gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 825
- 1,519
DAR ES SALAAM, TANZANIA— Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba, ameeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu uwezekano wa Tanzania kupata Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2029/2030.
Akizungumza katika mkutano uliowashirikisha wanasheria na wataalamu wa masuala ya kikatiba jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alibainisha kuwa mfumo wa sasa wa maandalizi na utaratibu uliopendekezwa una mlolongo mrefu mno wa kisheria na kijamii ambao hauwezi kukamilika kabla ya uchaguzi ujao.
Aidha, Jaji Warioba alitumia fursa hiyo kutoa ushuhuda wake kuhusu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM na Makamu wa Rais, Dr. Emmanuel Nchimbi, akisisitiza kuwa kiongozi huyo hana tabia ya "uchawa" na kueleza wasiwasi wake baada ya kushindwa kumpata kwenye simu kufuatia taarifa za kujiuzulu kwake.
"Sioni Uwezekano wa Katiba Mpya kabla ya 2030"
Jaji Warioba alieleza kuwa hatua zilizowekwa na Tume ya Chande—ikimemo Kamati ya Majaji kuchunguza vurugu za uchaguzi (wiki 5+), Kamati ya Wataalamu wa Kisheria, ukusanyaji wa maoni ya wananchi kwa angalau miezi sita, Tume ya Maridhiano, Kura ya Maoni na kipindi cha mpito cha kutunga sheria mpya—ziatachukua miaka kadhaa.
"Kama hatutapata Katiba Mpya tukaingia kwenye uchaguzi ujao kwa utaratibu huu na Tume hii, tutapata madhara makubwa zaidi. Wananchi bado wanaomboleza waliowapoteza, lakini viongozi wanaona ni jambo la kawaida tu litakalosaulika," alisema Jaji Warioba.
Ukweli Kuhusu Taarifa za Dr. Nchimbi
Kuhusu mfadhaiko wa kisiasa unaoendelea, Jaji Warioba alieleza uhusiano wake wa muda mrefu na Dr. Emmanuel Nchimbi tangu mwaka 1998. Alisema baada ya kuona taarifa za barua ya kujiuzulu kwa Nchimbi zikitrendi mitandaoni, alimpigia simu moja kwa moja.
"Alipopokea nilimuuliza kama ni kweli ameandika barua ya kujiuzulu, na aliniambia 'Ndio Mzee ni kweli'. Lakini baada ya hapo, nilijaribu kumpigia tena siku iliyofuata na jioni yake wakati wa press conference haikupokelewa na jumbe hazikujibiwa. Baadaye nikaambiwa amenyang'anywa simu zake na yuko kizuizini. Hili linanishangaza, hata kama chama kinachukua hatua za nidhamu, mtu anapaswa kubaki huru," alisisitiza.
Rushwa Kuchukua Nafasi ya Demokrasia
Akizungumzia ahadi za CCM za "Ntasema kweli daima fitina kwangu mwiko", Warioba alisema kwa sasa nidhamu hiyo imepotea na mtu akisema ukweli anaonekana ameleta fitina. Pia alikemea kushamiri kwa rushwa akisema imekuwa kigezo kikuu cha kupata uongozi badala ya uwezo na maadili.
Alitimisha kwa kuwasihi viongozi wote nchini kuweka mbele maslahi ya taifa kwa kuonyesha utashi wa kisiasa ili kufanya mabadiliko ya dharura ya kikatiba yatakayohakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa haki, amani na usawa.