima kabisa wa uchaguzi...?

#Na kushauriana huku kutawezekana vipi iwapo mwenyekiti wetu Tundu Lissu yuko gerezani kwa uhuni tu wa watawala...?

#Kama wanataka mashauriano, kwanza wamwachie Mwenyekiti wetu haraka na bila masharti yoyote maana hakuna sababu yoyote ya kumuweka gerezani. Wanajua fika wanamuonea tu, wananchi wanajua kuwa anaonewa na dunia inajua kuwa huo ni uonevu dhidi ya HAKI...!!

#NO REFORMS NO ELECTION
#FreeTunduLissu now
 
Kwamba Chadema ni katoto kalikojifanya kuzira kula, baada ya njaa kukazidia kakaenda kwa babu kulialia! Ahahahahaha!!
 

..tatizo liko kwenye muundo wa Tume, na mnyororo mzima wa watendaji wanaosimamia uchaguzi.
 
Lissu mtu wao na ana hoja za Msingi sana kila mwenye nia Njema na Nchi au anaeitakia mama nchi huwezi mpuuza Lissu hoja zake hii nchi yetu sote ukiwa uwanja hautakiwi kulalia upande
 
Kwa nini kwenye TUME ya Uchaguzi kusiwepo na Wakala mmoja mmoja kwenye Tume kule Ngazi ya Juu
 
Ndugu Kalamu, kanuni tu hazitoshi kuufanya uchaguzi huu na chaguzi zijazo kukidhi sifa ya kuwa chaguzi za haki, huru, wazi na za kuaminika...

Tunachotaka na kinachowezekana kwa sasa kama ni lazima sana uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu 2025 ufanyike ni;

1. Kufanyike minimal reforms ya katiba kwenye ibara inayohusu "Tume ya uchaguzi"; upatikanaji wa wajumbe wake, majukumu yao na uhuru na usalama wa nafasi zao ktk utekelezaji wa majukumu yao...

2. Kufanyiwa marekebisho sheria zote zinazosimamia chaguzi zetu kwa kuwaondoa watumishi wa serikali (wakurugenzi wa h/m, miji, manispaa, majiji, walimu, nk kuwa wasimamizi wa uchaguzi. Tume iwe na wafanyakazi wake wanaowajibika moja kwa moja kwa tume...

#Haya yana ugumu gani kufanyiwa kazi sasa? It's obvious inawezekana ony kama utashi wa kisiasa upo na tunaipenda nchi na wananchi wenzetu...

#Na kama muda wa maandalizi ya uchaguzi kwa serikali na washiriki wa uchaguzi ikiwemo vyama na wagombea ni mfupi, tunaweza kuusukuma/kuusogeza uchaguzi mbele kidogo hata kwa miezi mitatu au mitano ili kuruhusu reforms hizi kufanyika..

What's wrong with that aisee...???
 
CCM na viongozi wake ni washenzi sana na wanadhani watanzania hawana Akili TIMAMU kama wao wasivyo na Akili,NAANDIKA KWA HERUFI KUBWA KWAMBA CCM KWA WAKATI HUU TULIONAO CCM HAINA WATU TENA NA WALA CCM ISIJIDANGANYE KAMA ILIVYOJIDANGANYA HUKO NYUMA,TUSIPOKUBALI KWAMBA WATU WAMEICHOKA CCM TWAJIDANGANYA MCHANA KWEUPE,WATANZANIA WAMECHOSHWA SANA NA CCM HII.
 
Sheria ni jambo moja ila kama mnawatendaji hovyo wanaweza kufanya lolote na bado sheria hizo hizo zisifanye kazi.

Ila yaweza kuwa na sheria mbovu mkawa na watendaji wenye hofu ya Mungu wakatenda haki kwa kila mtu.
Integrity, honest kuwa responsible na accountable kwa sheria za asili inatosha kabisa.
 
Wamewaondoa rasmi kwa kuwa waliwatungia kanuni za kuwaondoa
Wamewaondoa rasmi kwa kuwa walipanga na kuwatungia kanuni za kufanya hivyo. Hapo 2019, 2020 na 2024 walikuwa wanaondoa kihuni kwenye chaguzi, wakaona isiwe kesi wawawekee na kanuni/sheria kabisa.
 
Mzee anaelewa vizuri sana ila ukiangalia anajitahidi kusimama katikati ili apate imani kwa pande zote mbili,hawezi kuingia mzimamzima-anajua wakishakaa lazima yote yataibuka-Negotiator lazima aaminike na pande zote ndio atafanikiwa.
Kwa TAL warioba ajipange hasa. Hasije leta maneno yasiyo na reforms. Bila kuongelea reforms warioba hasipoteze muda kuongea na TAL na Heche na chadema kwa ujumla. Hawa ccm wanafanya watu waishi kama mashetani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…