Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Jaji Warioba akihojiwa na Mwananchi Digital Aprili 7, 2024. amesema kuwa Mawaziri wasitokane na wabunge,
"Bunge liwe ni bunge, serikali isiingiliane na bunge, na vizuri mawaziri wasiwe kwenye bunge, mbunge asiwe waziri. Wakati tulipopata uhuru na hasa tulipobadili katiba tukawa Jamhuri, Rais alipewa madaraka mengi sana, Rais wakati ule alikuwa na madaraka makubwa kwanza kulikuwa na sheria ambazo zinampa madaraka ya kuwatia watu kizuizini bila kupitia utaratibu wa Mahakama, alikuwa na uwezo wa kuwahamisha watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ikatungwa sheria ambayo ilimpa madaraka hayo ya kuwatia watu kizuizini"
"Kwa upande wa uteuzi, Rais mwenyewe alisema kwamba anateua watu wengi mno ambao hawafahamu wala hawasimamii nidhamu yao haisimamii, akaona kwa utaratibu ule kulikuwa na hatari ya kuteua watu ambao hawana sifa au uwezo, zikawa zinaingia hata dalili za rushwa kwamba kwa kuwa ni Rais ndiye anayeteua na kuletewa mapendekezo na watu wengi inawezekana mtu akaenda akamhonga kiongozi fulani ili apigiwe debe ateuliwe ama mtu ana jamaa yake anaona amsaidie anakwenda kumpigia debe akasema hapana"