Kila kona taifa limeoza kwa ufisadi, leo hakuna uhakika wa umeme, shirika linapata hasara kwa kulipa madeni kutokana na mikataba ya hovyo ukiwemo wa RICHMOND sijui DOWANS ambao ulipelekea Lowassa kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi.
Kila mahali kunanuka ufisadi, watoto vyuo wanaishi maisha magumu kisa watu wanatafuta pesa, watu wanakufa hospitalin kisa huduma mbovu ama hakuna kabisa. Vijana hawana mitaji ili kuinua maisha yao.
Yote hii ni kutokana na ufisadi, na wote wanaoukumbatia hawapaswi kupewa heshima ya kuzikwa kishujaa na taifa wakati wao ndio wameliangamiza taifa, familia zao zinaishi vizuri, utajiri wa taifa wamerithisha familia zao na koo zao.