INTRODUCTION
Nimefuatilia kuhusu kuandika katiba Mpya ambalo ni takwa la watanzania wengi, nikajiridhisha kwamba, kama CCM ikiwa madarakani katiba Mpya ni haiwezekani.
MAIN BODY
Kwa sababu katika mataifa yote yalifanikiwa kuandika katiba Mpya, mambo mawili au matatu yametokea kwanza ndo Katiba mpya ikatokea!
Mosi; Msuguano wa kimawazo! Serikali ikiona suala la katiba nompya kutokuwa kipaumbele na wananchi wakiona kama kipaumbele baada ya kuridhika kwamba katiba imepoka mamlaka ya wanachi na kuyarundika katika mhimili mmoja unaoitwa serikali! Tanzania kwa Sasa iko katika hatua hii. Freeman Aikaeli Mbowe, anajaribu kusuguana na serikali kifikra! Na serikali ambayo imeshaonja utamu wa Katiba iliyopo inakuwa haionekani kujifunza wala kuchukua mawazo mbadala kuelekea katiba mpya, bali kutumia kila njama kuaminisha jamii kuwa suala hilo halina msingi kwa Sasa, na kufanya hivo ni chokochoko! Tunatakiwa kuvuka hapa twende hatua ya pili.
Pili, Kuvurugana kinguvu! Mbwai mbwai (sitamani itokee), lakini ni hatua! Kote ambako katiba Mpya imeandikwa kumetokea timbwili la Asha Ngedere kwanza ndo Katiba ikaandikwa! Fuatilia Kenya, na hata Zanzibar! Kimeumana kwanza ndo akili ya Viongozi ikakaa sawa! Siamini kama ni njia nzuri, lakini kwa uzoefu ipo katika hatua za kuitafuta na kuipata katiba Mpya! Kuna wakati mwalimu wangu wa history aliuliza why armed struggle, jibu lilikuwa rahisi tu, Failure of peaceful means! If you fail to provide the required demands of the society peacefully, they can try it through bloodshed! Tuwe makini! Kisiwa cha uvumilivu kina mipaka, kina ukomo!
Tatu, Kuondolewa chama Tawala Madarakani. Ni ngumu sana kuandika katiba Mpya Kama chama dola , ambacho kinanufaika na katiba iliyopo kikiwa Madarakani. Wakifanya hivo, ujue katiba hiyo itakuwa imepakwa rangi tu. Itakuwa ni Calorite kwenye ngozi ya mtu mweusi! Hivyo, jukumu letu kubwa ni kupigania kwanza kukiondosha chama Tawala. Maana hata katiba iliyopendekezwa si ile ya Warioba. Imechakachuliwa! Imepakwa rangi! Hivyo jambo kubwa ni box la kura, ambalo nalo halina haki ndani yake, kutokana na ukweli kwamba katiba iliyopo haitoi nafasi kwa vyama mbadala kushinda , hata kama wananachi wataamua tofauti!
HITIMISHO
Namba moja ni uchochezi na chokochoko na ugaidi. Namba mbili, kisiwa cha uvumilivu kilishajengewa hofu tangu enzi za Mwl, na kufundishwa kumuachia Mungu. Namba tatu, Mwamzi ni yule Mtoto wa chama dola! Haiwezi kumwangusha Baba, wala mama! Kwa hiyo, hata mimi sijui[emoji3]!
USHAURI!
Free Mbowe! Aendelee kutoa elimu, ili isaidie upatikanaji wa Katiba mpya kwa njia ya kwanza!
Ahsante