- Source #1
- View Source #1
Kumekuwepo na graphic inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, alisema:"Usitegemee katiba mpya sasa hivi. Watanzania tunatakiwa tujikite katika kujenga nchi yetu."
Katika ufuatiliaji uliofanywa kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya mtandaoni, ikiwemo hotuba, mahojiano na taarifa rasmi zinazopatikana hadharani, hakuna ushahidi unaothibitisha kuwa Jakaya Kikwete aliwahi kutoa kauli hiyo.
Sambamba na hilo graphic hiyo potoshi imeambatana na ujumbe ufuato kikwete ukiona mtu anazungumzia katiba mpya chunguza akili zake haziko sawa Tanzania nchi ya amani
Aidha, hakuna taarifa rasmi, rekodi za vyombo vya habari, wala hotuba zinazomnukuu Kikwete akisema maneno hayo. Hivyo, graphic hiyo inapotosha uhalisia kwa kumhusisha na kauli ambayo haijathibitishwa.
Uchunguzi pia umebaini kuwa graphic hiyo imeunganishwa na kiungo (link) kinachowashawishi watumiaji kukifungua, lakini badala yake huwapeleka kwenye maudhui yanayohusu tiba za asili.
Hali hiyo inaashiria kuwa graphic hiyo inaweza kuwa imetengenezwa kwa lengo la kuvutia watu kufungua kiungo hicho kwa kutumia taarifa ya kupotosha.
Madai hayo yameanza kusambaa wakati kukiwa na mjadala kuhusu Katiba Mpya, kufuatia kauli iliyotolewa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu umuhimu wa kuendelea na jitihada za kupatikana kwa Katiba Mpya.