Jakaya Kikwete awasili Ufaransa kuongoza vikao vya Bodi ya Global Partnership for Education

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, amewasili leo Juni Mosi, 2026 nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi ya kushiriki na kuongoza vikao vya Bodi ya Global Partnership for Education (GPE), taasisi ya kimataifa inayojihusisha na maendeleo ya elimu duniani, ambako anahudumu kama Mwenyekiti wa Bodi.
Kikwete alipokewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Charles De Gaulle na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Saidi Othman Yakubu, pamoja na watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Bodi ya GPE, Kikwete anaongoza juhudi za kimataifa zinazolenga kuimarisha upatikanaji wa elimu bora, jumuishi na yenye usawa kwa watoto katika nchi zinazoendelea. GPE ni ushirikiano wa kimataifa unaozileta pamoja serikali, mashirika ya maendeleo, sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine wa elimu ili kusaidia nchi zenye kipato cha chini na cha kati kuboresha mifumo yao ya elimu.

Kupitia ushirikiano huo, GPE hutoa msaada wa kifedha na kiufundi kwa nchi washirika ili kuongeza upatikanaji wa elimu ya msingi na sekondari, kuboresha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, kuimarisha usawa wa kijinsia katika elimu, pamoja na kuhakikisha watoto walio katika mazingira magumu wanapata fursa ya elimu.

Screenshot 2026-06-01 193024.png
 
So what?
 
Kula maisha nchi yako inateketea kwa rushwa, wauaji n utekaji.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom