Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wanabodi, kwa kauli hii ya Jaji Warioba ndio kusema kwamba CCM wanaanza kukubali mmoja mmoja kwamba walipora uchaguzi au kuna namna hatujamuelewa mzee wetu?
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati anaongea na wanahabari hivi karibuni amedokeza na kukubali kuwa chaguzi ndogo za serikali za mitaa za mwaka 2020 pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulikuwa na dosari kubwa.
Soma pia: Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
Jaji Warioba alidokeza kuwa ni kawaida kwa uchaguzi wowote duniani kuwa na kasoro lakini kwa chaguzi za mwaka 2019 na 2020 dosari zake zilikuwa ni kubwa kupita kiasi na ziliwafanya washtuke.
"Ni kweli kwamba kila uchaguzi una dosari. Hakuna uchaguzi mahali popote duniani ambao hauna dosari. Lakini zinakuwa ni dosari za kawaida. Zinakuwa ni dosari ndogo ndogo zinashughulikiwa. Kwenye chaguzi unaofuata unakuwa ni mzuri zaidi."
Jaji Warioba aliongeza kwa kusema:
"Uchaguzi unaokuja tunauzungumza sana kwa sababu ya matukio ya 2019 na 2020. Dosari za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2019 na uchaguzi wa mwaka 2020 zilikuwa ni kubwa na zilifanya tushtuke."
Source: Jambo TV