Jaji Warioba: Ukipewa nafasi ukaona inakuzidi sema atafutwe mwingine

Jaji Warioba: Ukipewa nafasi ukaona inakuzidi sema atafutwe mwingine

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Eid Mubarak Wanachama wa Jf na watanzania wote.

Ninaomba tujadili hii kauli ya Mzee wetu Jaji mstaafu Mzee Warioba.
Kuna eneo la msingi na LENYE maana kubwa kwetu sisi watanganyika kuelekea 2025.

Karibuni Kwa mjadala.

====


Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema viongozi wanaopewa fursa za kuongoza kwenye nafasi mbalimbali pindi wanapoona hawaziwezi wawe tayari kuziachia kwa manufaa ya taifa.

Jaji Warioba amesema yeye alifanya hivyo baada ya kutumikia nafasi ya uwaziri mkuu kwa kipindi cha miaka mitano ya utawala wa awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Amesema alifanya hivyo baada ya kuona amechoka na anahitaji kupumzika. Pia, uamuzi kama huo anasema uliwahi kufanywa na Edward Sokoine, akiwa waziri mkuu katika utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Julius Nyerere
https://www.mwananchi.co.tz/mw/haba...a-mambo-manne-yazingatiwe-katiba-mpya-4581602
Jaji Warioba: Ukipewa nafasi ukaona inakuzidi sema atafutwe mwingine

Jaji Warioba anatoa simulizi ikiwa sehemu ya safari ya uongozi wa uwaziri mkuu wa miaka mitano kuanzia Novemba 5, 1985 hadi Novemba 9, 1990 katika mahojiano maalum na gazeti hili, aliyoyafanya Aprili 5 mwaka huu ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Anasema katika kipindi chake cha uwaziri mkuu, baada ya miaka mitano kumalizika alimwomba Rais Mwinyi amruhusu kupumzika, asiendelee naye tena kwenye Baraza lake la Mawaziri kama waziri mkuu.

"Huwa nawaambia watu niliomba kupumzika lakini hawaamini, uzuri Mzee Mwinyi kwenye kitabu chake naye aliandika," amesema Jaji Warioba huku akitabasamu kwenye mahojiano hayo.

Kuhusu uamuzi huo, Jaji Warioba anasema hakutaka kuendelea na uwaziri mkuu baada ya kumaliza miaka mitano kutokana na ugumu aliopitia.

"Baada ya miaka mitano nilimwambia Rais, mimi tena basi tafuta mtu mwingine awe waziri mkuu. Nilikwenda kwa Rais nikamwambia Mzee, mimi nadhani sasa nipumzike pamoja na kwamba yeye (Rais) alitaka niendelee," anasema.

Anasema wakati ule ilikuwa ukipewa kazi kama unaiona unaiweza unafanya, huiwezi unakaa pembeni.

Jaji Warioba anatolea mfano mwingine wa Sokoine kuwa aliteuliwa kuwa waziri mkuu Februari 13, 1977 ilipofika Novemba 1980 yeye mwenyewe aliomba asiendelee.

"Mwalimu (Nyerere) alitaka aendelee naye, lakini yeye akaomba asiendelee apumzike. Baada ya miaka miwili Mwalimu akamrudia tena Sokoine,” anasema Jaji Warioba.

Sokoine alikuwa waziri mkuu kwa awamu mbili, Februari 13, 1977 hadi Novemba 7, 1980 kisha akaingia Cleopa Msuya. Baadaye Sokoine akarejeshwa tena Februari 24, 1983 hadi Aprili 12, 1984 alipofariki dunia kwa ajali ya gari.

Mzee Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29 mwaka huu, katika kitabu chake ‘Mzee Rukhsa- Safari ya Maisha Yangu’ kinachoelezea masuala mbalimbali, amegusia suala la Jaji Warioba akieleza namna alivyotaka kuendelea naye kama waziri mkuu huku yeye akiomba kuachia.

Katika sura ya 13 ukurasa wa 157 wa kitabu chake, Mzee Mwinyi anamshukuru Jaji Warioba aliyekuwa waziri mkuu wake wa kwanza baada ya kuingia madarakani 1985. Mwinyi anakanusha kile alichosema maneno ya watu kwamba ‘alimteua Jaji Warioba kuwa waziri mkuu kwa kulazimishwa na Mwalimu Nyerere.’

“Si, kweli, na waliosema hivyo ni wazi hawakumjua Mwalimu vizuri. Ni kweli kuna mambo nilikuwa nashauriana na Mwalimu; lakini Mwalimu hakuwa aina ya mtu wa kukulazimisha au hata kukuingilia kwenye kuunda timu yako ya uongozi.

“Mimi mwenyewe nilitaka kiongozi wa aina ya Warioba, na isingekuwa yeye mwenyewe kuomba kupumzika ningeweza kuendelea naye katika kipindi change cha pili,” anasema Mzee Mwinyi kwenye kitabu chake na kuongeza:

“Alipoomba kuondoka ilibidi nimuulize anitajie nafasi nyingine anayoweza kulisaidia Taifa. Hadi leo, naendelea kumshukuru kwa alivyonisaidia katika miaka mitano ya kwanza ya uongozi wangu wa Taifa letu.”

Kila siku ilikuwa ngumu

Jaji Warioba anaeleza kuwa kipindi chote cha miaka mitano ya mwanzo akiwa waziri mkuu nchi ilivyopita kwenye hali ngumu. Walipokea utawala kutoka kwa Mwalimu Nyerere aliyeamua kung’atuka madarakani na Mzee Mwinyi kushika uongozi.

"Tumeingia hatukuwa na uwezo, hatukuwa na fedha za kigeni, baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuvunjika, ilibidi tuanzishe mashirika mapya, yalitumia fedha nyingi," anasema Jaji Warioba aliyezaliwa wa Bunda, Mkoa wa Mara, Septemba 3, 1940.

"Kisha vikaja vita vya Uganda mwaka 1978, tukatumia akiba yetu yote kwenye vita, mwaka 1979 bei ya mafuta ikapanda.

Tumeingia hali ikiwa ni mbaya, hatuna mafuta ya kutosha, hatuna bidhaa madukani sababu hatukuwa na uwezo wa kununua, tuna njaa, ilikuwa ni kuhangaika, kurekebisha hayo kipindi chote kile nilipoingia kuwa waziri mkuu,” anasema

Jaji Warioba anasema, si kwenye uwaziri mkuu pekee, hata akiwa kwenye utumushi wa umma, matukio yalikuwa ni mengi.

"Kuanzia nilipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndipo Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika, ikabidi tuanzishe mashirika mapya, badaye nikawa waziri wa sheria. Hata Katiba hii tunayoizungumzia ya mwaka 1977 nikiwa mwanasheria mkuu tulipewa mwezi mmoja wa kuiandika,” anasema.

Anasema ni jambo ambalo lilizungumzwa kisiasa, mpaka chama kikaamua tunakuwa na Katiba mpya, wakati huo ilikuwa ni Tanu na ASP.

"Iliandikwa kwa mwezi mmoja, tena kwa Kiswahili, tuliyokuwa nayo kabla ilikuwa ni ya Kiingereza
Jaji Warioba anasema:"Hata nilipokuwa waziri mkuu, kulikuwa na matukio mengi tu, juzi juzi nilikuwa naangalia mafuriko ya Hanang, yalinikumbusha yaliyotokea Lindi na Mtwara mwaka 1990 nikiwa waziri mkuu."

Anasema alikwenda kuona madhara ambayo ukiacha miundombinu na madaraja makubwa vilivyosombwa na maji, alipofika Hospitali ya Ndanda, Padri wa pale akawa anamtembeza kwenye eneo ambalo lilibaki wazi.

"Aliniambia, pale kulikuwa na nyumba, nyingine ya bruda wao zimesombwa, na hata huyo bruda naye yuko humohumo kwenye maji, yapo hawajui ni wapi amenasa, tulipoteza watu zaidi ya 50,” anasimuliza Jaji Warioba
Anasema katika kipindi chake cha uwaziri mkuu kila siku ilikuwa ni ngumu.

"Ninachoshukuru tulikuwa na ushirikiano mzuri na timu ya washauri wa Rais ambaye pia alituamini tukaweza kusimamia mabadiliko. Kipindi chote cha Mwinyi kilikuwa cha mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa, kilikuwa kipindi kigumu, wakati ule itikadi zetu na sera zilikuwa ni ujamaa, hivyo kubadili kutoka comand economy (uchumi hodhi) kuja free market (soko huru) haikuwa rahisi,” anasema.

Mwalimu Nyerere awakingia kifua

Katika mahojiano hayo ya zaidi ya dakika 120,Jaji Warioba anasema wakati fulani mwaka 1967, yeye na wenzake vijana wasomi ndani ya Tanu walianzisha kitu kinaitwa study group.

Anasema vijana wa wakati ule akiwamo pia Kingunge Ngombale Mwiru kazi yao ilikuwani kuwa na mijadala kwenye suala fulani, kisha wanawasilisha mawazo yao kwenye chama.

"Ilifika mahali baadhi ya wazee wakawa wanaona hawa ni vijana wakorofi na wasaliti, wengine wakasema wanadhani tuadhibiwe au tufukuzwe kwenye chama.

"Aliyetuponya ni Mwalimu, alisema msishangae vijana kuwa na mawazo haya, akasema ukifika mahali ukute mawazo ya vijana yanafanana na ya wazee, ujue jamii ile imedumaa," anasema Jaji Warioba.

Anasema, Mwalimu aliwambia wale wazee kwamba, mabadiliko huwa yanaletwa na mawazo mapya na mawazo hayo yanatoka kwa vijana kwa kuwa wazee wanafanya vitu kwa mazoea.

"Hatukuwa tunatafuta vyeo, bali kutoa mawazo, tulijengwa vile kwa kutoweka tamaa ya cheo bali kupewa mafunzo ili uje uwe kiongozi mzuri, japo siku hizi wengi ni kama wanakazania vyeo," anasema.

Anasema, kwenye uongozi ni lazima vijana wapate uzoefu na mafunzo ili wakitoa mawazo yawe ni kwa nia ya kujenga.

"Siku hizi naona kama vijana wengi wanachotaka ni kuingia kule ili wapate nafasi," alisema Jaji Warioba akigusia mwelekeo wa vijana kupewa nafasi hivi sasa.

Anasema, hata wakati wao, Mwalimu Nyerere alitoa nafasi kwa vijana wengi.

"Mimi ni miongoni mwao, niliingia Baraza la Mawaziri mwaka 1976 nikiwa bado kijana wa miaka 35 nakwenda kufikisha 36.

"Baada ya uchaguzi wa 1975, Rais aliwapa nafasi vijana, alifanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri akaingiza vijana wengi, mmoja wetu alikuwa na miaka 24 au 25, wale wazee alioanza nao Mwalimu walibaki wachache, baadaye ndipo akawaleta vijana wengine kina (Benjamini) Mkapa na (Dk Salim Ahmed) Salim," anasema.

Anasema wakati Mwalimu Nyerere anakaribia kutoka madarakani alikuwa amebaki na wazee kama wanne alioanza nao.

“Alipokuwa anajiandaa kuondoka madarakani, Mwalimu akamteua Sokoine kuwa Waziri Mkuu, yeye naye alikuwa ni rika la vijana na hata utendaji kazi baada ya uteuzi huo ulibadilika,” anasema Jaji Warioba.

Maboksi mawili

Katika mahojiano hayo, Jaji Warioba anafananisha makundi mawili yanayopongeza viongozi na linalowapinga kama maboksi ambayo hayana afya kwa mustakabali wa Taifa.

“Siku hizi kuna maboksi, moja kazi yake ni kusifu na jingine ni la kupinga tu. Sio kila kitu ni kusifu tu, hasa ili la kuwasifu viongozi, inafikia mahali unajiuliza hizi ni sifa kweli au kujipendekeza! Kuna boksi jingine nalo ni kupinga, kupinga kila kitu,” anasema akionyesha kuchukizwa.

Anasema kuna mambo kama Taifa ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo, mnaweza kutofautiana lakini kama taifa mnakaa na kukubaliana jinsi ya kulitekeleza kwa manufaa ya nchi.

Alitolea mfano, ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere kuwa ni mradi mzuri wenye tija kwa Taifa ambao kila mmoja angeweza kushiriki kwa mawazo ili kufikia lengo kama nchi.

"Tunajua ni muhimu tuwe na nishati ya kutosha, Bwawa la Nyerere ni jambo la kitaifa, japo tunaweza kuhitilafiana namna ya kulitekeleza, lakini ni la kitaifa, au reli ya kisasa kuna vitu vya kitaifa vinahitaji majadiliano ya pamoja sio kupinga tu," anasema.

Anasema, siku hizi siasa imekuwa kama ni watu, akitolea mfano miaka ya nyuma nchi ilikuwa inafanya mambo yake na kupongezwa na wengine.

"Tanzania ilikuwa inasifika sana kwa kuwa ilifanya mambo yake kwa msingi wa kitaifa, haikuwa ikijitangaza. Siku hizi tunajisifu sana, lakini huoni hizo sifa zinatoka nje, tunabaki tunajisifu wenyewe.

Mimi nadhani ama ni kusifu au ni kupinga, ikifika kwenye mambo ya kitaifa tuwe na mijadala ya pamoja, lazima tujue sisi ni Watanzania hata kama tuna mawazo tofauti tuzungumze tukubaliane masuala ya kitaifa," anasema.

Mwananchi
 
Eid Mubarak Wanachama wa Jf na watanzania wote.

Ninaomba tujadili hii kauli ya Mzee wetu Jaji mstaafu Mzee Warioba.
Kuna eneo la msingi na LENYE maana kubwa kwetu sisi watanganyika kuelekea 2025.

Karibuni Kwa mjadala.
Tujadili nini na yeye katowa mawazo yake?
 
Anasema vijana wa wakati ule akiwamo pia Kingunge Ngombale Mwiru kazi yao ilikuwani kuwa na mijadala kwenye suala fulani, kisha wanawasilisha mawazo yao kwenye chama.

"Ilifika mahali baadhi ya wazee wakawa wanaona hawa ni vijana wakorofi na wasaliti, wengine wakasema wanadhani tuadhibiwe au tufukuzwe kwenye chama.

"Aliyetuponya ni Mwalimu, alisema msishangae vijana kuwa na mawazo haya, akasema ukifika mahali ukute mawazo ya vijana yanafanana na ya wazee, ujue jamii ile imedumaa," anasema Jaji Warioba.

Anasema, Mwalimu aliwambia wale wazee kwamba, mabadiliko huwa yanaletwa na mawazo mapya na mawazo hayo yanatoka kwa vijana kwa kuwa wazee wanafanya vitu kwa mazoea.

UVCCM wamefanana mawazo na wazee, kuunga mkono juhudi, kuwa machawa, kubeba mabango ya zidumu fikra kazi iendelee n.k

UVCCM hawana mawazo mbadala

KUTOKA MAKTABA:

VIJANA NA MABADILIKO, WAKATI HUU NI SAHIHI KUINGIA KTK NAFASI ZA MAAMUZI IKIWEMO URAIS


Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi, Vijana ni taifa la leo, watoto ndiyo viongozi wa kesho. Kauli za kilaghai kuwa vijana ni kwa ajili ya taifa la kesho siyo sahihi.

Vijana msihofu msuguano na wazee waliopo mamlakani, kusubiri kupewa ni kukubali kuwa tumejumuishwa na watoto chipukizi. Ni wakati wa vijana kuchagiza kwa mbinyo wa hoja kuwa uongozi wa nchi ni kwa ajili ya vijana.

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja kongwe, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhisha wananchi kama bandari kuchukuliwa kuwa vituo vya nchi ngeni, matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo zilizokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Huko Chile marekani ya kusini nchi iliyo viongozi wa vyama vya wanafunzi wenye kushiriki kikamilifu katika siasa pia maandamano imewezesha kiongozi kijana wa wanafunzi Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Gabriel Boric on the Chilean Student Movement:
59,554Views :2017 14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:

Department of Public Policy at CEU​

Mwanafunzi wa chuo kikuu Tanzania toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa anaimani na matumaini potofu ya Ilani ya CCM imeandika ahadi ya mambo ya uongo ya kupata ajira, mazingira ruhani kuwa wataweza kupata vyeo vya ulaji vya kisiasa UVCCM, kuwa MNEC Halmashauri Kuu ya CCM, mbunge wa CCM n.k au kuwepo mazingira (hewa) ya kujiajiri.
1712733445092.png


Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.

25 March 2024
Muheza, Tanga

Bi Yosefa Komba wa CHADEMA jimbo la Muheza azungumza mazito ktk mkutano mkubwa​


CHADEMA YAONGEA KUPITIA MKUTANO NA WANANCHI WA MUHEZA

View: https://m.youtube.com/watch?v=23VjK8gouCg

Kamanda Yosefa Komba aitisha mkutano kuzungumza na wananchi wanaokabiliwa na changamoto nyingi ambazo hazifuatiliwi na mkurugezi wa wilaya wala mbunge wa sasa aliyeingia kupitia uchaguzi uliovurugwa 2020
Source : RAI TV

Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Mimi nimemuelewa,

Mitano ya Sa100 inatosha, apumzike,

Umri wa kustaafu pia umefika 65yrs.

Kurudia Yale ya 2020 tena Kwa Sheria mbovu zaidi kuliko Ile, haikubaliki.

Kuuingia uchaguzi bila Tume HURU na Katiba mpya ni mtihani mkubwa Kwa USALAMA wa Nchi yetu.

Kuendelea na kiongozi anayeamini Watanzania hawawezi kusimamia raslimali zao Kwa Kugawa Bandari zetu haikubaliki.

Kiongozi anapokea ndege mpya zinapakiwa BILA mpango madhubuti kuhakikisha Nchi inapata Utalii kupitia ndege hizo ni mkwamo huo,

Kuendelea na kiongozi anayepokea Ripoti za CAG Kisha kuzitupa kapuni haikubaliki.

Kuendelea na kiongozi ambaye anaamini katika kukopa pekee haikubaliki.

Shilingi ya kitanzania inazidi kudidimia, mabadiliko ya kiuongozi yanahitajika haraka.

Bima za watoto chini ya miaka 5 zimefutwa, wakati huo huo wake wa viongozi wakilipwa, umama wa kiongozi u wapi?

Mitano ya Magu, ihitimishwe na mitano ya sa100, Kisha Utaratibu wa 10 yrs uendelee!!
 
Mimi nimemuelewa,

Mitano ya Sa100 inatosha, apumzike,

Umri wa kustaafu pia umefika 65yrs.

Kurudia Yale ya 2020 tena Kwa Sheria mbovu zaidi kuliko Ile, haikubaliki.

Kuuingia uchaguzi bila Tume HURU na Katiba mpya ni mtihani mkubwa Kwa USALAMA wa Nchi yetu.

Kuendelea na kiongozi anayeamini Watanzania hawawezi kusimamia raslimali zao Kwa Kugawa Bandari zetu haikubaliki.

Kuendelea na kiongozi anayepokea Ripoti za CAG Kisha kuzitupa kapuni haikubaliki.

Kuendelea na kiongozi ambaye anaamini katika kukopa pekee haikubaliki.

Bima za watoto chini ya miaka 5 zimefutwa, wakati huo huo wake wa viongozi wakilipwa, umama wa kiongozi u wapi?

Mitano ya Magu, ihitimishwe na mitano ya sa100, Kisha Utaratibu wa 10 yrs uendelee!!
Unguja leo
 

Attachments

  • VID-20240410-WA0034.mp4
    4.3 MB
Kuwapata watu wa aina ya Warioba au Mwinyi ndani ya CCM kwa sasa, ni kitu ambacho hakiwezekani.

Hata chawa ambaye hana uwezo kabisa akipewa nafasi yoyote ile hawezi kutamka kuwa hana uwezo.
 
Kuendelea na kiongozi ambaye anaamini katika kukopa pekee haikubaliki.
Kama wewe ni mfanya biashara utanisamehe; lakini Samia ni kama kiongozi aliyepo usingizini akiota. Ndoto moja inamwambia TRA isiwasumbue wafanya biasharai. Hiyo ikipita inamjia nyingine akiota kuhusu udanganyifu wanaofanya wafanya biashara hao kukwepa kulipa kodi stahiki!

Huyu ni kiongozi anayeyumba na upepo, hajui asimamie wapi.
 
"Tanzania ilikuwa inasifika sana kwa kuwa ilifanya mambo yake kwa msingi wa kitaifa, haikuwa ikijitangaza. Siku hizi tunajisifu sana, lakini huoni hizo sifa zinatoka"

Chema chajiuza, leo ukipita kila kona ni mabango yanayotangaza sifa hewa.
 
Kama wewe ni mfanya biashara utanisamehe; lakini Samia ni kama kiongozi aliyepo usingizini akiota. Ndoto moja inamwambia TRA isiwasumbue wafanya biasharai. Hiyo ikipita inamjia nyingine akiota kuhusu udanganyifu wanaofanya wafanya biashara hao kukwepa kulipa kodi stahiki!

Huyu ni kiongozi anayeyumba na upepo, hajui asimamie wapi.
Hapa tulipigwa haswa
 
Back
Top Bottom