PostGE2025 Jaji Warioba: Kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya vyombo vya usalama

PostGE2025 Jaji Warioba: Kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya vyombo vya usalama

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Akizungumza na Jamhuri TV Jaji Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba ameeleza kuwa alionya jeshi kuhusishwa na siasa na sasa matokeo yake yanaonekana ni kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya vyombo vya usalama.

"Nikasema tukihusisha vyombo vya ulinzi na usalama katika siasa tutapata matatizo na specifically nikasema jeshi la ulinzi lisije likahusishwa kabisa katika siasa.

Sasa tunaona matokeo yake ya vyombo hivi kuhusisshwa na siasa lakini kubwa zaidi kwa vyombo vyetu kuhusishwa kwa siasa vimegawanyika" - Jaji Warioba


 

There's a reason the government must separate military and the police, because one fights the enemies of the state, the other serves and protects the people. When the military becomes both, then the enemies of the state tend to become the people...☹️​

 
Na vikigawanyika itazalisha vikundi vya uasi na hatimaye CCM kufa kabisa.bora tufike huko ili watekaji wa Sasa nao waonje machungu ya vurugu.
 
Yule roporopo anaewaza nyama choma akifika Dodoma, badala ya kuwasaidia wananchi; sio muda mrefu atakuja na majibu ya pumba.
 
Na muasisi wa huu mgawanyiko ni Samia kwani alianza miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu kuyaandaa majeshi kwa ajili ya uchaguzi, kwa vile walijua kuwa wataiba kura na wnanchi watapinga dhuluma hiyo, kama kweli uchaguzi ungekuwa huru na wa haki hakuna hata mtu mmoja angeuwawa, Samia hana pa kujificha ushahidi upo kuwa ni yeye alikuwa anahamasisha majeshi yapambane na raia ambao watapinga udhalimu wake. Samia hana pa kutokea katika sakata la maelfu ya watanganyika waliouwawa na polisi wake kwa amri yake.
 
Na vikigawanyika itazalisha vikundi vya uasi na hatimaye CCM kufa kabisa.bora tufike huko ili watekaji wa Sasa nao waonje machungu ya vurugu.
Ni rahisi sana, tukiachana na huko kugawanyika. Wananchi wanapoona wazi kwamba sanduku la kura halina nguvu, kama tulivyojionea October ni hatari sana!

Leo hii hata mtu mjinga kabisa anaelewa kura yake haina maamuzi, ni hatari. Wakishauriwa, wanakimbilia kusema kuna watu wanatamani madini yetu. Rasilimali zetu zinatolewa macho miaka na miaka na itaendelea kuwa hivyo, wajibu wa viongozi ni kutenda haki kwa kufuata utawala wa sheria.
​
 
Back
Top Bottom