Jaji Warioba na Polepole tafadhali mtujibu!

Jaji Warioba na Polepole tafadhali mtujibu!

1954tanu

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
1,038
Reaction score
487
Watanzania wameonesha kutaka Tanzania mpya kupitia maoni yao ya katiba. CCM wakafuta na kutupilia mbali kabisa matakwa ya watanzania. CCM hawataki Mabadiliko wala mageuzi yatokanayo na wananchi.

Naombeni ninyi mliokuwa wajumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya al-maarufu kama Tume ya Warioba mtusaidie watanzania ambao tumetanzika hapa. Kwa mujibu wa maelezo yenu ile Rasimu ya Katiba Mpya iliundwa na kusukwa kutokana na maoni ya watanzania. Kwa rasimu ile Tanzania ingezaliwa upya.

Bahati nzuri, sijui mbaya CCM wakiwa wengi bungeni wakasema rasimu ile imetokana na maoni ya Warioba na si ya wananchi. Jaji Warioba,hata ukakunjwa shati, ukitetea kuwa rasimu ile ilitokana na maoni ya wananchi.

Leo hii,unaposimama majukwaani wewe na ndugu Polepole kwamba CCM ni wazuri mno wakati hata mwaka haujaisha tangu wakupinge wewe na tume yako kwamba mlitaka kuleta mabadiliko na mageuzi kupitia katiba mpya. Wakikutuhumu kuwa wewe ni MSALITI. Je! Sisi tulioamini kwamba hukuwa msaliti ila ulisimamia maoni yetu watanzania tuanze kukuita MSALITI wa umma?

Je! CCM kwa umoja wao waliposema wewe jaji Warioba na tume yako ni wazushi, sasa tuamini kwamba wewe na tume yako mlikuwa wazushi?

Watanzania kwa upande mwingine, tunafahamu kwamba mabadiliko au mageuzi ndani ya CCM ni ndoto ya mchana kweupe. Watanzania tunaamini kwa katiba mpya itakayotokana na maoni ya wananchi tutaweza kuibadili na kuigeuza nchi yetu ikawa mahala pazuri na salama kwa kuwa itakuwa imejengwa misingi ya HAKI kwa wote. Haki ikitamalaki amani inafanya makao mahali hapo.

Je! Jaji Warioba na Ndugu Polepole tutakuwa tunakosea tukisema ninyi ni WASALITI wa UMMA kwa kujiunga na kundi la wachache waliopinga rasimu ya katiba ya wananchi ambayo wananchi waliamini na wangali wanaamini kwamba ingeleta mabadiliko na mageuzi makubwa kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni katika taifa lao?

Leo hii, kweli...Jaji Warioba, ndugu Butiku na ndugu Polepole mnadiriki kushika vipaza sauti majukwaani mkisema CCM ni wazuri?

Kweli! Jaji Warioba kweli! Wewe uliyetamka pale Pearl Hotel Ubungo ukisema "...CCM ziko mbili: CCM Maslahi na CCM Imani. Hebu tuambie sasa, CCM unayoitetea ni ipi? Ni CCM Maslahi (ile ya Tegeta escrow account, ile ya kivuko feki cha MV Dar es Salaam, ile ya ufisadi wa Tshs 230bn kwenye miradi ya ujenzi wa barabara, ile ya posho za vikao vya bodi ya bandari kutumia TShs 9 bilioni kwenye kikao cha siku tisa ama CCM ipi unayoisimamia na kuitetea majukwaani wewe)

Wewe na wenzio bila shaka ni wakristo hebu someni Biblia Takatifu, Mithali 24: 24 -25
 
Mithali 24 - 24-25

24 Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia.

25 Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia.
 
Last edited by a moderator:
Hakika njaa ni mbaya sana. Bunge la kujadili Rasimu ya katiba kupitia Mh. Sitta Na Mama Samia huku wakiungwa mkono Na wajumbe Wa bunge hilo, waliiponda rasimu hiyo Na kumwita Warioba kazeeka Na mpumbavu kwa kuleta mapendekezo mabovu. Kama haitoshi Ofisi zao Na magari vilizuiliwa Na tovuti ya tume kufungwa, hakika ilikuwa in Dharau kubwa.

Kitu kinachonishangaza ni Jinsi Mzee Warioba Na Polepole wanavyoipigia debe rasimu ya CCM, rasimu iliyowaponda wao. Nimeamini kweli NJAA ni kitu kibaya sana. Warioba Kabamizwa MAKOFI Na Bw.MAKONDA Na kumpongeza Makonda kwa Kazi nzuri, Mh.Kikwete Kampa UKUU WA WILAYA.
 
Huyo warioba na pole pole njaaa ilikuwa ina wasumbua tu hakuna lolote
 
Kama vile Mbowe, Lissu, Mnyika, Sugu na Lema walivyogeukia kinyesi chao kwenye suala la kusafisha mafisadi? Njaa mbaya sana aisee
 
hata nilianza kupata shaka na warioba alipoanza kuchana kwa kwaruzo.nywele zinarud nyuma nikasema TUMASHAMPOTEZA MZEE

huyo polepole ni sawa na mjusi akiingia ndan
 
Tony ufisadi in MTU Na pia in taasisi yake .Hao mnaowaita Leo mafisadi kabla hawajatoka CCM mlikuwa mnawaita nani? CCM in taasisi kubwa yenye sifa kubwa nchini Na nje ya nchi kwa Ufisadi je aliyomo ndani ya taasisi hiyo in msafi kwa uelewa wako mdogo? Kwa taarifa yako taasisi CCM in fisadi waliomo in mafisadi
 
Hakika njaa ni mbaya sana. Bunge la kujadili Rasimu ya katiba kupitia Mh. Sitta Na Mama Samia huku wakiungwa mkono Na wajumbe Wa bunge hilo, waliiponda rasimu hiyo Na kumwita Warioba kazeeka Na mpumbavu kwa kuleta mapendekezo mabovu. Kama haitoshi Ofisi zao Na magari vilizuiliwa Na tovuti ya tume kufungwa, hakika ilikuwa in Dharau kubwa.

Kitu kinachonishangaza ni Jinsi Mzee Warioba Na Polepole wanavyoipigia debe rasimu ya CCM, rasimu iliyowaponda wao. Nimeamini kweli NJAA ni kitu kibaya sana. Warioba Kabamizwa MAKOFI Na Bw.MAKONDA Na kumpongeza Makonda kwa Kazi nzuri, Mh.Kikwete Kampa UKUU WA WILAYA.

Hivi kwa akili yako na kwa uelewa wako unadhani Joseph Sinde Waryoba anaweza kumpigia debe Lowasa? Ni dhahili kwamba hata CCM wangempitisha Lowasa kamwe usingemuona Waryoba majukwaani. Na kama angeonekana majukwaani ni kumponda Lowasa na si Vinginevyo.
Na hata Mr Polepole kwa nilivyouona msimamo wake CCM ingempitisha Mh Lowasa nae asingethubutu kumpigia campaign. Ukweli ni ni kwamba chaguo la CCM ndiyo limepelekea wawili hao kuipipia CCM campaign.
 
Hakuna mzima CCM wamejaa wagonjwa mbona mgombea nae moyo mkubwa huo in uzima?
 
Jaji Warioba,Polepole Na Mzee Butiku Njaa in KALI wao in WASALITI WA KATIBA YAWATANZANIA ndio maana wameungana Na wale waliowatandika MAKOFI pale Ubungo Plaza Mbona mlisema mtazunguka nchi nzima kuwaambia wananchi jinsi CCM ilivyodharau maoni yao?
 
Jmi issue sio kumpigia MTU kampeni jitahidi kutumia akili japo kidogo issue in Rasimu ya katiba acha kukurupuka kinachozungumzwa in jinsi chama cha mafisadi CCM kilivyoyakataa maoni ya watanzania wenye nchi hii Na kuweka upumbavu wao kwenye katiba ya kipumbavu kama Mgombea urais Mzee Rungwe alivyoiita Na pia CCM kumtuma DC. Makonda kumzaba makofi Waziri mkuu mstaafu Mzee Warioba Na kupongezwa kwa kupewa UKUU WA WILAYA
 
Tony ufisadi in MTU Na pia in taasisi yake .Hao mnaowaita Leo mafisadi kabla hawajatoka CCM mlikuwa mnawaita nani? CCM in taasisi kubwa yenye sifa kubwa nchini Na nje ya nchi kwa Ufisadi je aliyomo ndani ya taasisi hiyo in msafi kwa uelewa wako mdogo? Kwa taarifa yako taasisi CCM in fisadi waliomo in mafisadi

Nawataendelea kuwa mafisadi tu, hata waende wapi, hakuna chakusafishwa wala nini
 
Jmi issue sio kumpigia MTU kampeni jitahidi kutumia akili japo kidogo issue in Rasimu ya katiba acha kukurupuka kinachozungumzwa in jinsi chama cha mafisadi CCM kilivyoyakataa maoni ya watanzania wenye nchi hii Na kuweka upumbavu wao kwenye katiba ya kipumbavu kama Mgombea urais Mzee Rungwe alivyoiita Na pia CCM kumtuma DC. Makonda kumzaba makofi Waziri mkuu mstaafu Mzee Warioba Na kupongezwa kwa kupewa UKUU WA WILAYA

we unazani Ukawa asahivi inaweza kuleta katiba ya wananchi...Ile inayokemea mafisadi,Ile inayotaka viongozi waadilifu,ile inayohitaji demokrasia ya kweli......Watachofanya nikuweka serikali tatu tu basi wawaridhishe kisha waaendelee na mambo yao....
 
Back
Top Bottom