Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Akizungumza kuhusu ujio wa Emmanuel Nchimbi baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Katibu Mkuu, Jaji Joseph Sinde Warioba amesema Nchimbi si mtu mgeni kwake na kwamba tayari alikuwa akimfahamu kutokana na kazi zake.
“Nchimbi anakifahamu chama na amefanya kazi. Alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu, ndiyo kwa mara ya kwanza alikuja kunitembelea,” amesema.
Akizungumzia ushauri aliowahi kumpa Nchimbi kuhusu mwenendo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema alimweleza mambo aliyokuwa akiyasisitiza kwa muda, ikiwemo umuhimu wa wanachama kukutana kwa mujibu wa kalenda ya chama.
“Mimi nilimwambia yale yale niliyokuwa nikisema kwamba sasa tumeachama kama hakipo kwa sababu wanachama wakutane. Zile kalenda zetu zilizokuwa zinafanya hazipo. Pili, rushwa iliingia kwenye chama,” amesema.
Aidha, amemkumbusha Mwalimu Julius Nyerere kuhusu umuhimu wa vijana kupewa nafasi ya kutoa mawazo yao ndani ya chama na katika masuala ya maendeleo ya nchi.
Soma Pia: Jaji Warioba: Kwa ninavyomfahamu Nchimbi siyo chawa, hata kwa matamko aliyokuwa akitoa
Amesema Mwalimu Nyerere aliwahi kusisitiza kuwa vijana wanapaswa kuzungumza na kutoa mawazo yao kwa sababu mabadiliko mara nyingi huanzia katika mawazo mapya ya kizazi kipya.