Jakaya Kikwete kuanzisha Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Julius Nyerere

Jakaya Kikwete kuanzisha Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Julius Nyerere

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
4,465
Reaction score
1,171
Katika hotuba yake ya shukrani ambayo pia ilieleza mikakati ya serikali ya awamu ya nne katika kipindi kijacho cha miaka mitano, Rais Kikwete alisema kuwa atajenga makao makuu ya CCM ambayo yatakuwa ni ukumbi mkubwa utakaowawezesha kufanya vikao kwa usalama na utulivu.

Kwa sasa CCM inatumia majengo ya tawi la chama hicho mkoani Dodoma kuwa ofisi zake za makao makuu na hutumia ukumbi huomwa Kizota, ambao ulikuwa ghala la nafaka kufanyia mikutano yake mikuu.

Kikwete pia alisema kuwa katika kipindi hicho cha miaka mitano ijayo, atajenga Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Julius Nyerere mkoani Mara.
Awali, kabla ya Kikwete kupigiwa kura na Shein kuthibitishwa, ulisomomwa wasifu wa mgombea huyo na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru alisoma mwelekeo wa sera.

Wakuu hivi hivi vyuo vikuu vinavyoahidiwa na JK ni mipango iliyofanyiwa utafiti au siasa. SUA inasua sua lakini tunaambiwa kuna chuo kikuu cha kilimo kingine kitajengwa. UDSM iko hoi mpaka wanaomba michango ya kupaka rangi majengo lakini JK anawaza chuo mpya.

Tukisema JK hajafanya lolote kwenye infrastructure tunaambiwa anaendeleza zile za awamu ya tatu......... Sasa mbona vyuo haendelezi kama ilivyokuwa imekusudiwa?????? Mbeya Tech ilikuwa ndiyo iwe chuo kikuu cha ufundi nchini lakini hiyo hapana kuendeleza I think kwa JK ni politically incorrect. Leo tunazungumzia Hikichuo kipya. Hivi huyu jamaa huwa anafikiri kabla ya maamuzi ya aina hii kweli?????
 
Alikuwa amesahau akakumbuka....... This is important to note, usipoteze muda wako
 
Alikuwa amesahau akakumbuka....... This is important to note, usipoteze muda wako

Unajua it is just pathetic, huyu jamaa anweza hata kutuahidi kwamba ataanzisha space exploration in those next five years!
 
[/COLOR]

Wakuu hivi hivi vyuo vikuu vinavyoahidiwa na JK ni mipango iliyofanyiwa utafiti au siasa. SUA inasua sua lakini tunaambiwa kuna chuo kikuu cha kilimo kingine kitajengwa. UDSM iko hoi mpaka wanaomba michango ya kupaka rangi majengo lakini JK anawaza chuo mpya.

Tukisema JK hajafanya lolote kwenye infrastructure tunaambiwa anaendeleza zile za awamu ya tatu......... Sasa mbona vyuo haendelezi kama ilivyokuwa imekusudiwa?????? Mbeya Tech ilikuwa ndiyo iwe chuo kikuu cha ufundi nchini lakini hiyo hapana kuendeleza I think kwa JK ni politically incorrect. Leo tunazungumzia Hikichuo kipya. Hivi huyu jamaa huwa anafikiri kabla ya maamuzi ya aina hii kweli?????

Mkuu baada ya hapa, usishangae kusikia ili kuweza kukidhi haja y akutosheleza walimu katika vyuo vikuu, wanaweza kuanzisha "crash program" ya walimu wa vyuo vikuu. Tukapata lecturers voda vasta kama secondary za kata!!!

Hii ndo CCM bana!!!!
 
Ofcourse kwa mwendo huu lolote linaweza kutokea!
 
Jamani, basi. Imetosha!
Kila kitu kinapewa jina la Mwl Nyerere?
Bado tu hatujaambiwa waTanzania wote tutumie jina la ukoo la Nyerere.
Sawa alifanya mambo mengi, lakini hakuwa mwenyewe, na majina ya wengine yatumike sasa
 
Miaka si Mingi utajikuta tunafikia kule walikokuwa winigeria . sijui kama ni kweli kuwa unaweza kukuta professor wa uchumi kaajiriwa kama cashier kwenye taasisis fulani.

Sijui kama maamuzi haya yanaendana na upembuzi yanikinifu wa mahitaji ya kweli ya Taifa na unalenga kuzalisha balanced working force.Binafsi naona kuna gap ya kutoa middle class working force ambayo ni muhimu kwenye taifa lolote lile.

Hatuna vyuo vya kufundisha social skilss malezi ya watoto, wazee, walemavu , wenye matatizo ya akili
Hatuna vyuo bora vya kuoa technical skill za mambo ya kama ya kutengeneza kukarabiti ( Simu,kompyuta. TV,) kuejenga nyumba, na Auto mechanical.
Hatuna chuo cha Michezo kuwa kuendeleza vipaji kama kikimbia, mpira tennis.

Nadhani inabidi tubadilike matatizo yetu hayataisha kwa kila mtu kuwa na degree. Tunahitaji na tuna uhaba wa qualified skiled front line woking personnel.

Mwisho wa siku wanaaliza serikali inasema wasisubiri kuajiriwa wajiajiri wakati serikali yenyewe ndo inaendekeza white collar jobs

IFM iwe chuo Kikuu,Dar Tech iwe chuo kiku baadae Chuo cha usafirishaji kiwe chhuo kikuu . Chuo cha Maji na Veta nazo zitaomba nazo kuwa vyuo vikuu.
 
hahahaaaaaaaaah! anataka kutekeleza sera yake ya kilimo kwanza lol.
@MTAZAMAJI: kuhusu chuo cha maji mbona kiko kwenye mchakato huo? muda si mrefu na chenyewe kitaanza kutoa degree
hivi tu vilivyopo hata mikopo kuwapatia inakuwa tabu bado anata kuongeza vingine!!!? hizi siasa zetu hizi!!!?:A S-confused1:
 
SIO mbaya kama pesa itatoka mfukoni kwake, kwa kodi zetu HAPANA.
 
Mheshimiwa Rais wetu sijui kama ana advisors. Sijui kama ana speech writer wanaojua nchi na dunia.
Nikifikiria miaka 5 tena chini ya JK nakata tamaa. Yaani mzee anasema chochote kijacho mdomoni,kama wanadamu tungekuwa na machujio ya kauli mzee wetu lake lingekuwa limetoboka vibaya sana.
Chuo kikuu cha Kilimo!!! kwani SUA kimefika wapi,hivi wafadhili wakiondoka si chuo basi. Tena kinafanya vizuri sana katika utafiti, sasa hiki cha musoma ni cha nini tena, yaani yote haya ni kutaka jimbo la tarime!
Watanzania, 5 yrs na huyu bwana ni 20 yrs kurudi nyuma.

fikiria haya!
Computer kila shule ya msingi wakati hakuna dawati wala paa darasani!!!!!!!!
Maisha bora kwa kila mtanzania,inflation na uchumi zero
Jengeni flyover dar, hata bila ya technical advice. Kaibuka tu toka ikulu likamtoka mzee wetu.

so sad.
 
Ni kweli Kikwete katangaza kujenga Chuo kikuu. Lakini labda angeweza kusema kuwa katoa kibali.
Maana wajenzi ni Mkono na wahisani marafiki wa nyerere. Ndio maana kinaitwa Chuo kikikuu cha kilimo na ujamaa na kujitegemea
 
Mkuu baada ya hapa, usishangae kusikia ili kuweza kukidhi haja y akutosheleza walimu katika vyuo vikuu, wanaweza kuanzisha "crash program" ya walimu wa vyuo vikuu. Tukapata lecturers voda vasta kama secondary za kata!!!

Hii ndo CCM bana!!!!

Mkuu huko ndiko tunakokwenda. Hukumsikia katika hotuba yake kuwa ameanzisha MEM ya Health Sector na next move ni voda MEM ya madaktari?
kwake hakuna linaloshindikana! too pathetic!!!!
 
Mheshimiwa Rais wetu sijui kama ana advisors. Sijui kama ana speech writer wanaojua nchi na dunia.
Nikifikiria miaka 5 tena chini ya JK nakata tamaa. Yaani mzee anasema chochote kijacho mdomoni,kama wanadamu tungekuwa na machujio ya kauli mzee wetu lake lingekuwa limetoboka vibaya sana.
Chuo kikuu cha Kilimo!!! kwani SUA kimefika wapi,hivi wafadhili wakiondoka si chuo basi. Tena kinafanya vizuri sana katika utafiti, sasa hiki cha musoma ni cha nini tena, yaani yote haya ni kutaka jimbo la tarime!
Watanzania, 5 yrs na huyu bwana ni 20 yrs kurudi nyuma.

fikiria haya!
Computer kila shule ya msingi wakati hakuna dawati wala paa darasani!!!!!!!!
Maisha bora kwa kila mtanzania,inflation na uchumi zero
Jengeni flyover dar, hata bila ya technical advice. Kaibuka tu toka ikulu likamtoka mzee wetu.

so sad.

washauri ni akina January Makamba>>>>what product can you expect?
 
Kikwete pia alisema kuwa katika kipindi hicho cha miaka mitano ijayo, atajenga Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Julius Nyerere mkoani Mara.

Naomba ufafanuzi, je ni serikali itajenga au JK atajenga nikisoma between lines ni kama vile yeye raisi ndo atajenga. What is the position?
 
Hii ahadi mbona haisikiki tena??????????????????? Au sio vote attracting???????????
 
And now we have this one:

Chuo kikuu cha kilimo kujengwa Katavi

Na Mwandishi Maalumu

MIPANGO inaandaliwa kujenga chuo kikuu kipya cha kilimo katika mkoa mpya wa Katavi katika jitihada za kuwapata wataalamu zaidi wa kilimo nchini.Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, ambaye aliwasili kijijini kwake Kibaoni, Wilayani Mpanda juzi kwa ziara fupi ya mapumziko ya Pasaka, anatarajiwa kukutana na wadau wa ujenzi wa chuo hicho kesho, kwa mujibu wa ratiba ya ziara yake.

Kikikamilika chuo hicho kitakuwa cha kwanza katika eneo la Nyanda za Juu za Kusini Magharibi, zinazohusisha mikoa ya Rukwa na mkoa mpya wa Katavi, maeneo ambayo ni mashuhuri kwa kilimo, hasa cha mahindi.

Akiwasalimu wananchi katika Tarafa ya Inyonga, aliposimama akiwa njiani kutoka Tabora kwenda wilayani Mpanda kwa barabara, Bw. Pinda alisema anafurahi kuwa wadau wamejitokeza kujenga Chuo Kikuu Katavi wakati mkoa mpya unaanza.

Alisema mkoa wa Katavi unatarajiwa kuanza rasmi baada ya Julai Mosi wakati taratibu za bajeti yake, pamoja na ya mikoa mingine mipya iliyotangazwa kuwa itaundwa, itakapokuwa imekwishapangwa.

Mikoa mingine mipya ni Njoluma (kwa kuunganisha Wilaya za Njombe, Ludewa na Makete), Geita (kuunganisha maeneo ya Wilaya Geita na meneo ya Kagera na Shinyanga) na Simiyu (kuunganisha maeneo ya mkoa wa Shinyanga na ya mkoa wa Mwanza).

Mapema, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya cha Tarafa ya Inyonga, kitakachokuwa na vitanda 224, maabara, vyumba vya upauaji, chumba cha maiti na nyumba 14 za watumishi, kitakachogharimu Sh. bilioni moja na laki sita. Kituo cha Afya cha Tarafa hiyo sasa kina vitanda 25 na majengo chakavu.

Alisema Kituo hicho kitakapokamilika na Inyonga itakapokuwa Wilaya chini ya Mkoa mpya wa Katavi, kinaweza kupandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Wilaya.
 
Back
Top Bottom