benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amesema utoaji mikopo zaidi kutoka taasisi za kifedha zikiwemo benki, utachochea uwekezaji na ukuaji wa uchumi kupitia sekta mbalimbali zikiwemo biashara na kilimo nchini.
Kikwete alisema uimara wa taasisi za fedha nchini kwa sasa utasaidia zaidi ukuaji wa uchumi kwa kuwa wawekezaji kwenye sekta za biashara na kilimo wanategemea zaidi taasisi hizo ili kufanikisha uendeshai. wa miradi yao.
Akizungumza kwenye hafla ya futari iliyondaliwa na Benki ya NBC kwa wateja wake mwishoni mwa wiki, Kikwete alieleza kuridhishwa na uimara wa taasisi za fedha nchini akitolea mfano benki hiyo inayomiliki mali zenye thamani ya Shi.52 trilioni na amana zenye thamani ya Shl.96 trilioni.
"Hakuna uchumi bila uwekezaji kama ambavyo hakuna uwekezaji bila mikopo ya uhakika kutoka taasisi za kifedha. Pamoja na taasisi nyingine za kifedha ninawasihi mwendelee kuwa karibu na wawekezaji kwa faida ya ukuaji wenu kama wakopeshaji, pia na kwa faida ya wawekezaji wenyewe, jamii pamoja na Serikali kwa ujumla," aliongeza Kikwete.