Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education (GPE) ameongoza Vikao vya Bodi ya Taasisi hiyo vinavyofanyika Jijini Paris, nchini Ufaransa kuanzia tarehe 5 hadi 7 Disemba, 2022.
Vikao hivyo ni vya kwanza vya ana kwa ana tangu dunia ilivyokumbwa na ugonjwa wa COVID-19 mwishoni mwa mwaka 2019.
Katika vikao hivyo, Taasisi ya GPE inapitia na kuazimia masuala mbalimbali yatakayolenga kuboresha mifumo ya elimu katika nchi zinazoendelea ikiwemo kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu, wakiwemo watoto wa kike, na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa elimu.