Watanzania wameonesha kutaka Tanzania mpya kupitia maoni yao ya katiba. CCM wakafuta na kutupilia mbali kabisa matakwa ya watanzania. CCM hawataki Mabadiliko wala mageuzi yatokanayo na wananchi.
Naombeni ninyi mliokuwa wajumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya al-maarufu kama Tume ya Warioba mtusaidie watanzania ambao tumetanzika hapa. Kwa mujibu wa maelezo yenu ile Rasimu ya Katiba Mpya iliundwa na kusukwa kutokana na maoni ya watanzania. Kwa rasimu ile Tanzania ingezaliwa upya.
Bahati nzuri, sijui mbaya CCM wakiwa wengi bungeni wakasema rasimu ile imetokana na maoni ya Warioba na si ya wananchi. Jaji Warioba,hata ukakunjwa shati, ukitetea kuwa rasimu ile ilitokana na maoni ya wananchi.
Leo hii,unaposimama majukwaani wewe na ndugu Polepole kwamba CCM ni wazuri mno wakati hata mwaka haujaisha tangu wakupinge wewe na tume yako kwamba mlitaka kuleta mabadiliko na mageuzi kupitia katiba mpya. Wakikutuhumu kuwa wewe ni MSALITI. Je! Sisi tulioamini kwamba hukuwa msaliti ila ulisimamia maoni yetu watanzania tuanze kukuita MSALITI wa umma?
Je! CCM kwa umoja wao waliposema wewe jaji Warioba na tume yako ni wazushi, sasa tuamini kwamba wewe na tume yako mlikuwa wazushi?
Watanzania kwa upande mwingine, tunafahamu kwamba mabadiliko au mageuzi ndani ya CCM ni ndoto ya mchana kweupe. Watanzania tunaamini kwa katiba mpya itakayotokana na maoni ya wananchi tutaweza kuibadili na kuigeuza nchi yetu ikawa mahala pazuri na salama kwa kuwa itakuwa imejengwa misingi ya HAKI kwa wote. Haki ikitamalaki amani inafanya makao mahali hapo.
Je! Jaji Warioba na Ndugu Polepole tutakuwa tunakosea tukisema ninyi ni WASALITI wa UMMA kwa kujiunga na kundi la wachache waliopinga rasimu ya katiba ya wananchi ambayo wananchi waliamini na wangali wanaamini kwamba ingeleta mabadiliko na mageuzi makubwa kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni katika taifa lao?
Leo hii, kweli...Jaji Warioba, ndugu Butiku na ndugu Polepole mnadiriki kushika vipaza sauti majukwaani mkisema CCM ni wazuri?
Kweli! Jaji Warioba kweli! Wewe uliyetamka pale Pearl Hotel Ubungo ukisema "...CCM ziko mbili: CCM Maslahi na CCM Imani. Hebu tuambie sasa, CCM unayoitetea ni ipi? Ni CCM Maslahi (ile ya Tegeta escrow account, ile ya kivuko feki cha MV Dar es Salaam, ile ya ufisadi wa Tshs 230bn kwenye miradi ya ujenzi wa barabara, ile ya posho za vikao vya bodi ya bandari kutumia TShs 9 bilioni kwenye kikao cha siku tisa ama CCM ipi unayoisimamia na kuitetea majukwaani wewe)
Wewe na wenzio bila shaka ni wakristo hebu someni Biblia Takatifu, Mithali 24: 24 -25