PreGE2025 Jaji Warioba: Uenguaji wa Wagombea kwenye chaguzi nje ya sababu za Msingi zilizo kwenye Katiba ya JMT umezidi

PreGE2025 Jaji Warioba: Uenguaji wa Wagombea kwenye chaguzi nje ya sababu za Msingi zilizo kwenye Katiba ya JMT umezidi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Waziri Mkuu na Jaji Mstaafu nchini Tanzania Joseph Sinde Warioba ameeleza kuwa mwaka 2019 na 2020 ndiyo miaka pekee ambayo ameshuhudia wagombea wengi zaidi wa Vyama vya siasa wakienguliwa kwenye ushiriki wa Uchaguzi Mkuu na ule wa serikali za mitaa, nje ya sababu za Msingi zilizo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Warioba amebainisha hayo leo Mei 03, 2025 kwenye kongamano la Uchaguzi Mkuu wa Tanzania lililoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), lililofanyika Jijini Dar Es salaam akieleza kwamba " ukienda kwenye sababu zilizowafanya kuenguliwa hakuna hata moja iliyo kwenye Katiba"

''2015 Kuna sababu Nyingi zilizofanya wagombea wakaenguliwa lakini zile hazikuwa na Misingi iliyoko kwenye sheria za Uchaguzi wala Katiba ya Nchi na ilileta Matatizo mengi kwenye uchaguzi wetu'' - Jaji Warioba

Kulingana na Mzee Warioba, Katiba kwenye suala la uchaguzi wa Wabunge lmeeleza sifa tatu pekee ya kuweza kukufanya uwanie ama usiwanie ubunge ambazo ni lazima uwe raia wa Tanzania na mwenye miaka zaidi ya 21, uwe mwanachama wa Chama cha siasa na uwe katika maisha yako hukuwahi kupatikana na hatia ya kukwepa kulipa kodi.
 
Piga spana Mzee! Chama kimevamiwa na majambazi. Ukiwaambia tu ukweli wanakutafuta ili wakutese, au kukuaa kabisa.
 
Back
Top Bottom