Pre GE2025 Jaji Warioba: Waliosimamia Uchaguzi wa 2019 na 2020 wataendelea na je wanaaminika?

Pre GE2025 Jaji Warioba: Waliosimamia Uchaguzi wa 2019 na 2020 wataendelea na je wanaaminika?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema Chaguzi za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 zilikuwa kama ajali kwasababu hazikuwa katika utaratibu wa kawaida ikiwemo Mawakala kusambaratishwa wakati wa Kuhesabu Kura

Ameongeza kuwa hali hiyo imeanza kuibua hoja na maswali kuhusu kuaminika kwa waliosimamia Chaguzi hizo mwaka 2019 na 2020 na kama wataendelea kusimamia tena Chaguzi zinazokuja

Mwaka huu na mwakani kama kawaida hakuna uchaguzi ni kupoteza muda na fedha tu,kama mtu anasema wao kushinda ni lazima siyo mpaka Mungu apende,na mwingine anasema kushinda kwao kunategemea nani anahesabu kura na kutangaza matokeo na mwingine tena anasema watawapeleka watu maporini kwenda kuwashughulikia hapo unategemea nini!
 
Huyu mzee apewe cheo akae kimya sasa maana bila shugli huwa hatulii kabisa

USSR
Sidhani kama uzee wake unahusiana na kutaka cheo, au na hicho alichokiongea. Je, alichosema ni kweli, au ni uongo?
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema Chaguzi za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 zilikuwa kama ajali kwasababu hazikuwa katika utaratibu wa kawaida ikiwemo Mawakala kusambaratishwa wakati wa Kuhesabu Kura

Ameongeza kuwa hali hiyo imeanza kuibua hoja na maswali kuhusu kuaminika kwa waliosimamia Chaguzi hizo mwaka 2019 na 2020 na kama wataendelea kusimamia tena Chaguzi zinazokuja

View attachment 3100469
Mzee mkweli sana huyu.
Inasikitisha sana
 
Huyu mzee apewe cheo akae kimya sasa maana bila shugli huwa hatulii kabisa

USSR
Kwa hiyo tuseme uwezo wako wa kufikiria ndo umeishia hapa. 🤔🤔. ( ukipewa cheo hutakiwi kutulia, unatakiwa kutumikia taifa).
 
Back
Top Bottom